Boresheni hali ya wafanyakazi :Amnesty

Maandalizi ya kombe la Dunia
Maelezo ya picha, Maandalizi ya kombe la Dunia
Iliyochapishwa

Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnesty International ,linasema Qatar inalazimika kuboresha hali ya wafanyakazi wahamiaji wakati huu nchi hiyo inapoendelea na maandalizi ya kombe la dunia la mwaka 2022.

Wafanyikazi wa kigeni ndio wanaotumika kujenga viwanja Qatar

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Wafanyikazi wa kigeni ndio wanaotumika kujenga viwanja Qatar

Amnesty wanasema Qatar imepiga hatua kidogo sana kutekeleza ahadi nyingi walizozitoa mwaka jana, kwani wafanyakazi bado wanahitaji ruhusa kutoka kwa waajiri wao ,kubadili ajira au kuondoka nchini humo,mabadiliko ya malipo kwa wafanyakazi yanafanyika taratibu mno wakati ni jambo la muhimu mno.

Maelfu ya wafanyikazi wanasemekana kuishi katika mazingira duni

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maelfu ya wafanyikazi wanasemekana kuishi katika mazingira duni

Hata hivyo Serikali ya Qatar inasema mabadiliko makubwa yanakuja ifikapo mwishoni mwa mwaka huu,japo kuwa Amnesty inaitaka FIFA , kuishinikiza Qatar kuongeza kasi katika kuleta mabadiliko.