Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan

Kombe la Dunia 2018: Ubelgiji 3-2 Japan

Moja kwa moja

  1. Nafasi safi Hazard lakini Yoshida amnyima!, 36' Ubelgiji 0-0 Japan

  2. Hatari Japan, lango la Ubelgiji, 35' Ubelgiji 0-0 Japan

    Kompany ameondoa.

  3. Inuuuuuiiii, 33' Ubelgiji 0-0 Japan

    Nafasi nusu Japan lakini kichwa cha Inui kimetua viganja vya Courtois kwa utulivu!

  4. Hazard aachilia kitu, 27' Ubelgiji 0-0 Japan

    lakini Eiji Kawashima amnyima!

  5. Lukaku anaijua Japan, 25' Ubelgiji 0-0 Japan

    Lukaku amekosa, lakini ni onyo tu kwa sasa!

    ........Mwezi Novemba mwaka uliopita, ndio mara ya mwisho timu hizi kuchuana.

    Romelu Lukaku ndiye alikuwa mfungaji wa goli pekee lililoshuhudiwa mechi hiyo, Ubelgiji ikiondoka na ushindi wa 1-0.

  6. Japan yajitahidi, 20' Ubelgiji 0-0 Japan

    Lukaku anajaribu, lakini walinzi hawamruhusu! Kona Ubelgiji.

  7. Kwa nini Japan iwe makini dhidi ya Ubelgiji?, 18' Ubelgiji 0-0 Japan

    Kufikia sasa Ubelgiji imejipa mabao 9 Kombe la Dunia, Lukaku akifunga 4!

    Hakuna timu yenye mabao kama hayo!

    Mbali na Croatia na Uruguay, Ubelgiji pia imeshinda mechi zake zote za makundi!

  8. Nani atakosa robo fainali iwapo atalishwa kadi ya njano?, 15' Ubelgiji 0-0 Japan

    Brazil inajilaumu kwa sasa kwani Casemiro hatoshiriki robo fainali kwa kukusanya kadi mbili za njano. Lakini nani atajiunga naye?

    Ubelgiji: Thomas Meunier, Jan Vertonghen, Kevin De Bruyne, Youri Tielemans na Leander Dendoncker:

    Japan: Kawashima, Hasebe, Tomoaki Makino na Takashi Inui.

  9. Ubelgiji na Japan wacheza kwa taharuki, 11' Ubelgiji 0-0 Japan

    Inui amechanja krosi safi, akimtafuta Haraguchi, lakini beki Kompany ameondoa.

    Ushambulizi umeingia eneo la Japan sasa, lakini ni mpira wa juu.

  10. Romelu Lukaku mfukoni?, 08' Ubelgiji 0-0 Japan

    Mlinzi wa Southampton Maya Yoshida amemzuia Lukaku na kumnyamazisha mechini. Lukaku anazuilika kweli?

  11. Hazard hatari kwa Japan, 06' Ubelgiji 0-0 Japan

    Kiungo huyo ameachilia chenga chenga zake mechini, na kuwatatiza Japan.

  12. Senagal inashiriki Kombe la Dunia, kwa njia gani?, 05' Ubelgiji 0-0 Japan

    Refa wa mechi hii ni Malang Diedhiou kutoka Senegal.

    Ni timu ya soka imetolewa, lakini taifa linazidi kuwakilishwa.

    Alikuwa mwamuzi mechi za (Costa Rica 0-1 Serbia na Uruguay 3-0 Urusi).

  13. Nani atajiunga na Brazil Kazan Arena, Kazan Ijumaa?, 01' Ubelgiji 0-0 Japan

    Mshindi wa mechi hii atashiriki robo fainali dhidi ya bingwa mara 5 wa Dunia, Brazil.

  14. Kipenga kimepigwa Rostov Arena, 00' Ubelgiji 0-0 Japan

  15. Lukaku ana kwa ana na Harry Kane, Ubelgiji 0-0 Japan

    Mbio za kiatu cha dhahabu zarejea tena! Baada ya Ronaldo na Ureno kutoka,

    wanaoongoza sasa ni:

    Harry Kane, Uingereza: Mabao 5

    Romelu Lukaku, Ubelgiji: Mabao 4.

  16. Tangu 2002, Ubelgiji 0-0 Japan

    Ubelgiji na Japan wamewahi kukutana mara moja pekee katika Kombe la Dunia.

    Japan ilikuwa mwenyeji mwenza wa Dimba la Dunia mwaka huo.

    Walitoka sare 2-2.

  17. Japan imejipanga, hakuna uoga dhidi ya Ubelgiji!, Ubelgiji 0-0 Japan

    Ni wachezaji sita wapya kikosi cha Japan: Shinji Kagawa, Makoto Hasebe, Takashi Inui, Genki Haraguchi, beki Gen Shoji na mfungaji Yuya Osako wamerudi.

    Safu kamili ya Japan: Kawashima, Shoji, Nagatomo, Sakai, Yoshida, Shibasaki, Haraguchi, Kagawa, Inui, Hasebe, Osako

  18. Ubelgiji waingia na magwiji!, Ubelgiji 0-0 Japan

    Nyota wa Manchester United Romelu Lukaku, Kiungo wa Chelsea Eden Hazard, Mweka pasi hodari Kevin de Bruyne wa Manchester City na kipa wa Chelsea Thibaut Courtois wamerejea kikosini Ubelgiji baada ya kupumzisha misuli wakionana na Uingereza kipute kilichopita.

    Vincent Kompany wa Manchester City atashirikiana na Jan Vertonghen wa Spurs.

    Ubelgiji wameandaa kikosi cha kustajaabisha baada ya kuwataja wachezaji 10 wapya tofauti na kikosi kilichochuana na Uingereza siku chache zilizopita. Mabadiliko ya aina hiyo yameshuhudiwa mwisho 2006 wakati Uhispania iliwaleta wachezaji 11 wapya wakikwatuana na Saudi Arabia.

    Kikosi cha Ubelgiji: Courtois, Alderweireld, Kompany, Vertonghen, Meunier, De Bruyne, Witsel, Carrasco, Mertens, Hazard, Lukaku

  19. Lukaku na Hazard waanza: Japan taabani, Mchuano ujao wa hatua ya muondoano.

    Brazil imewasili robo fainali, Mexico iko nyumbani kuelekea nyumabani.......lakini

    ........Kidogo tuvuke hadi mchuano wa pili wa mchujo Kombe la Dunia siku hii ya Jumatatu......

    Washambulizi hawa wanarejea baada ya kupumzishwa dhidi ya Uingereza mechi ya mwisho ya makundi.

    Mshindi atachuana na Brazil Ijumaa.

    Tutakuletea matangazo ya mechi hii...

  20. Neymar aiondoa Mexico, Brazil yatua robo fainali mara ya 7 mfululizo., Matokeo: Brazil 2-0 Mexico

    Baada ya Mbappe wa Ufaransa Kuitoa Argentina, Cavani wa Uruguay kuitema Ureno, Neymar naye hakuchelea kuong'aa kwenye mechi iliyotabiriwa kuwa na uwezo wa kukatiza maazimio ya Brazil kuliinua Kombe la Dunia mara yao ya 6.

    Mexico iliwatatiza mabeki wa Brazil Neymar hakuwa na uoga mbele ya lango na kila alipoona mwanya, alifyatua kombora.

    Kufikia sasa Neymar ameandikisha shuti 23 dhidi ya wapinzani huku 12 mikwaju (12) ikizuiwa na wadakaji.

    Nyota huyo wa PSG pia ameonyesha ukarimu wake kwa wenzake kwa kubuni fursa 16, zaidi ya wafungaji wengine wote Kombe la Dunia kufikia sasa.

    Mexico ilianza mchuano ikijaribu mbinu ilizotumia dhidi ya Ujerumani za kufunga goli la mapema na kukusanyana mbele ya lango lao.

    Ushirikiano bora kati ya kipa wa Brazil Alisson Becker na walinzi wake Thiago Silva pamoja na Miranda ulikatiza mipango ya Carlos Vela na Javier Hernandez marufu Chicharito.

    Licha ya timu zote kutekeleza uvamizi, pande hizo zilienda mapumziko bila kufungana.

    Kipindi cha Pili:

    Brazil iliingia awamu ya pili kwa hamasa na kuhitaji tu dakika sita kuchukua uongozi.

    Neymar, alijitengenezea nafasi nzuri karibu na lango na kuwa makini, punde tu baada ya mpira kuwavuka wote mbele ya lango, akiwemo kipa Ochoa, aliyezuia wafungaji wa Brazil, Neymar aliuwezesha mpira kufululiza na kutulia kwenye kamba.

    Mexico iliwapa matumaini mashabiki wake kwa kufanya majaribio kwa lango la Brazil ili kusawazisha matokeo.

    Vitisho vyao vilifanywa na Vela na Layun waliobadili njia na kuwaandama mabeki wa kulia na wa kushoto wa Brazil, Fagner na Filipe Luis.

    Safu ya ufungaji ya Mexico ilipigwa jeki baada ya Kocha Juan Osorio kumtoa beki Rafael Márquez na kumtambulisha Miguel Layún.

    Mbinu zote za Mexico hazikuzaa matunda kwani Brazil ilitimua ushambulizi kama njia ya kujikinga na kuwadumisha Mexico eneo lao.

    Bao moja la Brazil lilitenganisha pande hizo hadi dakika 10 za mwisho lakini kocha Tite hakusita kuzidisha nguvu za mabeki wake.

    Mchezo wa Brazil ulibadilika wakati Fernandinho aliingia nafasi ya Paulinho. Kiungo huyo wa Manchester City, aliongeza ustadi wake kutuliza mechi.

    Dakika chache baadaye, masaibu ya Mexico yaliongezeka baada ya Philippe Coutinho kumpisha Roberto Firmino.

    Nguvu mpya Firmino, alikamilisha mbio za Fernandinho na kuzamisha matumaini ya Mexico dakika mbili kabla ya muda wa kawaida wa mechi kukamilika. Ilikuwa ni mguso wake wa pili wa mpira.

    Juhudi zake zimezua mjadala za iwapo Brazil inastahili kumuanzisha mbele ya Gabriel Jesus.

    Iwapo atahamisha fomu yake nzuri ya Liverpool hadi timu ya taifa, mchango wako huenda ukawastawisha Coutinho na Willian.

    Brazil itakwaruzana na mshindi kati ya Ubelgiji na Japan katika uwanja wa Kazan Arena, Kazan, siku ya Ijumaa.