Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 08.03.2022: Ronaldo, Rashford, Haaland, Paqueta, Martinelli, Nkunku
Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo huenda akahamia Paris St-Germain, ambayo inapania kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kuungana na mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, ikiwa Manchester United itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Football Transfers)
Arsenal, Newcastle na West Ham ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Uingereza Rashford huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akiaminika kufikiria hatma yake Manchester United. (90Min)
Paris St-Germain pia watajaribu kumsaini Rashford ikiwa Mfaransa Kylian Mbappe,23, atajiunga na Real Madrid. PSG ilijaribu kumsajili Rashford lmsimu uliopita lakini United hawakuwa tayari kumuuza. (Mail)
Manchester City na Real Madrid ni klabu mbili zinazoongoza katika mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland licha ya Bayern Munich na Barcelona kuonyesha nia ya kumtaka kiungo huyo matata. Hatma ya Haaland mwenye umri wa miaka 21- raia wa Norway inatarajiwa kuamuliwa katika "wiki chache zijazo ". (Athletic - Usajili unahitajika)
Mmiliki wa New York Jets Robert Wood Johnson anajiandaa kutoa ofa ya kuinunua Chelsea. Johnson anachukuliwa kuwa "mjuzi sana" wa klabu na Ligi ya Premia na aliwahi akuishi London kama balozi wa Marekani nchini Uingereza.(ESPN)
Muungano wa kibinafsi wa Saudi Media pia umefanya mawasiliano na kampuni ya Kimarekani ya Raine Group - ambayo inasimamia mauzo ya Chelsea - kuhusu kuinunua klabu hiyo kutoka kwa Roman Abramovich. (Goal)
Newcastle wameanzisha amazungumzo na Real Madrid kuhusu uhamisho wa mchezaji nyota wa Ubelgiji Eden Hazard, 31, ambaye anatarajiwa kuondoka mji huo mkuu wa Uhispania msimu wa joto. (Defensa Central -kwa Kihispani)
Arsenal wako tayari kumenyana na Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha kusajilikiungo mshambulizi wa Brazil Lucas Paqueta, 24, kutoka Lyon. (Calciomercato - kwa Kitaliano)
Mashambuliaji wa Brazil Gabriel Martinelli, 20, anasema anataka kusalia Arsenal kupigania kombe licha ya Liverpool kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. (Liverpool Echo)
Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa klabu zinazomnyatia kiungo wa kati wa Mfaransa wa RB Leipzig Christopher Nkunku. Mchezaji huyo wa miaka 24- huenda akagharimu karibu £62m. (Foot Mercato, via Express)
Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wamekejeli CV ya kocha wa muda Ralf Rangnick na kutoridhishwa na mbinu za Mherumani huyo. (MEN)
Juan Mata will ataondoka Manchester United kama mchezaji huru msimu wa joto huku kiungo huyo wa kati Mhispania mwenye umri wa miaka 33- akitakiwa na klabu kadhaa za La Liga. (Athletic - subscription required)