Rishi Sunak: Je, kiongozi mpya wa Uingereza atafanya nini kama Waziri Mkuu?

Chanzo cha picha, EPA
Rishi Sunak anatazamiwa kuwa waziri mkuu ajaye wa Uingereza, baada ya kushinda kinyang'anyiro cha kuchukua nafasi ya Liz Truss kama kiongozi wa Chama cha Conservative.
Kansela huyo wa zamani hakutoa ahadi zozote za sera wakati wa kinyanganyiro hicho kilichochukua siku nne au kutoa hotuba au mahojiano yoyote na vyombo vya habari.
Inamaanisha kuwa harakati zake ambazo hazikufanikiwa dhidi ya Bi Truss kuchukua nafasi ya Boris Johnson msimu wa joto zinasalia kuwa kielelezo bora cha sera zake.
Lakini baada ya Bi Truss kukumbwa na msukosuko wa kuhudumu kama waziri mkuu wa wiki sita, maswali makubwa yamesalia kuhusu mipango yake ya siku zijazo.
Je, amesema nini kuhusu kupunguzwa kwa kodi na kukopa kwa serikali?

Chanzo cha picha, PA Media
Wakati wa kinyang'anyiro cha uongozi katika majira ya kiangazi, Bw Sunak alipuuzilia mbali mipango ya Bi Truss ya kupunguzwa kwa ushuru papo hapo kama uchumi wa "simulizi" ambao ungeongeza mfumuko wa bei.
Alionya kuwa mipango yake ilihatarisha gharama kubwa za kukopa za serikali - onyo ambalo liliibuka tena baada ya msukosuko wa kifedha kufuatia bajeti ndogo ya Septemba .
Ingawa alisema alitaka kuona kupunguzwa kwa kodi kwa muda mrefu, alisema kuweka mfumuko wa bei chini ya udhibiti lazima iwe kipaumbele.
Akiwa Chansela aliinua bima ya kitaifa hadi asilimia 1.25, sera ambayo aliitetea katika kampeni yake yote kama muhimu katika kufadhili matumizi yasekta ya Afya.
Kufuatia bajeti ndogo ya Bi Truss, kiwango hicho cha juu kinatarajiwa kupunguzwa kufikia tarehe sita Novemba . Bwana Sunak hajasema iwapo punguzo hilo litaenedelea.
Pia alisema kwamba ataongeza kodi ya ushirikisho kutoka asilimia kumi na tisa hadi asilimia 2 Aprili ijayo , sera ambayo atatendelea kuitekeleza baada ya bi Truss kwenda kinyume na ahadi yake ya kufutilia mbali nyongeza hiyo.
Sekta moja ambayo alijitolea kupunguza , hatahivyo ni kodi - akiahidi kupunguza kiwango cha chini kwa asilimia nne kabla ya mwisho wa bungee lijalo.
Hii inashirikisha asilimia moja ya punguzo mnamo mwezi Aprili , punguzo ambalo bi Truss aliliwasilisha kwa mwaka mmoja kabla ya ahadi hiyo kupotea wakati wa bajeti yake ndogo.
Je aliahidi nini kuhusu nishati na mabadiliko ya hali ya hewa?

Chanzo cha picha, PA Media
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Jinsi bora ya kulinda kila nyumba na biashara dhidi ya gharama ya juu ya nishati pia ilitawala wiki za mwisho za kinyanganyiro cha uongozi huo.
Bwana Sunak alisema kwamba atafutilia mbali VAT katika malipo ya nishati kwa mwaka mmoja, sera ambayo aliipinga alipokuwa Chansela . Pia alisema kwamba atatumia mabilioni ye fedha kuwapatia afueni makundi yasiojiweza.
Hatahivyo, bi Truss hadi wakati huo ameweka mfumo kukabilia ghrama ya nishati katika kila nyumba na biashara , sera aliotabiri itagharimu £10bn kila mwezi.
Mfumo huo ulitarajiwa kutekelezwa kwa miaka miwili – lakini kwasababu ya mabadiliko katika bajeti hiyo ndogo utalazimika kuangaziwa upya mwezi Aprili mwaka ujao.
Iwapo atauongeza mradi huo ama kuubadilisha wote , ni mojawapo ya maamuzi makubwa yanayomkabili bwana Sunak akiwa Waziri Mkuu.
Katika majira ya joto, hakumfuata bi Truss katika kuondoa mgao wa nishati wakati wa majira ya baridi ikiwa ni katika mpango wa kuhifadhi mgao huo.
Kama mtangulizi wake , hatahivyo, alisema kwamba atapinga kuwekwa kwa paneli za jua katika mashamba, na kuunga mkono matumizi ya gesi pale inapohitajika na wakaazi.
Pia alisema kwamba amejitolea kuhkikisha kwamba Uingereza haizalishi gesi chafu kufikia 2050
Je, alisema nini kuhusu NHS na huduma ya afya?

Chanzo cha picha, EPA
Sera ya Afya haikuwa katika kinyanganyiro wakati wa kampeni za majira ya joto, lakini hatahivyo bwana Sunak alitoa ahadi muhimu.
Waziri mkuu mpaya aliahidi kuondoa mud awa mwaka mmoja wa kusubiri kufikia Septemba 2024 ili kuhakikisha kuwa idadi ya watu wanaosubiri tiba ya dharura kushuka kufikia mwaka ujao.
Aliahidi kufanya hivyo kwa kupiga jeki idadi ya vituo vya kutambua maradhi nje ya hospitali ikiwemo kukodi maduka yasiotumika katika barabara kuu.
Kwa lengo la kupunguza uchafu, pia aliahidi kwamba atawapiga watu faini ya hadi £10kwa kukosa kuonana na daktari. Pia aliahidi kuboresha kandarasi za madaktari wa meno na kudhibiti bajeti ya
£3bn waliowekewa.
Je ahadi zake zengine ni zipi
Mashindano hayo ya majira ya kiangazi pia yalishuhudia Bw Sunak akitoa ahadi kadhaa kuhusu uhamiaji, ikiwa ni pamoja na kuweka mpango tata wa Uingereza kupeleka baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda.
Pia aliahidi kuweka kikomo cha mwaka kwa idadi ya wakimbizi ambao Uingereza inawakubali, kuimarisha vigezo vya kufuzu kwa hifadhi, na kunyima misaada kutoka kwa nchi ambazo hazitachukua marejesho ya wahamiaji.
Tofauti na Bi Truss, hakuahidi kuongeza matumizi ya ulinzi hadi 3% ya mapato ya kitaifa ifikapo 2030 - badala yake alisema anataka lengo la sasa la 2% kuonekana kama sakafu.
Kuhusu Brexit, eneo lingine muhimu, Bw Sunak alisema alitaka "kurekebisha" matatizo ya kibiashara yaliyoundwa na Itifaki ya Ireland Kaskazini, na kurekebisha sheria zote za EU ambazo bado ziko kwenye kitabu cha sheria cha Uingereza kufikia uchaguzi mkuu ujao.












