Uchaguzi Kenya 2022: Watawala wa kurithi dhidi ya Watafutaji

    • Author, Evelyne Musambi
    • Nafasi, BBC News, Nairobi
  • Iliyochapishwa

Katika hatua inayofanana ya Trump ya kumuunga mkono Clinton katika uchaguzi wa Marekani, Rais wa Kenya anayeondoka  Uhuru Kenyatta anataka kumkabidhi taji la siasa hasimu wake aliyegeuka kuwa rafiki Raila Odinga  - lakini anamshuhudia naibu wake William Ruto akijaribu kunyakua taji hilo katika uchaguzi wa tarehe 9 Agosti. 

Imepelekea kuwepo kwa mchezo wa kuigiza ambapo Bw Ruto anajitaja kama  "hustler" au mtu aliyetafuta, anayepambana  na kile anachokiona kama  jaribio la kuendelezwa kwa ungozi wa mkubwa zaidi wa kuruthi wa-  Familia ya Kenyatta na ya Odinga -ili uendelee kubakia mamlakani.   

Akijaribu kupata huruma kutokakwa Wakenya, Ruto, amekuwa akifanya maombi, kuangua kilio, na kutoa madai makali kwamba Rais Kenyatta anamtisha. 

 "Ili mradi usiue watoto wangu nitakiukabili lakini wacha tuheshimiane," Bw   Ruto alisema, katika moja ya kampeni zake za mwisho huku umati ukimshangilia.

Akipinga madai yake, Bw Kenyatta alisema: "Umenitukana kwa karibu miaka mitatu. Kuna mtu aliyekugusa ?"Malumbano yao yalionyesha  jinsi hasira ilivyotawala kampeni za uchaguzi, huku Bw kenyatta akijitokeza kumuunga mkono Bw  Odinga kama mrithi wake.

"Rais amekwenda kinyume na mwelekeo wa lengo la Ruto, kulumbana naye, na kusahau kuhusu mshindani wake ," mchambuzi wa kisiasa wa Kenya  Profesa Masibo Lumala ameiambia  BBC.

 "Rais ameweza kuonyesha wazi upande wa naibu wake ambao unaonyesha hasira yake, jambo ambalo sio kitu kizuri ," aliongeza.

Naibu Rais William Ruto alikosana na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa muhula wa pili. Mchambuzi mwingine Profesa Macharia Munene alisema kuwa malumbano haya makali yalimfanya Odinga'' kuonekana kama mtu mwenye umakini zaidi" wakati wa kampeni, ingawa alipata mapigo kutoka kwa Bw Ruto, akihoji madai yake ya kuwa ''hustler'' akimtaja kuwa "mwanaume wa ardhi nyingi" - akimaanisha utata wa muda mrefu kuhusu jinsi naibu rais alivyokuwa mmiliki mkubwa wa ardhi nchini Kenya. Alikana kunyakua ardhi kinyume cha sheria.

Mchambuzi mwingine Profesa Macharia Munene alisema kuwa malumbano haya makali yalimfanya Odinga'' kuonekana kama mtu mwenye umakini zaidi" wakati wa kampeni, ingawa alipata mapigo kutoka kwa Bw Ruto, akihoji madai yake ya kuwa ''hustler'' akimtaja kuwa "mwanaume wa ardhi nyingi" - akimaanisha utata wa muda mrefu kuhusu jinsi naibu rais alivyokuwa mmiliki mkubwa wa ardhi nchini Kenya. Alikana kunyakua ardhi kinyume cha sheria.

Hatua ya Rais kumuunga mkono Bw Odinga kutaka kukumbukwa kwa kuunganisha familia mbili ambazo ziliungana kupigana na utawala wa mkoloni Muingereza - lakini baadaye zikakosana mwaka 1966, miaka mitatu baada ya uhuru, na kuendelea kupambana hadi kufikia muhula wake wa pili na wa mwisho.

Ilimaanisha kuwa Bw Ruto, ambaye aliunde naye Muungano katika uchaguzi wa mwaka 2013 ukabiliana na mashitaka katika Mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) juu ya ghasia za mauaji zilizoikumba Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

"Kile kilichokuwa kimewaunganisha kilitoweka ," Profesa Munene alisema, akiongeza kuwa: "Sasa Ruto anataka kuchaguliwa na Uhuru anataka kukumbukwa kwa aliyoyafanya sasa nia maslahi yao yamegongana ."

Bw Kenyatta alifanya mageuzi ya kushirikiana na Bw Odinga baada ya mzozo wa uchaguzi wa mwaka 2017. Akikataa matokeo, Bw Odinga alikuwa ametoa wito wa kusia kampuni kadhaa, ikiwemo ile inayohusiana na familia ya Kenyatta, na kujitangaza kama "rais wa watu" katika mkutano mkubwa katika mji mkuu Nairobi.

"Uhuru alilazimika kumpokea raila Odinga kwasbabu alikuwa na uwezo wa kusababisha matatizo na kuvuruga kazi yake ," Profesa Munene alisema, na kuongeza kuwa Odinga mwenye umri wa miaka 77 mwanasiasa mkongwe alikubali wito wa Bw Kenyatta kwasababu uliongeza uwezekano wa kuwa rais baada ya kushindwa jaribio hilo kwa mara ya nne.

"Bw Odinga anaonekana kuwa anataka sana kuwa rais kwasababu ya umri wake, na hii inaonekana kuwa fursa yake ya mwisho ," anasema profesa Munene.

Familia za Kenyatta na Odinga ni matajiri wa kupindukia. Thamani ya utajiri wao haijulikani wazi, lakini umma ulidokezewa kuhusu utajiri wa familia ya Kenyatta wakati nyaraka za Pandora zilizowahusisha na uwekezaji wa kampuni ya kigeni , ikiwa ni pamoja na hisa na hawala za thamani yad ola milioni 30 (Pauni milioni 22 )

Bw Ruto pia ni tajiri, lakini amekuwa akijionyesha kama mtu ambaye - wakati mmoja aliuza kuku na karanga kando ya barabara - anayefahamu maisha ya taabu wanayopitia masikini, na mtu atayayejali maslahi yao iwapo atachaguliwa.

Raila Odinga amemchagua Waziri wa zamani wa sheria Martha Karua kama mgombea mwenza.

Familia za Kenyatta na Odinga ni matajiri wa kupindukia. Thamani ya utajiri wao haijulikani wazi, lakini umma ulidokezewa kuhusu utajiri wa familia ya Kenyatta wakati nyaraka za Pandora zilizowahusisha na uwekezaji wa kampuni ya kigeni , ikiwa ni pamoja na hisa na hawala za thamani ya dola milioni 30 (Pauni milioni 22 ) .

Bw Ruto pia ni tajiri, lakini amekuwa akijionyesha kama mtu ambaye - wakati mmoja aliuza kuku na karanga kando ya barabara - anayefahamu maisha ya taabu wanayopitia masikini, na atayajali maslahi yao iwapo atachaguliwa.

Huku wanawake wakiwa ni hadi karibu nusu ya idadi ya wapigakura waliojisajiri, Bw Odinga, tofauti na Ruto, amemchagua mgombea mwenza mwanamke, Waziri wa zamani wa sheria Martha Karua.

Profesa Lumala alimuelezea kama mtu tofauti miongoni mwa kampeni ya inayotawaliwa na wanaume, na anasema aliwapatia Wakenya wakati wao wa "Kamala Harris" katika kampeni.

"Tuliweza kuona umama [ndani yake]. Alitunza heshima yake n ahata wakati wa yalipokuwepo malumbano makali alipima lugha yake ," aliongeza, ingawa yeye pia alimshambulia Ruto katika siku zake za mwisho za kampeni akisema anapaswa "kuacha kuwa Naibu wa Yesu" kwa kulia katika mikutano ya maombi.

Pia unawezakusoma: