Virusi vya corona: Mwanariadha wa Kenya Wilson Kipsang akamatwa kwa kulewa wakati wa amri ya kutotoka nje

Wilson Kipsang

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Bingwa wa zamani wa mbio za marathon duniani Wilson Kipsang
Iliyochapishwa

Aliyekua bingwa wa mbio za marathon nchini Kenya Wilson Kipsang ameachiliwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa kukiuka amri ya kutotoka nje iliotolewa na serikali ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Kipsang aliyeshinda rekodi ya dunia katika mbio za marathon mjini Berlin mwaka 2013 ni afisa wa polisi nchini Kenya.

Alikiri kupatikana na hatia katika mahakama siku ya Ijumaa baada ya kulala katika kizuizi cha polisi kabla ya kuachiliwa kwa dhama ya $47.

Maelezo ya sauti, Wachezaji wa Barcelona kupunguziwa mishahara

Kwa sasa anahudumia marufuku kutoka kwa shirika linalokabiliana na madawa ya kusisimua misuli duniani AIU.

"Tulimkamata Kipsang na watu wengine tisa akiwemo mmoja wa maafisa wa kaunti hii katika klbau cha burudani cha Keelu Resort wakinywa na kucheza pool mwendo wa saa nne usiku'', kamanda wa polisi katika kaunti ya Iten John Mwinzi alinukuliwa akisema na chombo cha habari cha AFP.

"Haya ni makossa makubwa sana . Hawa ni watu wanaoheshimika na wanafaa kuwa mfano kwa wengine na sio kuvunja maagizo ya serikali'', bwana Mwinzi'' aliongezea

Bingwa wa zamani wa mbio za London Marathon Wilson Kipsang
Maelezo ya picha, Bingwa wa zamani wa mbio za London Marathon Wilson Kipsang

Bwana Mwinzi pia aliagiza kukamatwa kwa wanariadha wengine 12 , ikiwemo wawili wa kigeni , waliopatikana wakifanya mazoezi katika eneo la Iten Magharibi , eneo linalovutia wanariadhaa maarufu nchini Kenya na wale wa kigeni .

''Kundi hilo lilikiuka sheria ya kutokaribiana'', aliongezea bwana Mwinzi