Odinga na Kenyatta: Mambo yalivyokuwa siku ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2017 tarehe 8 Agosti
Muungano wa upinzani nchini Kenya umepinga matokeo ya urais ambayo yamekuwa yakitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi IEBC.
Moja kwa moja
Wapiga kura kituo 'cha Bw Odinga'
Wapiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Olympic katika mtaa wa Kibera, Nairobi walifika mapema.
Abdinoor Aden ametutumia picha hizi za wapiga kura, baadhi wakitafuta majina yao katika orodha ya wapiga kura iliyowekwa ukutani. Baadhi wamekuwa wakitumia taa za simu zao kumulika.
Mgombea urais wa muungano wa upinzani National Super Alliance Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake katika kituo hicho baadaye leo mchana.
Wakenya waliokesha vituo vya kupigia kura
Baadhi ya Wakenya wamekesha katika vituo vya kupigia kura.
Kwa nini? Msikilize mmoja wao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Mambo muhimu kuhusu uchaguzi wa urais Kenya 2017
Uchaguzi wa mwaka huu una ushindani mkubwa kati ya Rais Kenyatta na Bw Odinga, rais huyo akipigania kuchaguliwa tena. Katika majimbo 47, uchaguzi unafanyika mara ya pili kuwachagua magavana baada ya kutekelezwa kwa mfumo wa ugatuzi mwaka 2013.
BBC imekuandalia mambo muhimu unayofaa kuyafahamu kuhusu uchaguzi huo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazo
Mwisho wa YouTube ujumbe
Waziri awahakikishia Wakenya usalama wakipiga kura
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Kenya, hasa kutokana na ushindani mkali unaoshuhudiwa kati ya wagombea urais wawili wakuu.
Wengi bado wanakumbuka ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, miaka kumi iliyopita.
Aidha, majuzi meneja wa masuala ya teknolojia wa tume ya uchaguzi IEBC Chris Musando aliuawa na watu wasiojulikana.
Kaimu waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang'i amewahakikishia Wakenya kwamba usalama umeimarishwa na hawafai kuwa na wasiwasi wakipiga na hata baada ya kupiga kura.
"Sisi wenyewe tumekomaa kisiasa kama nchi, mipango yetu ya kuandaa uchaguzi imeimarika zaidi na tume huru ya kusimamia uchaguzi imekuwa ikiimarika kila wakati. Sioni haja ya mtu yeyote kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine," Dkt Matiang'i aliambia BBC.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazo
Mwisho wa YouTube ujumbe
Familia za Kenyatta na Odinga
Chanzo cha picha, AFP/Getty
Kwa mara nyingine tena, Uhuru Kenyatta na Raila Odinga,
wanashindania uongozi wa taifa la Kenya baada ya
kukabiliana tena Machi 2013.
Rais Kenyatta ni mwana wa rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo
Kenyatta naye Bw Odinga mwana wa makamu wa rais wa kwanza Jaramogi Oginga
Odinga.
Familia hizo zilianza kwa kuwa marafiki wa kufa kuzikana wakati wa Kenya kujipatia uhuru wake. Jaramogi
alipewa fursa ya kuwa kiongozi wa kwanza wa Kenya na Waingereza lakini
akaikataa fursa hiyo na kusema Kenya haiwezi kupokea uhuru kiongozi wake Mzee
Kenyatta akiwa jela.
Jomo Kenyatta aliachiliwa na akawa waziri mkuu na mwaka mmoja baadaye baada ya Kenya kuwa jamhuri akawa rais wa kwanza wa Kenya, na Jaramogi akawa makamu wake.
Lakini uhasama ulizuka mwaka 1966 na Kenyatta akamfuta kazi
Jaramogi na kuanzia hapo uhasama wa muda mrefu kati ya jamii ya Wakikuyu
(Kenyatta) na Wajaluo (Odinga) ukaanza.
Uhuru Kenyatta na Odinga walishindana katika uchaguzi wa urais
mwaka 2013 na Bw Kenyatta akaibuka mshindi.
Wakati huu, kivumbi tena ni kati ya wawili hao.
Bw Odinga anagombea urais mara ya nne na ushindani kati ya wawili
hao ni kama umefikia kilele.
Wapiga kura waanza kufika vituoni
Ingawa vituo vya kupigia kura vitafunguliwa rasmi saa kumi na mbili, wapiga kura wameanza kujitokeza vituoni.
Katika baadhi ya vituo, watu walifika mapema mwendo wa saa tisa hizi.
Tayari vituo vingi kuna foleni.
Mwandishi wa BBC Dayo Yusuf alikutana na baadhi yao katika kituo kimoja Nairobi:
Hujambo!
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi mkuu wa Kenya. Wapiga kura 19 wanatarajiwa kufika vituoni kumchagua rais, , magavana wa kaunti, wabunge, maseneta, wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa wadi.