Akshata Murty: Mke wa Rishi Sunak ni nani?

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Kuingia kwa  Rishi Sunak madarakani kumevutia hisia nchini India - na sio tu kwa sababu yeye ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza wa asili ya Asia.

Mkewe Akshata Murty ni binti wa bilionea wa India Narayana Murthy, mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini humo ambaye amepewa jina la Bill Gates wa India.

Mrithi wa utajiri wa mabilioni, Bi Murty aliangaziwa ilipoibuka mapema mwaka huu kwamba alikuwa na hadhi kutolazimika  kulipa ushuru wowote kwa mapato yake kutoka nje ya Uingereza. Baadaye alikubali kulipa ushuru wa Uingereza kwa mapato yake hata ya nje ya Uingereza .

Licha ya utajiri mkubwa wa familia yake, Bi Murty alitoka katika maisha duni.

Katika barua kwa binti yake, iliyochapishwa katika mkusanyiko wa 2013, baba yake alikumbuka jinsi alivyosikia habari za kuzaliwa kwake huko Hubli mnamo Aprili 1980 kutoka kwa mfanyakazi mwenzake kwa sababu familia haikuweza kumudu simu.

"Mimi na mama yako tulikuwa wachanga wakati huo na tukihangaika kupata ustawi  katika kazi zetu," aliandika.

Alipokuwa na umri wa miezi michache tu, Bi Murty alitumwa kuishi bibi yake mzaa mama  huku mama yake, Sudha Murty, na babake wakiendelea na kazi zao huko Mumbai.

Mwaka mmoja baadaye, Bw Murthy alianzisha kampuni ya Infosys, kampuni ya huduma za IT ambayo imemfanya kuwa mmoja wa watu tajiri zaidi nchini India. 

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wazazi wa Bi Murty waliopata mafanikio makubwa   pia walisisitiza umakini wa elimu na bidii kwa watoto wao wawili. Bw Murthy alisema hakuna runinga iliyokuwa  nyumbani kwao ili kupata wakati wa "mambo kama kusoma, majadiliano na kukutana na marafiki".

Aliendelea na masomo ya uchumi na Kifaransa katika Chuo cha kibinafsi cha kiliberali cha Claremont McKenna huko California. Kisha Bi Murty alipata diploma katika chuo cha mitindo kabla ya kufanya kazi katika Deloitte na Unilever na kusomea MBA katika Chuo Kikuu cha Stanford.

Ni  katika chuo kikuu ambapo alikutana na Bw Sunak. Walifunga ndoa mnamo 2009 na wakapata watoto wawili wa kike.

Murty  mwenye umri wa miaka 42 alianza kazi yake ya kifedha huko California kabla ya kuzindua lebo yake ya mitindo, Akshata Designs, ambayo ilizindua mkusanyiko wake wa kwanza mnamo 2011. Aliiambia Vogue India kuwa alifanya kazi na wasanii katika vijiji vya mbali vya India kuunda miundo yake, ambayo ilikuwa kuhusu "uhalisi, ufundi na kulinda urithi  wenye utajiri".

Hata hivyo, gazeti la Guardian liliripoti kuwa biashara hiyo iliporomoka ndani ya miaka mitatu.

TH