Liz Truss aahidi mpango kabambe katika kinyang'anyiro cha waziri mkuu Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss
Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Liz Truss
Iliyochapishwa

Liz Truss ameahidi kutangaza mpango wa kukabiliana na kupanda kwa gharama za nishati ndani ya wiki moja ikiwa atakuwa waziri mkuu siku ya Jumanne.

Kiongozi huyo anayesemekana kuwa anayependwa zaidi kulingana na kura za maoni, aliambia mwandishi wa BBC Laura Kuenssberg ‘’atachukua hatua mara moja’’ kusaidia katika bili.

Lakini hakutoa maelezo yoyote, akisema atahitaji muda ofisini kwanza ili kukamilisha mapendekezo kamili.

Mpinzani wake Rishi Sunak alisema atalenga malipo zaidi kwa maskini zaidi.

Mmoja wa wagombea wawili atatangazwa kama kiongozi anayefuata wa Jumatatu, na atachukua nafasi ya Boris Johnson kama Waziri Mkuu siku inayofuata.

Wamekuwa chini ya shinikizo kuelezea jinsi wangelinda kaya na bili zinazoongezeka, na pia kutoa msaada kwa biashara, ambazo hazipo kwenye ukomo wa bei uliyowekwa kwa biashara za ndani.

Akizungumza kwenye kipindi cha BBC One Jumapili na Laura Kuenssberg, Waziri wa Mambo ya Nje Bi Truss alisema hatua kuhusu bili za nishati itakuwa ‘’muhimu’’ kwa watu na uchumi.

Aliongeza kuwa msaada zaidi utahitaji kwenda ‘’bega kwa bega’’ na mpango wa kuongeza usambazaji wa nishati ya ndani, akisema Uingereza imekuwa ikitegemea sana bei ya nishati ya kimataifa.

Waziri wa Fedha wa Uingereza, Rishi Sunak
Maelezo ya picha, Waziri wa Fedha wa Uingereza, Rishi Sunak
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Bw Sunak kwa upande wake alisema malipo zaidi ya kawi kwa wastaafu na wanaolipwa mshahara kidogo, zaidi ya wale aliotangaza kama chansela, yanapaswa kulenga wastaafu na wanaolipwa kidogo.

Amedai kuwa pendekezo lake la kupunguzwa kwa VAT kwenye bili za nishati kunaweza pia kutoa msaada kwa wote.

Pia alisema hawezi kuondoa matarajio ya kukatika kwa umeme wakati wa msimu wa baridi kwa usambazaji wa mgao, kwani hali ilikuwa ‘’mbaya’’ na ‘’kila chombo kwenye sanduku la zana’’ kitahitajika.

‘’Kwa kweli hatutaki kuwa katika hali hiyo, lakini nadhani inawajibika kutoiondoa,’’ aliongeza.

Bi Truss ameahidi kutoa kiasi cha £30bn katika kupunguzwa kwa kodi katika bajeti ya dharura baadaye mwezi huu ikiwa atashinda, ikiwa ni pamoja na kubadilishwa kwa kupanda kwa Bima ya Taifa kulikoshuhudiwa mwezi Aprili.

Akishinikizwa iwapo watu matajiri wangefaidika zaidi kutokana na upunguzaji huo, alisema: ‘’Watu walio juu ya mgawanyo wa mapato hulipa kodi zaidi - kwa hivyo bila shaka, unapokata kodi huwa unawanufaisha watu ambao wana uwezekano mkubwa wa kulipa kodi.’’

Lakini aliongeza: ‘’Kuangalia kila kitu kupitia ugawaji naamini si sahihi. Kwa sababu ninachozungumzia ni kukuza uchumi - na kukuza uchumi kunanufaisha kila mtu.’’

Mjadala wa kiuchumi kwa miaka 20 iliyopita umetawaliwa na majadiliano kuhusu usambazaji.

Na kilichotokea ni kwamba tumekuwa na ukuaji mdogo. ‘’Zaidi ya mapendekezo yake ya kupunguzwa kwa VAT kwenye bili za nishati, Bw Sunak amechukua mtazamo tofauti, akisema kupunguzwa kwa ushuru kwa kudumu kunapaswa kusubiri hadi mfumuko wa bei upungue.

Mwanasheria mkuu wa Labour Emily Thornberry alisema ilikuwa ni ‘’ajabu’’ hakuna mgombea ambaye alikuwa ametoa ‘’jibu mahususi’’ kuhusu mipango yao ya nishati wakati wa kinyang’anyiro cha uongozi kilichodumu kwa wiki kadhaa.

Aliongeza kuwa watu ‘’walitamani sana’’kusaidiwa, na wale wa kipato cha kati na maskini zaidi wanahangaika na kupanda kwa bili.