Jinsi mtoto aliyezaliwa njiti, bila mkono mmoja anavyojiona shujaa kwa kupata mkono bandia

Iliyochapishwa

Wakati ambao Jacob alipozaliwa wiki nane kabla ya siku zake za kuzaliwa kutimia, sehemu kubwa ya mkono wake wa kushoto ulikuwa unapotea.

Wazazi wake Gemma Turner na Chris Scrimshaw,kutoka Calderdale huko West Yorkshire, walifadhiliwa £16,000 kwa ajili yake.

Wakati wa kampeni hizo, hapo ndipo Ben Ryan, kutoka Menai Bridge on Anglesey, alipokuja kumbunia mkono Jacob, ambaye ana umri wa miaka mitano sasa.

Bwana Ryan alianza kubuni kutengeneza mkono wa mtoto huyo wakati akiwa na siku 10.

Unaweza pia kusoma:

Hatua hii ilimpelekea aache kazi yake ya ualimu wa saikolojia na kuanzisha kampuni yake mwenyewe miaka miwili na nusu iliyopita na kuiita 'Ambionics'.

Mteja wake wa kwanza akiwa mtoto Jacob.

Bwana Ryan amekuwa akifanya kazi karibu na familia ya mtoto huyo ili kupata mkono mzuri.

Familia yake walitaka kiwiko ambacho kitawekwa katika sehemu ambayo itamuwezesha kumrahisishia kufanya shughuli mbalimbali.

Bwana Ryan alisema kuwa mkono huo umebuniwa kwa namna ambayo inampa urahisi kwa Jacob kuukunja.

Aliutengeneza kwa ajili ya kufanya kazi kama mkono wa kawaida.

Lakini kwa upande wake Jacob, jambo la muhimu kwake ilikuwa rangi ya kijani ambayo alijiona shujaa.

"Kile nilichokitengeneza ni matakwa ya Jacob, mtoto huyo alitaka mkono mkubwa na hivyo huo mkono aliotengeneza ulikuwa sahihi kwake", alisema bw. Ryan.

Aliongeza kusema kuwa wakati anamvalisha mkono huo , matarajio yalizidi yale ambayo walitegemea.

"Sasa anaweza kumkumbatia kaka yake na kumpapasa kwa mkono wake" alisema.

Jacob alifurahia sana kuvaa mkono wake mpya na haimsumbui kuonekana kuwa tofauti na watu wengine wote.

Jambo lililobaki kwa Jacob ni kuzoea kutumia mkono huo tu, alisema mama yake.

Wakati wanachangisha fedha kwa watu , mtu ambaye hawamfahamu alitoa £5,000 - alisema kuwa alikuwa anaumwa sana na asingeweza kumaliza kile alichonacho.

Mwanzoni Gemma aliona kuwa kuna ugumu sana kuomba fedha kwa watu ambao hawajui ili kumtibia mwanae.

"Familia hii haikuwa na bahati ya kupata msaada wa kumsaidia Jacob ," alisema Ryan.

"Hakuna mtu ambaye alijitokeza na kitu ambacho kingeweza kumsaidia Jacob".