Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Barcelona wanamtaka kiungo wa Man City, Rodri

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Chelsea wako tayari kuidhinisha uhamisho wa mkopo kwa winga wake raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 25 Mykhaylo Mudryk, huku Coventry City ikiwa moja ya klabu tatu za Ligi Kuu England zikimtaka. (Football London)

Barcelona wana matumaini ya kumsajili kiungo wa Manchester City na Uhispania Rodri, 30, kwa kutoa ofa ya pili yenye thamani ya pauni milioni 51.3. (Times)

Inter Milan wako kwenye mazungumzo na Tottenham kuhusu mpango wa kumsajili beki wa kulia wa Uingereza, Djed Spence kwa euro milioni 30 (£25.6m), huku mchezaji huyo wa miaka 26 akitaka kuhamia kwa mabingwa wa Serie A. (Athletic)

Manchester United wanampa kipaumbele beki wa kushoto wa Newcastle, Lewis Hall, huku mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 pia akipendelea kuhamia Old Trafford. (Sun)

Chelsea na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati raia wa Uingereza, Myles Lewis-Skelly huku Arsenal ikiweza kushawishika kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 baada ya kuwasili kwa mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Bruno Guimaraes, 28, kutoka Newcastle . (Football London)

Manchester United wanafikiria kutoa dau la kwanza kwa beki wa kushoto wa Club Brugge, Joaquin Seys, mwenye umri wa miaka 21 na thamani ya pauni milioni 30. (Mirror)

Manchester United pia ilitaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil, Endrick, 20, kwa mkopo lakini meneja Jose Mourinho anataka kumbakisha katika timu hiyo ya Uhispania baada ya msimu huu wa joto. ( Mirror)

Napoli wana mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji raia wa Brazil, Gabriel Jesus lakini Arsenal itafikiria kumuuza mchezaji huyo wa miaka 29 tu ikiwa ofa zitaanza kwa euro milioni 20. (Caught Offside)

Iliman Ndiaye amekataa ofa ya kuhamia klabu ya Saudi Pro League, Al-Hilal , huku winga huyo wa Everton na Senegal, 26, akitaka kuendelea na Ligi Kuu England. (Fabrizio Romano)

Everton wanataka kusajili beki wa kulia katika siku saba hadi 10 zijazo, huku Alistair Johnston 27 wa Celtic na Canada, Aaron Wan-Bissaka 28 wa West Ham na DR Congo, na Mwingereza Brooke Norton-Cuffy wa Genoa, 22, wakiwa miongoni mwa walengwa. (The I)

Beki wa kati wa Crystal Palace , Mofe Jemide, mwenye umri wa miaka 19, anakaribia kuhamia Alverca katika ligi kuu ya Ureno. (Sky Sports)