Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 16.03.2024
Manchester City wamefanya mawasiliano kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle United na Brazil Bruno Guimaraes, 26. (AS - in Spanish)
Liverpool wana nia ya kufanya dili la kiungo wa kati wa Ujerumani Jamal Musiala, huku Bayern Munich wakiweka bei ya pauni milioni 100 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Football Insider)
Liverpool pia wanahusishwa na uwezekano wa kumnunua fowadi wa Eintracht Frankfurt kutoka Misri Omar Marmoush, 25. (Bild, via FourFourTwo)
Arsenal wanapanga kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid Brahim Diaz na wako tayari kulipa hadi pauni milioni 60 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye hivi karibuni ameweka mustakabali wake wa kimataifa kuichezea Morocco. (Football365)
Manchester City wamekubali mkataba wa majira ya kiangazi kumsaini winga wa Brazil Savio, 19, ambaye yuko kwa mkopo Girona kutoka klabu dada ya City, Troyes. (Football Insider)
Brentford na Aston Villa wana nia ya kumsajili kiungo wa Bologna na Scotland Lewis Ferguson, 24. (TeamTalk)
Fulham wanatayarisha ofa ya kandarasi mpya kwa mlinzi wa Uingereza Tosin Adarabioyo, 26. (Mail)
Leeds United wako tayari kusikiliza ofa kwa winga Mwingereza Jack Harrison, 27, ambaye ametumikia msimu huu kwa mkopo Everton. (Football Insider)
Jurgen Klopp bado anaweza kupata kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani huku wakiwa tayari kufanya makubaliano kwa ajili ya kocha anayeondoka Liverpool. (Football Transfers)
Kutokuwa na uhakika juu ya hatma ya Erik ten Hag kama meneja wa Manchester United kumeacha wakufunzi wake katika sintofahamu. (Mail)
Manchester United watapata adhabu ya pauni milioni 10 kila msimu wanaposhindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mujibu wa mkataba wao mpya wa jezi za pauni milioni 90 kwa mwaka na Adidas. (Times}
Reading wako kwenye mazungumzo ya juu na kampuni ya Marekani Kaskazini kununua klabu hiyo. (Sky Sports)
Wolves wanakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili kiungo wa kati wa Rochdale na Uingereza Matheus Mane, 16 kwa ajili ya akademi yao. (Fabrizio Romano)