Habari za hivi punde, Matokeo uchaguzi wa urais kufikia sasa: Kenyatta na Odinga
Matokeo kutoka vituo vya kupigia kura 2642 kati ya jumla ya 40883 :
- Uhuru Kenyatta ana kura 385,649 (59.61%)
- Raila Odinga wa ODM 256,582 (39.66%)
Muungano wa upinzani nchini Kenya umepinga matokeo ya urais ambayo yamekuwa yakitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi IEBC.
Matokeo kutoka vituo vya kupigia kura 2642 kati ya jumla ya 40883 :
Nchini Kenya, utawasikia wanasiasa wakizungumzia upigaji kura kwa vipande sita vya suti. Wanaposema hivyo, wanamaanisha nini? Mwandishi wa BBC Salim Kikeke anakufafanulia.
Kumbuka unaweza kusikiliza matangazo maalum ya Dira ya Dunia moja kwa moja kupitia Facebook. Leo, tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Zoezi la upigaji kura limekamilika katika kituo cha Arusha.
Raia wa Kenya wanaoishi katika taifa hilo kwa sasa wanasubiri matokeo.
Nafasi ya urais pekee ndio Ilikuwa ikipigiwa kura hapa.
Shughuli hiyo pia ilifanyika mjini Dar es Salaam nchini Tanzania

Matokeo ya vituo 293 kati ya jumla ya vituo 40883 kote nchini Kenya yametangazwa. Kufikia sasa
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto wa kike akisubiri kupiga kura nchini Kenya.
Paulina Chemanang alisaidiwa kujifungua mtoto huyo na wapiga kura wengine katika shule ya upili ya West Pokot kabla ya kukimbizwa katika kituo cha afya kilichokuwa karibu.
Baadaye alirudi kupiga kura. ''Baada ya kujifungua kituoni .
Ni baraka kwangu na namshukuru Mungu, alinukuliwa akisema Bi Chemanang alimtaja mwane Chepkura''.

Shughuli ya kuhesabu kura imeanza nchini Kenya muda mchache uliopita baada ya raia kujitokeza kwa wingi na kupiga kura.
Baadhi ya vituo vilivyofunguliwa mapema vilikamilisha shughuli ya kupiga kura na sasa vinahesabu kura hizo.
Hatahivyo baadhi ya vituo vilivyofunguliwa kuchelewa vinaendelea kupiga kura huku tume ya IEBC ikisema kuwa vitangozewa muda kuendelea na zoezi hilo.
Mapema alfajiri milolongo mirefu ya kupiga kura ilishuhudiwa katika maeneo nchini humo.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mwendo wa saa kumi na mbili alfajari.
Wengi wa wapiga kura walipiga kambi katika vituo hivyo usiku kucha wakisubiri kutekeleza haki yao ya uchaguzi.
Baadhi ya vituo vilishuhudia mvua kubwa na hivyobasi kuathiri operesheni za shughuli hiyo .

Chanzo cha picha, AFP
Raia wanapiga kura katika uchaguzi mkuu nchini Kenya huku kukiwa na hofu kwamba matokeo yanaweza kuzua ghasia za kikabilia.
Rais Uhuru Kenyatta ametaka kuwepo kwa umoja, akisema kuwa atakubali matokeo na kuwataka wapinzani wake kukubali.
Milolongo mirefu imeshuhudiwa mapema alfajiri huku mikanyagano michache ikiripotiwa.
Idhaa moja ya redio nchini humo imetangaza kuwa mtu mmoja amefariki katika ghasia kusini mwa mji wa Kilifi.
Ushindani ni kati ya rais Uhuru Kenyatta dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu Raila Odinga na unaonekana kuwa wa karibu sana.
Bwana Kenyatta ambaye ana umri wa miaka 55 ni mwana wa rais wa kwanza wa taifa hilo anayetetea kiti chake kwa muhula mwengine na wa mwisho.
Wagombea wengine sita pia wanawania wadhfa huo.

Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imesema itawashtaki maafisa wake waliopatikana katika maeneo tofauti nchini wakikiuka sheria za uchaguzi .Mjini Mombasa afisa mmoja wa tume hiyo alikamatwa kwa kutoa makaratasi mawili mawili kwa wapiga kura huku eneo la Murang'a baadhi ya maafisa hao wakikamatwa kwa kufanya njama ya kubadilisha majina ya makarani wa kusimamia shughuli hio.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kuchelewa , huku operesheni zikiathiriwa na mvua kali IEBC imetangaza kuwa muda wa kupigia kura utaongezwa katika maeneo hayo. Lakini matatzio mengine yalizuka .Kituo kimoja cha kupigia kura kilikuwa katika eneo lisilo na mtandao wa mawasiliano ya simu ,hatua ambayo itawalazimu maafisa wa IEBC kusafiri hadi maeneo yenye mtandao wa simu ili kutuma matokeo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amewania urais kwa mara ya 3 na kupoteza kila mara. Rais Uhuru Kenyatta alimshinda katika uchaguzi uliopita wa 2013 , hatahivyo upinzani wao wa kisiasa ulianza wakati wa baba zao miaka ya 60. Rais Kenyata na naibu wake William Ruto walishtakiwa na mahakama ya ICC kwa majukumu yao katika ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007 yapata miaka 10 ilioita. Hatahivyo kesi hiyo ilishindwa kutokana na ukosefu wa ushahidi baada ya mashahidi muhimu kufariki na hata kupotea

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati amesema kuwa ni asilimia 40 ya wapiga kura pekee iliotambulika na vifaa vya kielektroniki ambavyo ni 25,000

Mkuu wa kundi la waangalizi wa uchaguzi kutoka bara Ulaya Marietje Schaake amesema kuwa vituo vya kupiga kura vilikuwa vikiendelea na shughuli yao ya kawaida na raia wengi walijitokeza kupiga kura

Raila Odinga aliwaambia wafuasi wake kila moja ni lazima mawe na wino wa kuonyesha kuwa amepiga kura, "tujitokeze kwa wingi tupige kura" Raila aliwaambia wafuasi wake. Baada ya kumaliza kupiga kura saa za jioni tukutane bustani ya uhuru park tusubiri matokeo.


Mwandishi wetu Abdinoor Aden ametutumia picha zaidi za hali ilivyokuwa mgombea wa muungano wa upinzani Nasa alipokuwa anapiga kura yake Kibra, Nairobi.
Tazama:




Wakati wananchi wakipiga kura, mwanamume huyu amekuwa akiwahimiza kudumisha amani wakati wa uchaguzi wenyewe na baadaye.
Mwandishi wetu Abdinoor Aden alikutana naye karibu na kituo cha Olympic mtaa wa Kibera, Nairobi.
Kwenye nguo zake, kuna ujumbe wa 'Zuia Noma', lugha ya mtaani ya kuwataka watu wazuie fujo na balaa.



Chanzo cha picha, Uhuru Kenyatta / Facebook
Rais Uhuru kenyatta amepiga kura katika kituo cha Mutomo katika eneo lake la nyumbani la Gatundu, eneo la kati nchini Kenya.
Ametoa wito kwa viongozi na wapinzani wake kukubali uamuzi wa wananchi.
Amesema mwenyewe yuko tayari kukubali kushindwa iwapo atashindwa na amesema anatarajia wenzake wafanye vivyo hivyo.
Kenyatta ametoa wito kwa Wakenya wasikubali kutenganishwa na uchaguzi.
Naibu Rais William Ruto amepiga kura yake katika kituo cha shule ya msingi ya Kosachei katika kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya.

Mgombea wa Urais kupitia chama cha ODM na Mrengo wa NASA Raila Odinga amepiga kupiga kura katika shule ya msingi ya Kibra, mjini Nairobi.
Mwandishi wa BBC Abdinoor Aden amekuwa katika kituo cha kupigia kura kiongozi huyo alipopiga kura yake akiandamana na mkewe Ida. Unaweza kutazama video iliyopigwa moja kwa moja hapa:

