Odinga na Kenyatta: Mambo yalivyokuwa siku ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2017 tarehe 8 Agosti

Muungano wa upinzani nchini Kenya umepinga matokeo ya urais ambayo yamekuwa yakitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi IEBC.

Moja kwa moja

  1. Hata wakongwe hawajaachwa nyuma kuhakisha kuwa wametekeza haki yao ya kupiga kura

    Hata wakongwe hawajaachwa nyuma
  2. Mji wa Nakuru wabaki 'mahame'

    Maeneo mengi ya miji yamebaki bila watu, wengi wakielekea katika vituo vya kupigia kura kupiga kura. Mwandishi wetu Idris Situma amepiga picha hizi mjini Nakuru.

    Mitaa ikiwa bila watu na biashara nyingi kufungwa mjini Nakuru
    Mitaa ikiwa bila watu na biashara nyingi kufungwa mjini Nakuru
    Mitaa ikiwa bila watu na biashara nyingi kufungwa mjini Nakuru
    Mitaa ikiwa bila watu na biashara nyingi kufungwa mjini Nakuru
  3. John Kerry, mmoja wa waangalizi wa uchaguzi awasili kituo cha kupigia kura cha Moi Avenue, Nairobi

    John Kerry awasili kituo cha kupigia Kura
  4. Wapiga kura wakipata chai ya asubuhi wanaposubiri kupiga kura

    Wapiga kura  wakipata chai
    Wapiga kura  wakipata chai
  5. IEBC: Tunaangazia changamoto zinazoshuhudiwa

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC amekuwa akiwahutubia wanahabari ukumbi wa Bomas.

    Amesema anafahamu kwamba baadhi ya Wakenya walirauka hata kabla ya vituo kufunguliwa.

    Amewahimiza wapiga kura ambao hawajafika vituoni kufanya hivyo.

    Bw Chebukati amesema anafahamu kwamba katika baadhi ya vituo kumeshuhudiwa changamoto na wanaangazia kuzitatua.

    Katika baadhi ya maeneo, amesema mvua kubwa ilitatiza uchukuzi na wamelazimika kutumia helikopta.

    "Katika vituo vilivyochelewa kufunguliwa, tutaongeza muda wa kufunga vituo, sawia na muda uliocheleweshwa."

  6. Mtindo wa mavazi katika kupiga kura

    Wapiga kura wamekuwa wakijitokeza kwa njia mbalimbali na wakiwa wamevalia mavazi mbalimbali. Lakini utafanyaje kuonesha uzalendo? Pengine uvalie kama watatu hawa katika kituo cha Mutomo, Gatundu ambapo Rais Kenyatta anatarajiwa kupiga kura baadaye.

    Uzalendo
  7. Upigaji kura kituo cha William Ruto

    Upigaji kura unaendelea katika kituo cha Kosachei katika kaunti ya Uasin Gishu ambapo Naibu Rais William Ruto anatarajiwa kupiga kura yake baadaye leo.

    Kosachei
    Kosachei
  8. IEBC: Tunafahamu kuna vituo vilichelewa

    Tume huru ya uchaguzi nchini Kenya imesema inafahamu kwamba kuna baadhi ya vituo vya kupigia kura ambavyo vilifunguliwa kwa kuchelewa.

    Tume hiyo imeandika kwenye Twitter kwamba maafisa wake wanashughulikia hilo na tahakikisha hakuna mpigaji kura anayetatizika.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  9. Foleni katika baadhi ya vituo

    Katika baadhi ya vituo, kuna foleni ndefu. Mfano ni katika kituo hiki cha Kipsigis County Council mjini Kericho kama alivyoshuhudia mwandishi wa BBC Rob Wilson.

    Je, wewe ni Mkenya, hali iko vipi ulipo?

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  10. Yasemavyo magazeti ya Kenya kuhusu uchaguzi

    Nation
    Standard
    Taifa
    Business Daily
  11. Wakenya wapiga kura nchini Tanzania

    Raia wa Kenya waishio Tanzania wamekuwa wakipiga kura nchini Tanzania katika miji ya Dar es Salaam na Arusha.

    Mwandishi wa BBC Halima Nyanza yupo katika kituo cha kupigia kura mjini Arusha ambapo ameshuhudia upigaji kura ukiendelea.

    Kura Arusha
    Arusha
    Watawa kutoka Kenya wakijiandaa kupiga kura mjini Arusha
    Maelezo ya picha, Watawa kutoka Kenya wakijiandaa kupiga kura mjini Arusha
  12. Hitilafu za kimitambo kituo cha Kibra

    Mwandishi wa BBC Abdinoor Aden anasema mitambo ya kuwatambua wapiga kura katika kituo cha shule ya Olympic, Kibra imeanza kukubwa na hitilafu.

    Shughuli ya upigaji kura imesimama kwa muda maafisa wa tume ya uchaguzi wakijaribu kutatua tatizo hilo.

    Afisa msimamizi wa ucahguzi kituo hicho Aggrey Mulera amesema wanajaribu kutafuta suluhu.

    Mitambo
    Wapiga kura
  13. Hakuna kuachwa nyuma

    Watu wa jamii ya Kalasinga hawajaachwa nyuma katika mji wa Kisumu, magharibi mwa Kenya. Mwandishi wetu Odeo Sirari amekutana na wawili hawa kwenye foleni kituo cha Ukumbi wa Aga Khan.

    Kalasinga
  14. Kukanganywa na rangi Kisumu

    Mpiga kura huyu anasema hakuweza kutofautisha rangi za karatasi za kupiga kura, rangi ya karatasi za wawakilishi wa wadi na wawakilishi wa wanawake.

    Rangi ya karatasi ya kupigia kura inafanana na rangi ya vifuniko vya masanduku ya kutumbukiza kura.

    Rangi ya karatasi ya urais ni nyeupe na vivyo hivyo, masanduku ya kura za urais yana vifuniko vyeupe.

    Ugavana rangi ni ya samawati. Kura ya seneta ni ya manjano, mbunge ni kijani kibichi na mwakilishi wa wanawake ni ya kizambarau nazo za mwakilishi wa kaunti biji.

    rangi
  15. Upigaji kura wachelewa kuanza Garissa

    Upigaji kura katika kituo cha kupigia kura cha Maktaba ya Garissa umechelewa kuanza. Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay anasema upigaji kura umeanza dakika chache zilizopita.

    Garissa
  16. Wapiga kura wa kwanza Kisumu

    Mwandishi wetu Odeo Sirari yupo katika kituo cha Aga Khan mjini Kisumu na amewapiga piga wapiga kura hawa ambao walikuwa miongoni mwa waliopiga kwanza kituoni humo.

    Mpiga kura 1
    Mpiga 2
  17. Wapiga kura wa kwanza Kwale

    Upigaji kura umeanza katika kituo cha Wabungo, Kwale pwani ya Kenya na baadhi ya watu washamaliza kupiga kura.

    Pichani ni mmoja wa waliopiga kura kwanza.

    Upigaji kura
  18. Garissa raia kupiga kura maktabani

    Shughuli ya upigaji kura imeanza katika kaunti ya Garissa, mashariki mwa Kenya. Usalama umeimarishwa.

    Pichani ni maafisa wa Tume ya Uchaguzi wakijiandaa kwa upigaji kura.

    Garissa
  19. Hali ilivyo Mwabungo eneo la Kwale pwani ya Kenya

    Hivi ndivyo hali ilivyo kituo cha kupigia kura cha Mwabungo kaunti ya Kwale. Hapa, watu wa jamii ya Makonde watapiga kura mara ya kwanza baada ya kutambuliwa kuwa raia wa Kenya.

    Mwabungo
    Mwabungo
  20. Habari za hivi punde, Vituo vya kura vyafunguliwa

    Vituo vya kupigia kura nchini Kenya vimefunguliwa rasmi.