Wimbi la joto Ulaya katika picha

Iliyochapishwa

Wimbi la joto linaendelea kote barani Ulaya, huku halijoto katika kisiwa cha Sardinia nchini Italia ikitarajiwa kufikia kiwango cha juu cha 46C (114.8F) siku ya Jumanne.

Kumekuwa na moto wa nyika kwenye kisiwa cha Uhispania cha La Palma na Ugiriki bara.

Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani linasema hali mbaya ya hewa inahitaji kuangaziwa kwa makini.

Huko Roma, watalii na wakazi walibarizi mbele ya Ukumbi maarufu wa Kirumi (hapo juu) na kwenye chemchemi za umma ( hapo chini).

Bologna, nchini Italia pia, ilishuhudia matukio kama hayo - ikiwa ni pamoja na mtu mmoja akiendesha baiskeli katikati ya jiji akiwa na feni.

Mtu akijikinga na jua ufukweni kwenye ukingo wa ziwa Ada huko Belgrade, Serbia.

Mamlaka zinakabiliana na moto wa nyika katika eneo la Magoula, magharibi mwa Athens, Ugiriki.

Mioto ya nyikani pia imeteketeza eneo la La Palma, Uhispania.

Picha zote zina haki miliki.