Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Juhudi za kupata tiba zimefikia wapi?
Ni kana kwamba maarifa zaidi yanahitajika kusaidia kupatikana kwa dawa ya kukabiliana na janga la corona ambalo linaendelea kumaliza wengi.
Je kipi kinaweza kuwa mkombozi wa changamoto ya janga la corona?
Kampuni zinajaribu kuja na suluhu mbalimbali.
Kampuni ya utengenezaji dawa ya Exscientia, ilikuwa ya kwanza kutoa dawa iliyofikia hatua ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu, inafuatilia dawa 15,000 kutoka taasisi ya utafiti ya Scripps, California.
Na Healx, kampuni moja ya Cambridge iliyoanzishwa na mvumbuzi mwenza wa dawa ya Viagra Dr David Brown, imefanya mabadiliko ili kugeukiwa uchunguzi wa kuvumbua wa dawa za magonjwa nadra.
Mfumo unaofuatwa umegawanywa mara tatu:
- Kufanya utafiti wa kila ugonjwa wenye kuonesha uhusiano na wa virusi vya corona
- Kufanya utafiti wa vinasaba na muundo wa virusi vyenyewe
- Kuangalia dawa ambazo huenda zikawa na ukaribu na ugonjwa huu
Kawaida mchakato wa utengenezaji dawa mpya umekuwa wa polepole.
"Nimekuwa nikifanya kazi hii kwa miaka 45 na nimefanikiwa kutoa dawa tatu ambazo zipo sokoni," Daktari Brown ameiambia BBC News.
Lakini kampuni ya Brown inajitahidi kwenda kwa kasi.
"Imechukua wiki kadhaa kupata taarifa tunazohitaji na pia tumepata taarifa mpya siku chache zilizopita, na sasa tuko kwenye kipindi muhimu mnoo," Daktari Brown amesema.
"Mchakato ulianza sikukuu ya pasaka na tutakuwa na matokeo ya njia hizo tatu siku saba zijazo."
Kampuni ya Healx inatarajia kwamba taarifa hizo zitawezesha kutengenezwa kwa dawa kadhaa kufikia Mei na tayari inafanya mazungumzo na maabara kadhaa kuchukua matokeo hayo na kuyapeleka kwenye kliniki ili kufanyiwa majaribio.
Kwa waliopo kwenye nyanja ya kutafuta dawa, wana machaguo mawili linapokuja suala la virusi vya corona:
- Kutafuta dawa mpya kabisa na wasubiri miaka kadha kabla ya kuidhinishwa kuwa salama kwa matumizi
- Ama kuboresha dawa ambazo tayari zinafanya kazi kutibu magonjwa mengine
Lakini kulingana na Daktari Brown ni vigumu sana kwa dawa moja kuibuka kuwa na uwezo wa kutibu virusi vya corona.
Prof Ara Darzi, mkurugenzi wa taasisi ya uvumbuzi wa dawa duniani, imeambia BBC: Kampuni ya Healx ni moja ya zinazotegemewa kupata uvumbuzi wa dawa ya corona lakini kuna haja ya kuwa na takwimu za kutosha.
"Hadi kufikia sasa, data kama hizi zina makampuni binafsi.
"Sasa kuna haja kubwa ya kukusanya pamoja data zote hizo ili kuwezesha upatikanaji wa dawa mpya itakayotibu ugonjwa wa Covid-19 haraka iwezekanavyo."
Utafiti wa kushangaza
Kawaida, kuleta makampuni pamoja ili kushirikiana inachukua mwaka mzima", amesema mkuu wa kampuni ya utengezaji dawa ya Schipher, Alif Saleh.
Lakini kupitia teknolojia kama vile mikutano kwa njia ya video kumeharakisha mazungumzo kwa makampuni ya kutengenza dawa ya kukabiliana na civid-19.
"Kile ambacho kimefanyika katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, kingefanyika kwa kipindi cha nusu mwaka," alisema.
Tayari utafiti ambao umefanywa na makampuni hayo umezindua matokeo ya kushangaza:
- Virusi vya corona vinaweza kuingia kwenye tishu za ubongo na hilo linaelezea kwanini baadhi ya watu wanapoteza hamu ya kula na ukosefu wa uwezo wa kuvuta harufu.
- Pia unaweza kuathiri mfumo wa afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake.
Hadi kufikia sasa, utafiti umefanikiwa kubaini dawa 81 ambazo zinaweza kuwa na mchango mkubwa.
Lakini njia zote tatu zinahitaji kujumuishwa pamoja.
"Mbinu tofauti tofauti zinatumika kwa mitazamo tofauti lakini zote zina zina uhakika" alisema Profesa Albert-Laszlo Barabasi.
Kuna baadhi ya kampuni za kutengeneza dawa zinazosema kwamba tayari zimegundua dawa ambazo zinaweza kusaidia pakubwa kupata tiba ya virusi vya corona.
Kampuni ya Benevolent imetambua dawa ya Baricitinib, ambayo inatumika kutibu ugonjwa wa baridi yabisi, yaani rheumatoid arthritis kama yenye uwezo wa kutibu na kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kwenye seli za mapafu.
Na kwasasa inafanyiwa majaribio na Taasisi ya Taifa ya Marekani ya kukabiliana na Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio.
Wakati huohuo, wanasayansi kutoka Korea Kusini na Marekani wanafanya utafiti wa uwezekano wa dawa za kuzuia maambukizi na kupendekeza kwamba dawa ya Atazanavir, inayotumika kudhibiti makali ya Ukimwi, inaweza kuwa dawa nzuri zaidi.
Kampuni zingine zinachunguza kufahamu ni wagonjwa gani watakaokuwa na uhitaji wa mashine za kupumua.
Kampuni ya Teknolojia ya Alibaba, kwa mfano, imetangaza kifaa chenye uwezo wa kubaini ugonjwa huo ndani ya sekunde 20, ambacho usahihi wake ni asilimia 96.
Kuna haja ya kuimarisha juhudi za kimataifa kuanzia kwa watungaji wa sera, kushawishi makampuni makubwa ya kutengeneza dawa kushirikiana na kampuni ndogo, wanasayansi na mashirika ya utafiti kuleta pamoja raslimali za upatikanaji wa takwimu, amesema Profesa Darzi.
"Hiki ni kipindi muhimu sana cha kupata takwimu za dawa ili kusaidia kukabiliaba na ugonjwa wa Covid-19," alisema.