Hawa ndio wakina 'Mbappe' wa Afrika na Amerika

Julian Alvarez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Julian Alvarez
Iliyochapishwa

Kwa wafuatiliaji wa soka, bila shaka hakuna aliyemfahamu Kylian Mbappe, nyota wa Ufaransa anayechezea Klabu ya Ufaransa ya PSG. Wiki iliyopita alifunga bao muhimu katika mchezo wa ushindi wa 1-0 wa ligi ya mabingwa Ulaa dhidi ya Real Madrid.

Alianza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 16 pale Monaco na kufanikiwa kutwaa taji la ligi kuu ya Ufaransa 'league 1, na kutwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi Ulaya. Katika umri wa miaka 23 aliyonayo sasa, amefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu Ufaransa mara tatu, amekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo kwa misimu mitatu mfululizo, na ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa ufaransa mara mbili.

Ameanza kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa akiwa na miaka 17 na ndani ya mwaka mmoja akaisaidia kutwaa kombe la dunia akiibuka mfungaji bora wa pamoja kwa kupachika mabao. Alifunga katika fainali dhidi ya Croatia na kuwa mchezaji kinda wa pili duniani kwa kufunga goli kwenye fainali , akiwa nyuma ya Pele, gwiji la Brazil.

Anatajwa kama mchezaji bora kwa sasa duniani akiwa kundi moja na kina Lewandsik, Halaaand, Salah… na anayetajwa kuwa mrithi ajaye wa wachezaji nguli wa daraja la pekee, Messi na Ronaldo. Kasi, akili ya mpira, uwezo wake wa kukokota mpira na uwezo wake wa kufunga mabao unamuweka daraja tofauti la mchezaji ataketawala doka la dunia katika miaka 7 mpaka 10 ijayo.

Mkataba wake na PSG unakamilika mwishoni mwa msimu, huku timu hiyo ikiandaa kumshawishi kwa kumpa mkataba utakaomfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani kuliko wote ili kumzuia asiende Real Madrid.

Wakati bara la Ulaya wana Mbappe, Afrika, Asia na Amerika pia wana 'Mbappe' wao wanaotazamwa kutawala soka na kupeperusha sifa za mabara yao. Miongoni mwao ni hawa wafuatao;

Julian Alvarez 'Mbappe' wa Amerika

Julian Alvarez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Julian Alvarez

Ni mshambuliaji kinda wa miaka 21, ambaye tayari ni gumzo kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao na kasi kwenye mchezo. Anachezea River Plate ya Argentina. Na sifa yake ya kupachika mabo, inamfanya afananishwe na gwiji la Argentina, Sergio Aguerro.

Na haishangazi, Klabu kubwa kama Manchester City, vinara na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England 'EPL', kumsajili kwa kitita cha kueleweka ili kuziba nafasi ya Aguerro ambaye aliikacha timu hiyo na kutimkia Barcelona, kabla ya kubainika kuwa na matatizo ya moyo, yaliomfanya atundike daruga.

Juma lililopita, amepachika mabao matatu 'hat-trick' dhidi ya Patronato na kusifiwa sana na kocha wa City, Pep Gurdiola, 'ni mchezaji mzuri, mwenye kipaji na atakuwa msaada katika miaka mingi ijayo', alisema Pep mbele ya waandishi wa habari hivi karibuni.

Read Madrid walivutiwa nae akiwa kinda wa miaka 11, alipofanya majaribio na klabu hiyo ya Hispania, kilichozuia asisajiliwa ni sharti u la umri wake kutokana na sheria na kanuni za wakati huo. Lakini akaibukia ligi ya Argentina akiwa na River Plate, klabu anayoishabikia tangu akiwa na miaka 4. Msimu uliopita aliibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 18.

Licha ya kutokuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza, Alvarez alijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kilichoshiriki kombe la dunia mwaka 2018 huro Urusi, ili kukaa karibu na kina Messi, Aguerro na Di Maria, kupata uzoefu.

Hasa baada ya kusajiliwa na Manchester City, katika dirisha lililopita la mwezi Januari na kubakizwa River plate kwa mkopo mpaka Mwezi Juni, 2022, macho ya watu wengi nje ya bara lake wameanza kumfuatilia. Hakuna namna dunia itaacha kutambua uwezo wake wa sasa.

Shirikisho la soka na watu wa benchi la ufundi walijua uwezo wake tangu akiwa na miaka 17 kwamba angefaa kuwa msaada kwenye timu ya taifa. Leo akiwa ameichezea Argentina michezo chini ya 10 anatajwa kama mrithi wa Messi kwenye timu ya taifa ya Argentina atakayetawala kipindi cha miaka 10 ijayo lakini anatazamwa kama 'Mbappe' mwingine kwenye soka la Amerika Kusini na Kaskazini, atakayewika na Manchester City.

Wakati Afrika ikiendelea kuona kina Mohamed Salah na Sadio Mane wakitawala sasa soka la bara hilo na kutarajiwa kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika. Wako vijana wadogo ambao… hawawezi kuwa 'Mbape' wa kesho ila wana nafasi ya kufanya vyema katika asoka duniani.

Issa Kabore

Issa kabore

Chanzo cha picha, BSR Agency/getty images

Maelezo ya picha, issa kabore wa Burkina Fasso

Huyu ni mlinzi wa kulia wa Manchester City, anayechezea kwa mkopo klabu dada ya City, ESTAC Troyes. Katika mashindano yaliyopita ya kombe la Afrika, AFCON, aliibuka mchezaji bora wa mashindano hayo, akitoa pasi 3 za mabao.

Kwa mlinzi kuwa katika nafasi muhimu ya kuchangia mabao, kwa kiwango hicho kwenye mashindano makubwa kama hayo ya Afrika ni jambo linalomweka juu miongoni mwa wanasoka chipukizi Afrika

Abde Ezzalzouli,

Winga wa Barcelona na Morocco, Abde Ezzalzouli

Chanzo cha picha, facebook

Maelezo ya picha, Winga wa Barcelona na Morocco, Abde Ezzalzouli

Winga wa Barcelona na Morocco, Abde Ezzalzouli, 20, anaangaliwa kama mfalme ajaye wa soka la Afrika kama ataendelea kuwa timamu kimwili. Ni mchezaji wa kwanza kuichezea Barcelona akiichezea timu hiyo kwa mara a kwanza mwezi Oktoba mwaka jana.