Uchaguzi mkuu wa Tanzania 2025: Mtandao waendelea kuminywa kwa siku ya pili mfululizo

Chanzo cha picha, Getty Images
Tanzania inaendelea kushuhudia siku ya pili ya kukatwa kwa mtandao hatua ambayo imefanya mawasiliano kuwa changamoto.
Hapo jana siku ya uchaguzi, shirika la kimataifa la uchunguzi wa mtandao wa Netblocks, lilisema kuwa limegundua kufinywa kwa mtandao kote nchini humo.
"Imethibitishwa: Takwimu za mtandao wa moja kwa moja zinaonyesha usumbufu wa kitaifa kwa kuunganishwa kwa mtandao nchini Tanzania Siku ya Uchaguzi," Netblocks aliandika katika machapisho kwenye vyombo vya habari vya kijamii.
Tatizo la ukosefu wa mtandao limeathiri pia wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao kwa njia hiyo.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza Tanzania kukutana na tukio kama hili ikikumbukwa pia uchaguzi wa 2020 mtandao wa X ulifungwa.
Pia unaweza kusoma:



