Viumbe 10 vyenye sura mbaya zaidi duniani

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 6

Sio viumbe vyote vina sura nzuri. Ikiwa utawaita wanyama wabaya au viumbe vyenye changamoto ya urembo, bado kuna aina nyingi za wanyamapori wa kuvutia Duniani.

kuna spishi nyingi porini, kuanzia misitu hadi baharini, ambazo zina kile ambacho sisi wanadamu tunaweza kukiona kuwa sio sura ya kawaida.

Watu wengi huvutiwa na wanyama wenye sura kama za watoto - fikiria macho makubwa, pua ndogo, nyuso za mviringo. Ni kwa sababu tunawajali watoto wetu.

Lakini upendeleo huo huathiri jinsi tunavyowaona wanyama. Wanyama ambao si 'wazuri' mara nyingi hawazingatiwi sana na hawapewi ulinzi wa kutosha.

Hawa ndio wanyama ‘wabaya’ zaidi duniani.

Komba wa Madagascar (Aye-aye)

Ana vidole vyake virefu, manyoya meusi na meupe, meno kama panya, na macho ya duara, aye-aye ana mwonekano wa kipekee.

Anafanana na komba, lakini huyu asili yaj Madagascar. Aye aye myama wa usiku, huwinda kwa kugonga miti yenye mashimo hadi mara nane kwa sekunde, huwinda kwa kutumia midundo, ili kupata wadudu wanaojificha.

Bahati mbaya, aye-aye yuko hatarini kutoweka, kwani makao yake ya msitu yamekatwa sana. Pia amekuwa akiwindwa kwa sababu ya ushirikina, kwamba ni ishara ya kifo na uovu.

Spishi hiyo hapo awali ilidhaniwa kuwa imetoweka kabla ya kugunduliwa tena 1957. Leo kuna sheria maalum zimewekwa ili kuwalinda.

Nyani aina ya Proboscis

Nyani wa Proboscis ni mmoja wa nyani wa kipekee zaidi duniani, na si kwa sababu tu ya pua yake kubwa, ambayo inaweza kukua hadi sentimita 17 (inchi 7). Ana manyoya pia, mwekundu kichwani na mwili wa kahawia, na kijivu kwenye miguu yake.

Nyani wa Proboscis pia ni mwogeleaji mzuri, kutokana na miguu yake kama ya bata, na ana uwezo mzuri wa kukimbia mamba ndani ya maji.

Nyani huyu huenda asifae mgeni wa sherehe ya chakula cha jioni mwenye adabu zaidi - hububujika mara kwa mara tumbo lake lenye vyumba linapochachusha chakula chake. Hupiga mbweu mara kwa mara wakati anaposaga chakula.

Nyani wa Proboscis dume wana pua kubwa zaidi kuliko jike, na kadiri pua inavyokuwa kubwa, ndivyo wanavyoonekana kuvutia zaidi. Pua kubwa hutumika kama ishara ya afya na nguvu, na kuongeza nafasi za dume za kupata jike.

Panya aina ya naked mole

Panya wa aina hii ana mwili wenye mikunjo na meno makubwa ya manjano, kwa sababu hiyo huenda hatashinda tuzo ya uzuri.

Lakini kuhukumu panya huyu kwa mwonekano wake pekee kutamaanisha unapuuza baadhi ya mambo mengine ya kuvutia zaidi ya kiumbe huyu mdogo.

Kwa mfano, panya huyu ni mara chache sana kupata saratani hata anapozeeka na anaweza kuishi maisha marefu na yenye afya ikilinganishwa na panya wengine.

Hii inatokana na mapigo yake ya moyo kwenda polepole, na uwezo wa kupunguza kiwango kasi ya mmengenyo wa chakula na oksijini wakati wa hali ngumu.

Pia, panya huyu hahitaji kunywa maji, hupata maji yote anayohitaji kutoka katika chakula anachokula.

Samaki aina ya Blobfish

Kwa kawaida huishi katika Ukanda wenye giza nene katika bahari katika kina cha kati ya mita 600 hadi 1,200 (futi 2,000 hadi 3,900), ikimaanisha kwamba ili kuishi katika hali kama hiyo ni lazima awe na misuli midogo na mifupa laini.

Hii ina maana kwamba anapotolewa majini mwili wake huwa tepetepe na kukusanyika wote, na kupoteza umbo lake la asili kama akiwa kwenye maji.

Papa aina ya Goblin

Papa wa goblin ni nadra sana na ana ukoo wake umeanzia zaidi ya miaka milioni 125 iliyopita.

Pua yake ni ndefu na taya yenye nguvu inayoweza kutanuka, wakati wa mawindo. Mara nyingi, taya hufunga na kuficha safu ya meno yake ambayo ni makali sana.

Papa huyu wa baharini hupatikana sana pwani ya Japani, ingawa ameonekana katika maeneo mbalimbali duniani. Kwa sababu huwa anaishi katika kina kirefu cha maji mita 100 hadi 1,300 (futi 330 hadi 4,300) - ni vigumu kumuona.

Papa goblin anahesabiwa kuwa yuko hatarini kutoweka.

Chura wa zambarau

Chura wa zambarau, au chura mwenye pua ya nguruwe, ana sehemu kubwa ya nyuma. Sehemu yake ya nyuma yenye misuli humpa nguvu ya kuchimba ndani ya udongo, ambapo hutumia muda mwingi wa maisha yake. Tofauti na vyura wengine wengi, anahitaji miguu yenye nguvu kwa ajili ya kuchimba, si kuruka.

Kuishi chini ya ardhi pia kunamaanisha chura huyu hahitaji kuona sana – ndio maana ana macho madogo. Na umbo la ajabu la kichwa chake ni kwa ajili ya kutafuta chakula katika ardhi yenye unyevunyevu akitafuta mchwa.

Vyura dume pia wana sauti ya kipekee wanayotumia wanapotoka kwenye mashimo yao ya chini ya ardhi ili kuvutia jike.

Igawa spishi hii iligunduliwa mwaka 2003, idadi yake imepungua, na wako hatarini kutoweka.

Ngiri

Ngiri huenda asiwe mnyama mzuri duniani, lakini pembe zake humlinda kutokana na wanyama wanaowinda wanyama wengine. Licha ya kuwa na silaha hizi, ngiri si mkali na hula wadudu na matunda.

Kiumbe huyu anaishi katika nyasi za wazi huko Afrika na huliwa na simba, chui, fisi na wanadamu. Cha kushangaza, anaweza kukimbia hadi kasi ya kilomita 48 kwa saa (30mph) - ambayo ni muhimu sana kwa kuwatoroka wanyama wawindaji.

Tumbili mwenye upara (Uakari)

Uakari mwenye upara kiasili ana uso mwekundu. Tumbili huyu mdogo huishi katika misitu inayozunguka bonde la Mto Amazon na ana sifa ya uso wake mwekundu, kichwa chenye upara na manyoya marefu. Uso wake mwekundu ni ishara ya afya njema.

Hata hivyo, uakari mwenye upara ana uwezekano wa kupata malaria, ambayo humpa uso mweupe zaidi na kuifanya asipendezeke.

Uakari mwenye upara ameorodheshwa na Umoja wa Uhifadhi wa Mazingira Kimataifa (IUCN) kama spishi iliyo hatarini kutokana na ukataji miti, na mengi zaidi yanahitaji kufanywa ili kuwalinda nyani hawa wa kuvutia.

Popo wa Hammerhead

Popo huyo anayeitwa Hypsignathus ndiye popo mkubwa zaidi barani Afrika, na popo wa tatu kwa ukubwa duniani.

Popo wa dume ni mkubwa zaidi kuliko wa jike, akiwa na kichwa kikubwa zaidi. Pia ana sauti ya ajabu sana, kwa ajili ya kumvutia jike.

Popo wa hammerhead hula matunda na nzi na huishi katika maeneo ya misitu ya mvua ya chini.

Kobe kama mamba

Kwa kuwa na ganda lenye miiba inayoonekana, kichwa chake kilichochongoka na mdomo ulichongeka, huyu ni kombe anyaefanana mamba.

Ni kobe mkubwa zaidi wa maji safi anayepatikana Marekani na ana taya zenye nguvu sana za kula samaki na mamalia wadogo, akitumia ulimi wake ili kuwavutia mawindo.

Ingawa si mnyama anayevutia zaidi, ni mfano mzuri wa mabadiliko ya tabia na mageuko katika utendaji.

Spishi hiyo inachukuliwa kuwa hatarini kadri idadi ya wanyama inavyopungua kutokana na upotevu wa makazi na uwindaji.