Iran: Simulizi ya siku 1,000 za kifungo cha kutengwa na wengine na mateso kupita maelezo

A photo of brothers Navid, Vahid and Habib Afkari (left to right)

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, Gharama kubwa ya maandamano ya amani nchini Iran huku Vahid Afkari (katikati) akishikiliwa katika kifungo cha upweke na kaka zake Navid (kushoto) na Habib (kulia) wakilengwa pia.
    • Author, Maryam Afshang
    • Nafasi, BBC Persian
  • Iliyochapishwa

Vahid Afkari, 37, ametumia siku 1,000 katika kifungo cha kutengwa na wengine au cha upweke nchini Iran.

Licha ya ukandamizaji mkali dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali kwa miaka mingi, ni nadra kwa mamlaka kumweka mtu katika seli ya gereza peke yake kwa muda mrefu.

"Kila wakati familia hiyo inapomtembelea Vahid gerezani, wanajaribu kumuonesha kuwa wako pamoja naye lakini mwishowe, yeye ndiye anayeibuka kuwatia moyo," chanzo cha karibu cha familia amesema.

Hii sio tukio la pekee la familia ya Afkari. Nimefuatilia simulizi yao kwa miaka mingi na inaonyesha jinsi utawala wa Iran utafanya chochote kunyamazisha upinzani.

'Hakuna ushahidi wowote'

Matatizo ya familia ya Afkari yalianza miaka michache iliyopita katika mji wao wa Shiraz kusini mwa Iran.

Watu walikuwa wakiandamana kupinga kupanda kwa bei za bidhaa na kupunguzwa kwa mishahara.

Ndugu watatu - Vahid, Habib na Navid -- waliingia mitaani. Navid, mdogo zaidi, alikuwa bingwa wa mieleka na anayejulikana sana. Hii ilimfanya apewe adhabu kali zaidi kutoka kwa mamlaka.

The Afkari family

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, Navid, Afkari mdogo, yuko mbele ya picha upande wa kushoto, akiwa amezungukwa na baadhi ya ndugu zake na jamaa.

Mnamo 2018, ndugu hao watatu walikamatwa. Miaka miwili baadaye, walipatikana na hatia ya kumuua afisa wa usalama. Wote watatu walikana kuhusika.

Nimethibitisha makumi ya nyaraka zinazoonyesha kuwa ndugu wa Afkari walilalamika kwa mamlaka ya mahakama kuhusu kuteswa ili kukiri makosa wakiwa kizuizini.

Ujumbe wa sauti kutoka kwa Navid ulishirikisha kwenye mitandao ya kijamii mnamo Agosti 2020. "Hakuna hata chembe ya ushahidi katika kesi hii ambayo inathibitisha kuwa nina hatia," alisema. "Natambua kuwa wanatafuta chochote kunipata na hatia." Neno hili baadaye lilienea sana.

Mwezi huo huo, ujumbe wa sauti kutoka kwa Vahid ulisafirishwa nje ya gereza la Adel Abad huko Shiraz, ambapo wote walikuwa wakishikiliwa.

"Niligoma kula mara mbili kwa siku 20 kila moja, nikitumai kuwa sauti yangu ingesikika lakini haikufanyika," alisema Vahid. "Hatimaye, nilijaribu kujitoa uhai kutokana na mateso ya kiakili na kisaikolojia niliyokuwa nimevumilia."

Vahid Afkari standing on the roof of a car with his arms in the air

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, Vahid ana sifa ya msomaji na mwenyefikra za kipekee katika familia yake, mwenye dhamiri kali ya maadili

Navid alihukumiwa kifo huku Vahid na Habib awali wakihukumiwa miaka 54 na 25 jela kila mmoja.

Familia yenye upendo

Chanzo hicho kinaniambia ndugu hao watatu kutoka katika familia ya wavulana watano na msichana mmoja walilelewa katika mazingira ya upendo japokuwa pesa ilikuwa ngumu kupata. "Walipata furaha nyingi kwa kuwa pamoja, mambo rahisi zaidi yalikuwa ya kusisimua zaidi," chanzo kinasema.

Vahid na Habib walikuwa wanafunzi bora na walihudhuria chuo kikuu. Vahid hakuwahi kuwa mzigo wa aina yoyote ile kwa mama yake. "Siku zote alikuwa na wasiwasi ikiwa angekuwa na chakula cha kutosha," kilisema chanzo. Vahid alikua mpaka chokaa baada ya chuo kikuu kwa sababu hakukuwa na kazi.

Wakati huohuo, Habib na Navid, kama watoto wawili wa mwisho, walikuwa karibu kila mara wanakabiliwa na maovu.

Wakati Navid alipoanza kushinda mataji kama mwanamieleka, hakuwahi kujivunia mafanikio yake. "Mama yao angejikwaa na alama mpya za ubingwa zilizofichwa kwenye kabati lake," kilisema chanzo.

Kuwekwa seli chinichini kando ya chumba cha mauaji

Mnamo Septemba 2020, ndugu hao watatu walipigwa vibaya gerezani na kuwekwa katika seli za chinichini kando ya chumba cha mauaji.

Seli zilikuwa hazijawashwa bila madirisha, vitanda au blanketi -- choo na sinki vilikuwa kwenye kona.

Wafungwa huingia kwenye seli wakiwa uchi na hupewa sare iliyovaliwa hapo awali, ambayo mara nyingi hufunikwa na damu kutokana na kupigwa au kujidhuru.

Mfungwa wa zamani aliniambia "kuwazia shimo jeusi kama unavyoweza kuona kwenye sinema". Ndugu pia walifunikwa macho.

"Umefungwa pingu na vifundo vya miguu yako vimefungwa. Kwa sababu ya baridi, pingu za chuma huwa na wembe. Maumivu ni makali sana unalazimika kulalia kifua chako," mfungwa huyo wa zamani aliongeza.

Navid Afkari

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Navid Afkari alikuwa bingwa wa mieleka lakini hakujigamba kwasababu ya mafanikio yake

Kabla ya jua kuchomoza tarehe 22 Septemba 2020, Vahid na Habib walisikia utaratibu wa kunyongwa ukiendeshwa.

Dakika chache baadaye, mlinzi aliingia ndani ya seli zao na kusema, "Rambirambi".

Kaka yao mdogo Navid alinyongwa akiwa na umri wa miaka 27.

Kampeni ya ndani na nje ya Iran ya kusitisha kunyongwa kwake ilishindikana.

'Sina hatia'

Baada ya kunyongwa kwa Navid, wenye mamlaka waliendelea kuweka shinikizo kwa ndugu hao wawili.

Hawakuruhusiwa kutembelewa au hata kupiga simu kwa majuma kadhaa, na familia haikujua ikiwa bado walikuwa hai.

Wakati familia ya Afkari hatimaye iliporuhusiwa kuwatembelewa, waligundua kwamba Vahid alikuwa chini ya shinikizo zaidi la kujishtaki yeye mwenyewe na kaka yake Habib aliyebaki.

Vahid and Habib Afkari seated in a family photo

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, Mamlaka ya Iran ilimtishia Vahid (kushoto) kwa kila kitu -- ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa kaka yake Habib (kulia) -- ili tu akiri kutenda makosa.

Vahid aliambiwa angeachiliwa ikiwa atakiri mauaji hayo. Kama hangefanya hivyo, mamlaka ingemuua Habib mbele yake.

Vahid alisema alimpenda sana Habib lakini hawakuwa na hatia.

Kisha maafisa hao walimwambia Vahid kwamba haogopi kifo.

Akajibu: "Naogopa lakini sina hatia." Hatimaye Habib aliachiliwa mnamo Machi 2022 baada ya shinikizo la kimataifa.

Mourners at Navid's grave in Shiraz

Chanzo cha picha, Family photo

Maelezo ya picha, Kaburi la Navid lilikuwa limejaa maua katika ukumbusho wa mwezi mmoja tangu kunyongwa kwake tarehe 22 Oktoba 2020

Vahid bado yuko kwenye kifungo cha upweke au peke yake. Inasemekana yuko katika hali nzuri na anafanya mazoezi katika seli yake kila siku.

Kampeni ya kimataifa imehamasishwa kutaka kuachiliwa kwake.

"Vahid Afkari hapaswi kamwe kukaa jela hata siku moja, licha ya kufungwa jela kinyume na haki na siku 1,000 katika kifungo cha upweke.

Ni lazima aachiliwe mara moja," Amnesty International ilisema katika taarifa yake.

Kaburi la Navid bado halina jiwe la msingi linalofaa.

Mara ya mwisho familia hiyo ilipojaribu kuisimamisha, liliondolewa na wenye mamlaka.