Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City yakaribia kumsajili Ayyoub Bouaddi

Hj
Maelezo ya picha, Ayyoub Bouaddi
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester City inakaribia kumsajili Ayyoub Bouaddi, 18, kutoka Lille, kiungo huyo wa Morocco ana thamini ya euro milioni 100 (pauni milioni 85). (Guardian)

Real Madrid wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania, Martin Zubimendi, 25, kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Arsenal. (Football.London)

Mshambuliaji wa Arsenal na Brazil, Gabriel Jesus, 29, yuko tayari kuhamia Napoli msimu huu wa joto. (La Gazzetta dello Sport)

Klabu ya Italia, AS Roma imefanya mazungumzo ya awali na wawakilishi wa Gabriel Martinelli juu ya uhamisho wa winga huyo wa Arsenal na Brazil mwenye umri wa miaka 25. (Mirror)

Barcelona na Tottenham zote zimefanya mazungumzo hivi karibuni na Bayern Munich kuhusu mshambuliaji raia wa Uingereza, Harry Kane, 33, kuhusu uhamisho wa msimu wa joto. (Teamtalk)

Manchester City wanafahamu nia ya Nottingham Forest kumsajili kiungo wao wa kati raia wa Uholanzi, Tijjani Reijnders, 28, ambaye alisajiliwa kutoka AC Milan msimu uliopita wa joto kwa pauni milioni 46. (Sky Sports)

Liverpool licha na Arsenal zote zimeonesha ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Bradley Barcola, 23, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa takriban pauni milioni 130. ( Sun)

Beki wa Inter Milan na Italia, Alessandro Bastoni, 27, na kiungo wa kati wa Crystal Palace na England, Adam Wharton, 22, bado wanavutiwa kujiunga na Real Madrid, timu ambayo ina nia ya kusajili wachezaji wengine watatu msimu huu. (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Marseille na Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg, 31, amekataa fursa ya kujiunga na Newcastle. (Talksport)

Manchester United inafikiria kumsajili beki wa RB Leipzig na Ujerumani, David Raum, 28, baada ya kushindwa kumsajili beki wa kushoto wa England, Lewis Hall, 21, kutoka Newcastle. ( Teamtalk)

Hj

Chanzo cha picha, Reddit

Maelezo ya picha, Djed Spence
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Beki wa Tottenham na England, Djed Spence, 26, amerejea kwenye darubini ya Inter Milan baada ya timu hiyo kushindwa kumsajili winga wa zamani wa Aston Villa na Ufaransa, Moussa Diaby kutoka Al-Ittihad . ( Sky Sport)

Jamie Vardy anaweza kurejea kwenye soka la Uingereza huku timu ya West Ham inayoshiriki Championship ikifikiria kumsajili mshambuliaji huyo wa zamani wa Leicester City na Uingereza mwenye umri wa miaka 39, ambaye ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya Cremonese ya Italia kumalizika. ( Sun)

West Ham pia wanafanya mazungumzo na Arsenal ili kumsajili Reiss Nelson, winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 ambaye alitumia misimu miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu za Brentford na Fulham. ( Standard)

Timu iliyopanda daraja Ligi Kuu England, Hull City imekataliwa ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Swansea City, Zan Vipotnik, mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia mwenye umri wa miaka 24 ambaye alimaliza kama mfungaji bora katika Championship msimu uliopita. (Athletic)

Beki wa Sunderland na DR Congo, Arthur Masuaku, 32, anatarajiwa kurejea Uturuki huku akikamilisha uhamisho wake kwenda Konyaspor. ( Sky Sports)

Atletico Madrid wameanzisha dau la euro milioni 35 (pauni milioni 30) ili kumsajili mshambuliaji wa Lille, Matias Fernandez-Pardo, mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia anatakiwa na Arsenal na Liverpool. (L'Equipe)

Napoli wamefungua tena mazungumzo na Chelsea katika juhudi za kukamilisha mpango wa kumsajili beki wa kati wa Ufaransa, Benoit Badiashile, 25. (Sky Sport)