Iwapo unatumia manukato au marashi, hizi ndio mbinu sahihi za kuitumia

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya kuoga asubuhi , jambo la kwanza tunalolifanya ni kujipulizia marashi ama manukato. Kabla ya kuvaa nguo watu wengi hasa vijana kujipulizia manukato ya aina ya kiondoa harufu (deodorant) mwilini kwanza kabla ya kuanza shughuli za siku.
Manukato haya huusaidia mwili kuondokana na harufu ya mwili kwa siku nzima . Aina fulani za kemikali zinazotengeneza 'deodorant' huzuia kukua kwa bakteria wanaotengeneza jasho. Hivyo basi husaidia kudhibiti harufu mbaya ya jasho.
Kwa sasa, deodorant zenye manukato ya harufu mbali za kunukia zinauzwa katika masoko mbali mbali . Hizi ni pamoja na zile za kujipulizia, za maji maji, za kuzungusha (roll-on) na hata zile zinazobandikwa mwilini .
Lakini je ulishawahi wakati mmoja kujiuliza iwapo kutumia manukato kunaweza kukuua?
Kwasababu, hivi karibuni ilifichuliwa kuwa msichana mwenye umri wa miaka 14 alifariki baada ya kujipulizia deodorant nchini Uingereza.
Kulikuwa na mijadala mingi kuhusu kutumia deodorant wakati tukio hili lilipotokea.
Ni nini hasa kilichotokea?
Msichana mwenye umri wa miaka 14 alifariki baada ya kupumua hewa ya marashi iliyopulizwa ndani ya mapafu yake.
Georgia Green, msichana aliyeishi Uingereza alipuliza deodorant katika chumba chake na alikuwa na mshituko wa moyo.
Georgia alikuwa na hali ya kiafya ya autistic na baba yake alisema kuwa alipenda kujipulizia marashi. Alikuwa akiipulizia kwenye blanketi yake na hilo lilimfanya ajihisi vizuri .
Jinsi ya kutumia marashi
Iwapo unatumia marashi ya kupachika au ile yakupaka, izungushe mara 2 hadi 3 kwenye mwili ambao bado una unyevu nyevu baada ya kuoga.
Iwapo unatumia deodorant ya kupuliza, ipulize umbali wa mita 10 hadi 15 kutoka mwilini mwako ili kuifanya inukie kwa muda mrefu mwilini mwako, wanasema wataalamu wa vipodozi.
Kupuliza marashi kutoka umbali mfupi sana au kutoka mbali sana na mwili, haina faida wanasema, wataalamu wa vipodozi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tofauti kati ya marashi ya kupaka na manukato ya maji maji (body spray)
marashi huua bakteria. Hufanya kazi ya kuangamiza bakteria wanaotengenezwa na jasho la mwili .
Manukato yanayopulizwa hutengenezwa kwa mafuta. Hutumiwa kama mbadala wa manukato ya perfume.
Marashi kwa kawaida zimetengenezwa kwa ajili ya kupulizwa katika maeneo fulani ya mwili pekee . Manukato ya kupulizwa au Body sprays yanaweza kupulizwa kwenye mavazi.
Je marashi ni hatari ?
Kama ilivyoelezwa hapo awali katika habari, msichana mwenye umri wa miaka 14 alifariki kwa mshituko wa moyo baada ya kutumia manukato aina ya deodarant.
Nchini Uingereza pekee, kulingana na ofisi ya taifa ya takwimu, kati ya mwaka 2001 na 2022, vifo 11 ‘’vilisababishwa na marashi’’.
Kati ya mwaka 2000 na 2008, idadi ya watu walifariki kwa kuvuta hewa ya manukato sawa na marashi na glues walizidi wale waliofariki kutokana na madawa, kulingana na ripoti ya taasisi ya Talk to Frank, ambayo ni washauri wa matumizi ya madawa nchini Uingereza .
Vingi kati ya vifo vilitokea miongoni mwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 10 na 15.
Kilingana na Mayo Clinic, watoto kati ya 100 na 200 hufariki kila mwaka kwa kuvuta hewa ya kemikali zinazotishia maisha

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini idadi halisi huenda ikawa kubwa zaidi kwasababu viungo fulani katika marashi havikutajwa katika vyeti vya vifo vya watu hao.
Taasisi ya kuzuia ajai ya uingereza -The Royal Society of Prevention of Accident imesema kuwa watu wengi hufariki kutokana na manukato ya deodorant.
Je ni vizuri au ni vibaya kutumia marashi?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baadhi ya watu huathirika kwa kupata mzio baada ya kutumia marashi.
Baadhi huhisi kushindwa kupumua vyema kwasababu ya marashi, kulingana na Profesa msaidizi katika hospitali ya Professor at Osmania Hospital, Hyderabad nchini India .
Profesa Pratibha Lakshm anasema , “Baadhi ya watu huhisi muwasho , vipele n ahata wengine hujikuna baada ya kutumia deodorant . Huanza ni kitu fulani kidogo kama mzio wa Ngozi. Na wakati mwingine mzio huo unaweza kuendelea na kuwa saratani ya hatari .”
Manukato huwa na kiungo cha parabens, kilevi na magfuta ya manukato. Pia huwa na kemikali hatari inayoitwa propylene glycol. Hii inaweza kuwa hadi asilimia 50 katika baadhi ya deodorant.
Kemikali hii inaweza kuathiri moyo na ini, na inaweza kuwa hatari zaidi kwa watu wenye ngozi isiyoweza kuhimili kemikali hii.
Hivyo basi ni bora kila mara kutumia deodorant ambayo ina kiwango cha chini ya asilimia 2 ya kemikali ya propylene glycol.
Aluminum pia hutumiwa katika kutengeneza deodorant. Baadhi wanaamini kuwa ni hatari kwa matiti ya wanawake, lakini hakuna ushahidi thabiti wa kuthibitisha hili kwani bado halijafanyiwa utafiti.
Weka deodorant mbali na watoto
Kutokana na sababu zote hapo juu, ni vyema kuweka mbali kemikali zote sawa na zilizomo katika deodorant mbali na watoto, kwasababu zina uwezekano mkubwa wa kuwa na athari mbaya kwao.
Kuvuta hewa ya deodorant kwa watoto kunaweza kusababisha kizunguzungu, maumivu ya kichwa, kutapika, na matatizo ya kupumua. Katika baadhi ya visa inaweza pia kusababisha kifo. Kwahiyo ni wajibu wetu kuweka mbali watoto na deodorant na itumie kwa uangalifu mkubwa.
















