Jonathan Dos Santos aingia Mexico, 55' Brazil 1-0 Mexico
Ni mabadiliko ya kutafuta bao la kusawazisha baada ya Brazil kuchukua uongozi!
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan
Ni mabadiliko ya kutafuta bao la kusawazisha baada ya Brazil kuchukua uongozi!
Mchezaji wa bei ya juu zaidi duniani amedhihirisha ni kwa nini PSG ililipa Euro Milioni 200 kumsaini!
Bao lake limeiweka Brazil mbele!
Neymar ametengeza nafasi 14 za kufunga magoli Kombe la Dunia kufikia sasa.
Hii ni baada ya kubuni nafasi 3 dhidi ya Mexico mechi inayoendelea na kuwa mchezaji mwenye kuunda nafasi zaidi Kombe hili.
Linaudhi kufahamu kuwa Brazil imefunga mabao 5 pekee hadi sasa.
Gabriel Jesus tayari amemlazimu kipa wa Mexico Ochoa, kutema shuti zake.
Je, atachukua majukumu ya Neymar na Coutinho ya ufungaji magoli?
Alijaribu kumzuia Carlos Vela, lakini akasababisha mkwaju wa ikabu.
Mkwaju wa ikabu kwa Mexico!
Edison Alvarez wa Mexico amepokea kadi ya njano kwa kumkanyaga staa huyo.
Neymar amepiga nje frikiki iliyopewa Brazil.
Ni mpira wa kipa kwa sasa.
Mashabiki wa Arsenal wanafahamu vyema sana kwani aliwahi kuitumikia timu hiyo.
Lakini mechini, mabeki wa Brazil wameweza kutambua uwezo wake.
Neymar alikosolewa awali kwa kuwekeza kwa nywele zake, badala ya kuisaidia Brazil.
Lakini hata baada ya kuingia kwenye mechi, bado makali yake hayajaonekana.
Mabeki wa Mexico wamekaba kweli kweli.
Carlos Vela na nafasi nzuri kwenye sanduku, lakini mkwaju wake umepaa!
Messi wa Argentina na Ronaldo wa Ureno kwa sasa wanatazama mechi za Kombe la Dunia tofauti na awali walipotazamwa, je, Nyota wa Brazil Neymar, ataondoka nao?
Neymar amefunga bao moja tu Kombe la Dunia.
Iliichukua Brazil dakika kumiliki mpira mbele ya lango la Mexico.
Coutinho, amekatazwa. Jesus hakufanikiwa na sasa mpira unamilikiwa na Mexico.
Neymar alikaribia kuipa Brazil uongozi, lakini kipa wa Mexico amepangua!
Andres Guardado, Carlos Vela, Hirving Lozano na Javier Hernandez 'Chicharito' wamekita kambi goli Brazil.
Dalili za Mexico kupata bao mechini?
Kumbuka Brazil ililazimishwa sare na Uswizi mechi yake ya kwanza.
Usisahau kuwa waliwaliza mabingwa wa 2014, Ujerumani, mechi ya kwanza Kundi F Kombe la hili.
......Watatu hao wanastahili kucheza kwa makini zaidi la sivyo, atakayepokea kadi ya njano hatoshiriki Robo fainali.
Hilo huenda likaathiri mipango ya Brazil kuondoka na Kombe mwaka huu!
Achia mbali Neymar, kutana na Chicharito, nyota wa zamani wa Manchester United.