Emiliano Sala: Rubani alimwambia rafiki yake ndege ilioangamia ilikuwa 'haiaminiki'

Iliyochapishwa

Rubani wa ndege ya Emiliano Sala aliwaambia marafiki zake kwamba ndege hiyo ilikuwa "haiaminiki" kabla ya ndege hiyo kumuua mwanasoka huyo wa Argentina, inaweza kubainika.

David Ibbotson anasikika katika sauti ya kipekee iliyopatikana na BBC akisema "nitakuwa nimevaa jaketi langu la usalama" katika safari ya kutoka Ufaransa kuelekea Wales.

Alimwambia rafiki yake kwamba alisikia mlio wa "bang" katika safari ya awali. Ndege hiyo ilianguka katika mkondo wa bahari wa English Channel mwaka 2019.

Sauti mpya pia ilifichua kanda za video za wawili hao walipokuwa hai.

Sala alikuwa amenunuliwa na klabu ya ligi ya premia Cardiff City kwa dau la £15m, kutoka klabu ya Ufaransa ya Nantes wakati ndege hiyo ilipoanguka katika mkondo huo wa bahari.

Matatizo ya kiufundi

Aliendeshwa na bwana Ibbotson - rubani wa muda ambaye alikuwa hana leseni ya kuwabeba abiria waliokuwa wakilipa - kurudi magharibi mwa Ufaransa akisema kwaheri na kukusanya mizogo yao.

Alisafiri kutoka Nantes siku ya Jumamosi , tarehe 19 Januari na kupanga kurudi siku ya Jumatatu - siku ya ajali hiyo.

Sauti ya simu kutoka kwa rubani mwengine ilipatikana na BBC , ikifichua kwa mara ya kwanza matatizo ya kiufundi ambayo bwana Ibbotson alipata katika safari yake ya kuelekea Ufaransa.

Ndani yake , alisikika akisema kwamba alisikia mshindo mkubwa wa " bang" wakati wa safari hiyo na kulalamika kwamba alikuwa akihisi ukungu mchache ndani ya ndege hiyo ya miaka 35 ya Malibu.

'Nilikuwa katikati ya mkondo wa bahari na mara nikasikia 'Bang', bwana Ibbotson alimwambia Kevin Jones kuhusu safari yake ya kuelekea Nantes.

Nasafiri na mara nasikia 'boom'. Nikafikiria nini kimetokea? Nilianza kuchunguza na kuangalia masharti iwapo nimetimiza, kila kitu kilikuwa katika hali nzuri na ndege ilikuwa bado inapaa''

Aliongezea: "Hiyo Malibu, mara kwa mara inakuwa na kama ukungu kila baada ya muda fulani. Unaweza kuhisi, chini sana, chini sana kwenye kiwango cha hewa."

Bw Ibbotson, 59, alisema pia aligundua kuwa kikanyagio cha breki ya kushoto ya Piper Malibu hakikuwa kikifanya kazi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Nantes Atlantique. "Ndege hii lazima irudi kwenye hanger," alimwambia rafiki yake.

Mazungumzo hayo yalirekodiwa kimakosa na tangu wakati huo yamepatikana na podikasti ya BBC ya Uhamisho: Hadithi ya Emiliano Sala.

Kabla ya safari ya ndege kurejea Cardiff, Bw Ibbotson aliongeza: "Kwa kawaida ningekuwa na koti langu la usalama katikati ya viti lakini kesho nitalivaa."

Watu wawili pekee kwenye ndege hiyo walikuwa Emiliano Sala na Bw Ibbotson, kutoka Crowle, Kaskazini mwa Lincolnshire, ambao miili yao haijawahi kupatikana.

'Jamani, ninaogopa'

Mwanasoka huyo pia alikuwa ameelezea hofu yake kuhusu ndege hiyo katika ujumbe wa sauti uliotumwa kwa marafiki zake wa karibu wakati ndege hiyo ilipokuwa ikipakia kwenye barabara ya kurukia ya uwanja wa ndege wa Nantes Atlantique.

Mchezaji huyo aliwaambia, "jamani, ninaogopa" na kwamba ndege aliyokuwa "inaonekana kama inaanguka". "Sijui ikiwa kuna mtu atanitafuta kwa sababu hatanipata," Bw Sala aliwaambia marafiki zake kuhusu ajali inayoweza kutokea.

Cardiff City FC walikuwa wamempa mchezaji wao mpya ndege ya kibiashara, kusafiri kupitia Paris, lakini alitaka muda zaidi wa kuwaaga marafiki na wachezaji wenzake huko Nantes kabla ya kurejea Wales kwa kikao chake cha kwanza cha mazoezi na klabu yake mpya.

Kwa hivyo Willie McKay, mtu aliyesaidia udalali, alikodisha ndege ya kibinafsi - moja kwa moja kati ya Nantes na Cardiff - kupitia rubani mwingine, David Henderson.

Kwa sababu Henderson hakuweza kutekeleza ombi hilo, alimpigia simu Bw Ibbotson.

Muajentina huyo hakujua kuwa Bw Ibbotson hakuwa na sifa ya kusafiri usiku huo wa maafa. Mfungaji huyo wa gesi alikuwa rubani asiye na ujuzi na hakuwa na leseni ya kubeba abiria wanaolipa au kuruka kihalali nyakati za giza.

Takriban saa moja baada ya kupaa kutoka kwenye barabara ya tatu ya uwanja wa ndege, huko Nantes, Piper Malibu N264DB ilipoteza mawasiliano ya rada kwenye mkondo wa bahari wa English Channel, na uokoaji wa anga na baharini ukaanzish

Ndege hiyo ilikuwa inarukaurefu wa futi 5,000 lakini rubani alishindwa kuidhibiti ilipokuwa ikishuka ili kuepuka mawingu na kutua kwenye mkondo wa bahari wa English Channel , kwa kasi inayokadiriwa kufikia 270mph (434kph).

Wachunguzi wa ajali za anga waligundua kuwa mchezaji huyo wa soka "angekuwa amepoteza fahamu" kutokana na sumu ya kaboni monoksidi na kwamba huenda rubani angeathirika pia.

Mwili wa mchezaji huyo ulipatikana kutoka kwenye mabaki hayo ulipogunduliwa umbali wa mita 68 (futi 223) kwenye sakafu ya mkondo wa bahari wa English Channel, wiki mbili baada ya ajali hiyo. Ndege N264DB iliachwa chini ya bahari.

Henderson ambaye ndiye aliyepanga safari ya ndege hiyo, alihukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kuhatarisha usalama wa ndege bila kujali jinsi alivyopanga safari na kutumia ndege ya kibiashara bila kibali.