Uchaguzi wa kenya 2022: Picha za watu na matukio muhimu siku nzima ya upigaji kura Kenya

ggg
Maelezo ya picha, Sarah Mwihaki mwenye umri wa miaka 96
Iliyochapishwa

Raia wa Kenya leo Jumanne wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura nchini humo wakiwa na shauku ya kuchagua rais atakayeiongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo pamoja na viongozi wengine wakiwemo Maseneta, gavana, wabunge na madiwani.

Kura hiyo inafuatia kampeni kali iliyotawaliwa na mijadala kuhusu gharama za maisha, ukosefu wa ajira na ufisadi.Wanaogombea urais ni aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, George Wajackoyah, David Mwaure na Naibu Rais wa sasa William Ruto.

Dosari chache zimejitokeza ikiwemo ucheleweshaji vifaa katika baadhi ya maeneo pamoja na vifaa vya kielektroniki vinavyokagua alama za vidole (vinavyojulikana kama vifaa vya Kiems) kuripotiwa kutofanya kazi vizuri katika maeneo tofauti.

Lakini kwa ujumla mchakato unaonekana kwenda vizuri mpaka sasa. Hizi ni picha za matukio mbalimbali yaliyojiri katika siku hii ya uchaguzi wa Kenya

ddd
Maelezo ya picha, Katika eneo laKibera mapema Alfajiri watu walianza kujitokeza katika vituo vya kupigia kura

Watu walidamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kuwahi foleni katika vituo vya kupigia kura

ddd
Maelezo ya picha, Selah Zainabu, amekuwa kwenye foleni tangu saa kumi alfajiri. Yuko na mtoto wake wa miaka 2 kwa sababu hana mtu nyumbani wa kumuacha mtoto.

Wengine walithubutu hata kulala vituoni ili kuwahi nafasi asubuhi

ddd
Maelezo ya picha, Margaret Mwangi, 59, mchuuzi wa matunda aliamua kutokwenda nyumbani kulala. Alipiga kambi hapa akisubiri kupiga kura alikuwa wa pili kwenye foleni na baada ya kupiga kura alienda nyumbani kufuatilia habari kwenye televisheni.

Changamoto chache zilijitokeza kama hii ya Rahab Nduta ambaye yeye hakukuta jina lake katika kituo chake cha kupigia kura na kuambiwa kuwa jina lake lipo kituo kingine

ggg
Maelezo ya picha, Rahab Nduta, 85, alifika kwake kituo cha kupigia kura na kuambiwa maelezo ya kura yake yapo kituo kingine cha kupigia kura na alisema "Lakini sijawahi kubadilisha kituo changu cha kupigia kura, sasa nifanyeje?"

Wazee, wenye ulemavu na hata wajawazito hawakubaki nyuma na walipata ushirikiano mzuri.

ggg
ggg
Maelezo ya picha, Sarah Mwihaki, 96, akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Mutomo, Gatundu Kusini, kaunti ya Kiambu.
bbb
Maelezo ya picha, Mwalimu Joy Njue. Anasema anapiga kura kwa ajili ya mustakabali mwema wa mtoto wake ambaye hajazaliwa na wanafunzi anaowafundisha.
fff

Chanzo cha picha, BBC

Maelezo ya picha, Wapiga kura katika eneo la Nyali, Mombasa walijitokeza kupiga kura kwa wingi licha ya wao kukosa kumpigia kura gavana wanaompenda
ggg
Maelezo ya picha, Peter Mungai anasema upigaji kura ulikuwa rahisi kwake. Vifaa vya KIEMs havikusajili alama ya vidole kwenye jaribio la kwanza lakini ilifanya kazi katika jaribio lake la pili. Anasisitiza wale ambao hawakupiga kura wasilalamike baadaye kwa sababu hawakushiriki na kiongozi ambaye hawakumtaka anaweza kuchaguliwa kwa sababu ya kutoshiriki kwao.
ggg
Maelezo ya picha, Kijana huyo alifika katika kituo cha kupigia kura cha Kisumu ya Kati akiwa na taulo na mswaki tayari kwa ajili ya kupiga kura