Afrika Kusini: Waumini wasombwa na maji katika mto wa Jukskei uliofurika

Chanzo cha picha, ROBERT MULAUDZI
Afrika Kusini: Waumini wasombwa na maji katika mto wa Jukskei uliofurika
Watu wawili wamefariki dunia nchini Afrika Kusini na wengine 15 hawajulikani walipo baada ya mto kufurika na kusomba waumini waliokuwa wakishiriki ibada ya kanisa.
Baadhi ya waumini zaidi ya 30 walikuwa wamesimama juu ya mawe katika mto huo siku ya Jumamosi wakati mafuriko ya maji yalipopitia, mtu aliyeshuhudia alisema.
Mchungaji aliokolewa baada ya kung’ang’ania tawi la mti lililokuwa likining’inia, aliongeza.
Waokoaji walianza tena msako katika mto Jukskei mjini Johannesburg siku ya Jumapili.
Mafuriko hutokea mara kwa mara wakati wa msimu wa mvua nchini Afrika Kusini, mwandishi wa BBC Nobuhle Simelane mjini Johannesburg anasema.
Operesheni hiyo ya utafutaji wasiojulikana walipo inahusisha polisi na zima moto pamoja na timu maalum za uokoaji wa majini, Robert Mulaudzi msemaji wa Huduma za Dharura za Jiji la Johannesburg alisema.
Victor Ncube, ambaye alikuwa akishiriki katika ibada ya kanisa, aliambia kituo cha habari cha ndani cha eNCA kwamba alifanikiwa kuwatoa watu watano kutoka mtoni ambao walikuwa wamesombwa na maji umbali wa mita 100 chini ya mkondo.
Wengine walikuwa wamebebwa mbali sana chini ya mto wakati anajaribu kuwaokoa, alisema.
Kati ya 33 waliokuwa kwenye ibada hiyo, 15 bado hawajulikani waliko, mamlaka inasema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe













