Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita Ukraine: Urusi yakanusha kuwa na mipango ya kutangaza vita Mei 9
Urusi imepuuzilia mbali uvumi kwamba itatangaza vita vya pande zote nchini Ukraine katika siku zijazo kama "upuuzi".
Moscow hadi sasa imekanusha kuwa iko vitani, badala yake ikirejelea uvamizi huo kama "operesheni maalum ya kijeshi".
Lakini maafisa wa Magharibi wanadhani kwamba Rais Vladimir Putin anaweza kutumia Gwaride la Ushindi la Mei 9 kutangaza kuongezeka kwa hatua za kijeshi.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov, hata hivyo, alisema hakuna ukweli kwa uvumi huo "kabisa".
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema wiki iliyopita kwamba gwaride la Moscow - kukumbuka kushindwa kwa Wanazi na kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia - linaweza kutumiwa kupata uungwaji mkono wa uhamasishaji mkubwa wa wanajeshi na kusukuma tena Ukraine.
"Sitashangaa, na sina habari yoyote kuhusu hili, kwamba labda atatangaza siku hiyo ya Mei kwamba 'sasa tuko kwenye vita na Wanazi wa dunia na tunahitaji kuhamasisha watu wa Urusi kwa wingi' ," aliiambia redio ya LBC.
Maafisa wa Urusi wanarejelea tu uvamizi huo kama "operesheni maalum ya kijeshi" ya "kuondoa jeshi" au "kuondoa-Nazi" , wakirejelea madai yasiyo na msingi kuhusu Wanazi katika serikali ya Ukraine ambako Moscow ilitumia kuhalalisha uvamizi huo.
Pamoja na gwaride la kila mwaka huko Moscow, pia kuna ripoti za muda mrefu kwamba Kremlin inapanga aina fulani ya gwaride la ziada katika jiji la Mariupol kusini mwa Ukraine, ambapo iko chini ya udhibiti wa Urusi. Vikosi vya Ukraine vimebaki katika eneo moja la jiji - ambako kuna kiwanda kikubwa cha chuma kinachoitwa Azovstal.
Ripoti za hivi punde zinaonesha kuwa baada ya mafanikio ya hivi karibuni ya kuwahamisha baadhi ya raia, mashambulizi katika eneo hilo yameanza tena na mawasiliano yamepotea na kuna askari waliobaki ndani.
Maafisa wa Ukraine wanasema mitaa ya katikati ya jiji inasafishwa kwa kuondolewa miili na mabomu ambayo hayakulipuka. Sehemu kubwa ya jiji liko katika magofu, baada ya vikosi vya Urusi kulishambulia bila kuchoka kwa wiki kadhaa .
Mwanasiasa wa Ukraine Alyona Shkrum aliiambia BBC kuwa anatarajia mambo kuwa magumu zaidi pamoja na sherehe za siku ya ushindi wa Urusi.
"Kwa Putin na kwa himaya anayojaribu kujenga, kimsingi hii ni siku ya mfano, sawa?" alisema.
"Kwa hivyo anachukua aina fulani ya siku ya ushindi na anaibadilisha kuwa pambano kubwa hivi sasa dhidi ya Wanazi, ambayo ni wazi kuwa ni propaganda za Urusi na ujinga kabisa.
"Tunatarajia kuwa kutakuwa na nyakati ngumu hapa Kyiv na Odesa na Mariupol, na katika miji mingine mnamo Mei 9."
Katika hatari ya kusema wazi, kuna mtu mmoja tu ambaye anaweza kuwa na uhakika kabisa, jinsi Urusi inavyopanga kuadhimisha Siku ya Ushindi ya kila mwaka mnamo Mei 9 naye ni Vladimir Putin.
Na anaweka kadi zake karibu na kifua chake.
Kukanusha kwa Moscow kwamba inapanga kutangaza vita siku hiyo kunahitaji kuchukuliwa kwa msisitizo zaidi.
Katika siku zilizotangulia uvamizi wa Februari 24, maafisa wa Urusi walipanga foleni kukejeli maoni ya uvamizi unaokuja kama "hasira na propaganda za magharibi". Hata hivyo walivamia, na kukamata hata Waukraine wengi kwa kuwashtukiza.
Kwa hivyo kwa kiasi fulani tunachoweza kutarajia ni matangazo ya ushindi ya malengo yaliyofikiwa na maadui (wa kweli au wa kufikiria) wameshindwa.
Lawama kwa kasi ndogo ya maendeleo ya Urusi katika eneo la mashariki la Donbas huenda ikawekwa kwa Nato na pengine kutakuwa na maonyo zaidi kwa nchi za Magharibi kuacha kuisaidia Ukraine kujilinda.
Chochote kitakachotokea tarehe 9 Mei ni vigumu kuona vita hivi vikiisha hivi karibuni.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine