Makocha 6 waliopoteza kazi baada ya Kombe la Dunia

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Kombe la Dunia 2026 lilikuwa na mabadiliko mengi, ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya timu kutoka 32 hadi 48.

Upanuzi wake ulizipatia nchi nyingi imani ya kushiriki kwa katika mashindano hayo.

Nchi kama Korea Kusini, ambazo zilianza mashindano vizuri kwa kuifunga Jamhuri ya Czech mabao 2-1, ziliweka juhudi kubwa, lakini hatimaye hazikuweza hata kuvuka hatua ya makundi.

Nyingine, kama Ureno, zilifanikiwa kusonga mbele, lakini safari yao haikufika mbali kama ilivyotarajiwa.

Baada ya baadhi ya nchi kuondolewa kwenye mashindano, kama vile Senegal, kulitokea mgawanyiko kati ya wachezaji na kocha, jambo lililofichua mzozo wa ndani ambao haukujulikana hapo awali.

Baadhi ya nchi kama vile Tunisia waliwatimua makocha wao katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo kwa kushindwa kukidhi matarajio.

Wafuatao ni baadhi ya makocha walioacha kazi baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

Ronald Koeman - Uholanzi

Ronald Koeman alistaafu baada ya timu ya taifa ya Uholanzi aliyokuwa akiiongoza kuondolewa kwenye kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia.

Taarifa za kujiuzulu kwake zinajiri huku kukiwa na msururu tuhuma za ubaguzi dhidi ya wachezaji waliofunga penati kama Kluivert kwenye mitandao ya kijamii.

Uholanzi ilitolewa na Morocco katika hatua ya 32 kwa mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya 1-1.

Justin Kluivert, Quinten Timber na Crysencio Summerville walikosa penati, jambo ambalo liliwafanya kukabili na unyanyasaji wa kibaguzi.

Kocha huyo alitoa kisingizio kuwa mkewe alikuwa anaumwa na ndiyo maana alitaka kuacha kazi ili aweze kumhudumia.

Pape Thiaw - Senegal

Senegal imemtimua kocha Pape Thiaw baadaya kuondolewa katika hatua ya timu 32 kwenye Kombe la Dunia.

Thiaw amekuwa akiinoa ''Teranga Lions'' tangu Desemba 2024, lakini katika mashindano hayo, ilianza kwa kufungwa na Ufaransa na baadaye Norway katika mechi zake mbili za kwanza.

Walifanikiwa kuifunga Iraq mabao 5-0 na kusonga mbele kwa pointi tatu, hatua iliyowawezesha kufika raundi ya timu 32.

Katika hatua ya makundi, Ubelgiji iliifunga Senegal mabao 3-2 - katika mechi hiyo, Senegal ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 85, kabla ya wapinzani wao kusawazisha na hatimaye kuibuka na ushindi.

Kufutwa kazi kwa Thiaw kulitokana na malalamiko ya Pape Gueye, ambaye alisema angeacha kuichezea timu ya taifa iwapo kocha huyo na kikosi chake cha ufundi wangeendelea kuinoa timu hiyo.

Julian Nagelsmann - Ujerumani

Kocha wa Ujerumani, Julian Nagelsmann, naye alikumbwa na dhoruba ya Kombe la Dunia kufuatia kuondolewa kwa kushtukiza na Paraguay katika hatua ya timu 32.

Ingawa hakuonyesha nia ya kuondoka—akisema katika mahojiano kuwa "sipendi watu wanaotoroka majukumu"—baadaye alipata taarifa kutoka kwa Shirikisho la Soka la Ujerumani kwamba limeanza mazungumzo na mrithi wake mtarajiwa.

Hali hii imemuacha Julian Nagelsmann bila nia ya kujiuzulu kwa sasa, lakini hana budi kusalimu amri.

Aliyekuwa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp, amethibitishwa kuwa kocha mpya.

Tayari ametoa jibu kwa Shirikisho la Soka kwamba ameridhia uamuzi huo, kama ilivyotangazwa.

Hii ilikuwa michuano ya pili ya kimataifa kwa Julian Nagelsmann baada ya kuiongoza Ujerumani katika Euro 2024, ambapo alifika hatua ya nusu fainali.

Tangu kushinda Kombe la Dunia mwaka 2014 katika mechi dhidi ya Ujerumani, timu hiyo imeshindwa kuvuka hatua ya makundi katika michuano ya 2018 na 2022.

Roberto Martinez - Ureno

Shirikisho la Soka la Ureno lilitangaza kujiuzulu kwa kocha wa timu ya taifa Roberto Martinez baada ya timu hiyo kufungwa na Uhispania katika hatua ya 16.

Martinez alitangaza mnamo Januari 2023 nia yake ya angeachia ngazi.

Ureno ilimaliza ya pili katika kundi lao, ikitoka sare mara mbili dhidi ya Colombia na DR Congo, ikiichapa Uzbekistan mabao 5-0, na kuifunga Croatia katika hatua ya 32.

Katika hatua ya 16 bora, Uhispania iliifunga Ureno bao 1-0 katika dakika za mwisho za mchezo kupitia bao la mshambuliaji wao, Merino.

Martinez, mwenye umri wa miaka 52, aliiongoza Ureno katika michuano ya UEFA Nations League mwaka 2025, lakini mwaka 2024 timu yake iliondolewa katika hatua ya nusu fainali na Ufaransa kupitia mikwaju ya penati.

Kocha huyo amekosolewa kwa madai ya kumpa kipaumbele Ronaldo—ambaye umri wake umesonga—kuliko wachezaji vijana ambao wangeiwezesha timu hiyo kupata ushindi.

Hong Myung-Bo - Korea Kusini

Siku moja baada ya Korea Kusini kuondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia, kocha wa taifa Hong Myung-Bo alitangaza kujiuzulu.

Kustaafu kwake kulifuatia ukosoaji mkali kutoka kwa Rais aliyesema "hafai" na kutaka nafasi yake katika michuano hiyo ifanyiwe uchunguzi wa kina.

Nchi hiyo ilianza kwa ushindi katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Jamhuri ya Czech lakini ilishindwa katika mechi zote mbili za makundi zilizosalia.

Cyprus iliizuia kufika hatua ya 32, kwani ililazimika kusubiri Mexico itoke sare au kushindwa, lakini Mexico ilishinda mechi yake.

Kocha Hong Myung-Bo aliombamsamaha hadharani, kusema anachukua jukumu la kushindwa kama kocha.

Sabri Lamouchi - Tunisia

Tunisia ilimfukuza kazi kocha Sabri Lamouchi baada ya timu hiyo kufungwa katika Kombe la Dunia.

Uswidi ilianza kwa kuichapa timu hiyo mabao 5-1 katika mechi ya Kundi F iliyochezwa kwenye Uwanja wa Monterrey huko Guadalupe, Mexico.

Baadaye taarifa ziliibuka kwamba Lamouchi amefukuzwa kazi, lakini chanzo kimoja kiliiambia BBC kuwa kocha huyo aliendelea kusimamia mazoezi ya timu hiyo siku moja baada ya kuondolewa.

Hata hivyo, baadaye Shirikisho la Soka la Tunisia lilitangaza kuwa hatua hiyo ya ilifikiwa kwa heshima na utaratibu mwema.

Kisha walimteua Herve Renard, aliyewahi kuwa kocha wa Morocco na Saudi Arabia, kuwa kocha mpya wa timu hiyo hadi mwisho wa mashindano.

Lamouchi alikuwa kocha wa kwanza kufukuzwa kazi katika mashindano hayo, na baada yake, makocha wengine kadhaa waliacha kazi.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi