Uamuzi wa Abramovich kuiuza Chelsea: 'Sielewi kwanini' - Kocha wa Blues Thomas Tuchel

Iliyochapishwa

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel amesema amebaki gizani kuwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anaiuza klabu hiyo, ila Mjerumani huyo anatarajia uwepo wa "mabadiliko makubwa".

Mfanyabiashara huyo wa Urusi alitoa taarifa kabla ya ushindi wa Chelsea wa raundi ya tano ya Kombe la FA katika uwanja wa Luton akiuita "uamuzi mgumu sana wa kufanya".

Abramovich amekuwa mmiliki wa Chelsea tangu mwaka 2003 na kushinda mataji makubwa 19.

"Ni mapema mno kuzungumza, kwa sababu naweza tu kufikiria Chelsea yenye Roman Abramovich," alisema Tuchel.

"Imekuwa ngumu sana kwangu. Ni mabadiliko makubwa ya kweli. Hatukuzungumza juu ya hili [kabla ya Luton]. Tumekubali.

"Wachezaji wanatumia mitandao, wanaangalia TV kwa hivyo wanajua, wanapata ujumbe. Lakini tulizingatia maandalizi tu juu ya michezo yetu.

"na labda inawezekana baadhi ya wachezaji wamethirika zaidi, wengine hawajaathirika, lakini mwishowe tuliweza kuzingatia mchezo wetu na kutafuta namna ya kushinda."

Baada ya kuinunua klabu hiyo ya Stamford Bridge kwa dau la £140m, mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 55 sasa anadaiwa kuiza klabu hiyo kwa thamani klabu hiyo kwa kiasi cha £3bn.

Katika taarifa yake Abramovich anasema "haijawahi kuwa kuhusu biashara au pesa, lakini juu ya mapenzi na shauku safi kwa mchezo na klabu", akisema mapato ya mauzo yatapelekwa kwa "waathiriwa wa vita nchini Ukraine".

Hii inafuatia taarifa ya Jumamosi ambapo Abramovich alitangaza kuiacha majukumu ya "usimamizi na utunzaji" wa Chelsea kwa bodi ya wadhamini wake kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

"Sidhani kama ninahitaji kuzungumzia suala hili, sifahamu mengi kama unavyofikiria," aliongeza Tuchel. "Mimi si mtendaji mkuu au mjumbe wa bodi. Kwa hivyo, nina hakika klabu itazungumza na sisi na wachezaji.

'Msingi wa makombe'

Mchambuzi wa BBC Radio 5 Live John Murray anasema Abramovich kuiuza klabu hiyo ni "moja ya nyakati muhimu zaidi katika historia nzima ya Chelsea na miongo miwili iliyopita ya Ligi Kuu ya England".

"Katika kipindi chake walikuwa na mafanikio zaidi ya timu zote katika Ligi Kuu," alisema. "Imekuwa njia ambayo ameendesha klabu, kuwekeza pesa. Kabla ya hapo hatukuwahi kujua kitu chochote ambacho Roman Abramovich alifanya.

"Awali Chelsea iliamini kwamba kuwa imara maana yake ni mafanikio, Chelsea chini ya Roman Abramovich ilibadilisha mtazamo huo kwa sababu waliendelea kubadilisha mameneja wao lakini jambo moja ambalo halikubadilika ni ukanda wa mataji."

Hata hivyo, winga wa zamani wa Chelsea Pat Nevin anasema habari hii ya Abramovich haijamshangaza "pengine amechagua chaguo sahihi", licha ya kubadilisha muelekeo wa klabu hiyo katika miaka yake 19 huko Stamford Bridge.

Hakuna kulaani kuhusu anayoendelea Ukraine

Beki wa zamani wa Manchester City Micah Richards aliiambia BBC kwamba Tuchel alikuwa anajitoa kwenye lawama lakini Alan Shearer anaamini kuwa watendaji wa klabu walipaswa kuja mbele ya vyombo vya habari badala ya bosi wa Chelsea.

"Thomas Tuchel hakuwa na Amani wakati anajibu maswali," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa England. "Sio kitu ikilinganishwa na hali waliyonayo watu maskini wa Ukraine katika wakati huu.

"Anapaswa kuwaomba watendaji walio juu yake wajibu, labda anawaambia ila hawamsikilizi. Inaathiri kila mtu, sisi sote tunaangalia habari. Wewe si binadamu kama haikuathiri."

Shearer pia alieleza mauzo yanaweza kuchukua miezi au miaka, na kuongeza kuwa ni "wakati muhimu" kwa Chelsea kwa sababu ya "mafanikio makubwa" waliyopata wakati wa utawala wa Abramovich.