Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Fahamu hasara ya ililopata jeshi la Urusi tangu uvamizi wake ulipoanza
BBC inafahamu majina ya wanajeshi 3,052 wa Urusi waliouawa katika vita nchini Ukraine. Ingawa Wizara ya Ulinzi ya Urusi haijatoa taarifa mpya za waliofariki tangu mwisho wa Machi, askari, maafisa na wale ambao wameanza rasmi kuitwa "wanaojitolea" huzikwa kila siku nchini humo. Mbali na wote waliofariki walioripotiwa na mamlaka za mitaa - lakini makaburi mengi yana ushahidi mpya wa hasara iliyopata jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Je, makaburi na mahitaji yanatuambia nini?
Katika uchanganuzi wao wa hasara, Idhaa ya BBC ya Urusi na timu ya watu wa kujitolea hutegemea ripoti kutoka kwa wakuu wa miji ya Urusi na machapisho kutoka kwa vyombo vya habari vya ndani - katika kila kesi, angalau jina na ubini wa askari aliyefariki hujulikana. Kwa wakai huu, iliwezekana kudhibitisha habari kuhusu askari na maafisa waliokufa 3052.
Hesabu hii haiwezi kuwa sahihi, kwa kuwa vyombo vya habari na mamlaka ya kikanda hutaja zaidi ya waliofariki, hata kama "miili 200" tayari imewasilishwa katika miji na miili ya marehemu imezikwa. Wazo la ni wangapi waliokufa hawakujumuishwa kwenye takwimu hutolewa na taarifa kutoka makaburi ya mkoa.
Katika baadhi ya miji, vichochoro vyote vimetengwa kwa ajili ya mazishi ya waliouawa nchini Ukraine. BBC ilifahamishwa kuhusu hali hiyo kwenye makaburi ya huko Stavropol, Kazan, Krasnodar, Yekaterinburg, Novosibirsk, Balashikha, karibu na Ulyanovsk na katika mkoa wa Kaliningrad.
Mwili wa kila askari aliyefariki baada ya Februari 24, 2022 ulipatikana katika kila kaburi. Katika eneo la wazi, majina ya wote amabo hawajazikwa yaliwekwa. Sio ngumu kuelewa kuwa makaburi ya wanajeshi wako mbele yetu: umri wa waliofariki ni kutoka miaka 18 hadi 45, kuna picha za watu waliovaa sare ya jeshi kwenye msalaba na taji za maua kutoka Wizara ya Ulinzi juu ya kaburi.
Baada ya kuanza kwa vita huko Ukraine, makaburi mapya ya kijeshi 42 yalionekana kwenye makaburi ya Arkhangelsk karibu na Ulyanovsk. Kati ya hao, majina 21 ya waliofariki hayakutajwa hadharani na hata kutajwa katika mitandao ya kijamii.
Katika makaburi ya "Kurgan" huko Kazan, majina ambayo hayakujulikana hapo awali ni 30%. Katika makaburi ya Mikhailovsky karibu na Stavropol pia karibu 30%. Kwenye barabara ya kijeshi ya makaburi ya Kopansky karibu na Krasnodar ni yote 100%.
Mapema Aprili, video ya tukio la kuomboleza ilichapishwa kwenye vyombo vya habari, ambapo picha 55 za askari waliopoteza maisha wa Kikosi cha ulinzi cha 247 cha mashambulizi ya anga walionyeshwa.
Kati ya hao, ni majina 29 tu ndiyo yalitajwa hadharani. Kama matokeo, waandishi wa habari wa Mediazona (wanaotambuliwa na mamlaka ya Kirusi kama "wakala wa kigeni"), ambao pia wanahesabu hasara ya Urusi, waliweza kutambua majina yote 55 kwa kutumia zana za ziada za utafutaji wa habari. Kwa hivyo, 52% ya majina ya askari waliofariki kutoka ibada yamazishi ambapo hayakujulikana hapo awali.
Kwa hivyo, tunaweza kudhani kwamba orodha ya hasara iliyothibitishwa iliyohifadhiwa na BBC inaweza kuwa na angalau 40-60% ya majina machache ya waliofriki kuliko waliozikwa kweli nchini Urusi.
Kulingana na ujasusi wa Uingereza, hadi mwisho wa Mei, Urusi ilikuwa imepoteza watu wapatao 15,000 nchini Ukraine. Kwa mujibu wa na Mkuu kikosi wa Ukraine, idadi ya vifo vya wanajeshi wa Urusi imezidi 30,000.
Kwa tangazo
Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, vyombo vya habari na maafisa wamezidi kutaja "wanaojitolea" kati ya waliofariki ingawa hawakuwa wameandika kuwahusu kabisa hapo awali. Hali halisi ya watu hawa haipo wazi kila wakati.
Kufikia mwisho wa Mei, BBC ilikuwa imepata ripoti za vifo vya watu wasiopungua 81 waliotajwa kama watu wa kujitolea kwenye machapisho. Baadhi yao walipigana nchini Ukraine kama sehemu ya baadhi ya vikosi vya Cossack, wengine walipata mafunzo ya wiki moja katika chuo kikuu cha vikosi maalum huko Chechnya na, inaonekana, walitia saini mkataba wa muda mfupi na Wizara ya Ulinzi.
30% ya waliokufa wa askari iwa kujitolea ni watu zaidi ya miaka 40, watu kumi walikwenda kupigana wakiwa zaidi ya miaka 50.
Tangu mwanzoni mwa Machi, kazi za huduma za kandarasi zimekuwa zikijitokeza kwa maelfu kwenye tovuti maarufu za kutafuta kazi kama vile HeadHunter. Kama ambavyo BBC Idhaa ya Urusi inavyosema, kwa kujibu tangazo, unaweza kuingia kwenye vita nchini Ukraini baada ya wiki chache.
Licha ya hayo, mamlaka ya Urusi na Rais Vladimir Putin binafsi walidai kwamba ni wataalamu wa kijeshi tu na wanajeshi wa mkataba wanapigana nchini Ukraine.
Sasa kuna nafasi 500 zilizotumwa kwenye tovuti ya Idara ya Ulinzi pekee. Karibu 30% ya kesi katika vituo vya uteuzi kwa ajili ya huduma ya kijeshi ziko katika miji ya Dagestan - katika Makhachkala, Khasavyurt, Kaspiysk, Derbent na Buynaksk.
Hasara za Urusi
Wanajeshi wa Urusi waliofariki katika vita kati ya Urusi na Ukraine. Kufikia Mei 30, viongozi na vyombo vya habari vya Dagestan vilitaja idadi kubwa ya wanajeshi waliokufa kutoka mkoa huo ni 176.
Huko Dagestan, takriban wakazi 176 wa eneo hilo tayari wanajulikana kuwa wamefariki katika vita nchini Ukraine. Raia ndio wanaoongoza kwa idadi ya waliopoteza maisha katika vita hivi. Lakini takwimu hii haionyeshi kiwango halisi cha hasara kati ya wenyeji wa Dagestan, kwani inazingatia ripoti rasmi tu kuhusu "miili 200" na machapisho ya vyombo vya habari vya ndani na ripoti kutoka kwenye mazishi.
Nafasi ya pili kwa suala la idadi ya waliojeruhiwa bado inashikiliwa na Buryatia - mazishi ya wanajeshi 136 yalitangazwa hapo.
Katika nafasi ya tatu ni mkoa wa Volgograd na 109 waliofariki. Tangu katikati ya Mei, katika kituo cha kikanda - kwenye viingilio na katika usafiri wa umma - vipeperushi vilionesha wakazi wa Volgograd "kushiriki katika operesheni maalum."
Nyaraka rasmi zinaonsha wale tu ambao hapo awali walitumikia jeshi. Mshahara ulioahidiwa ni kuanzia ruble elfu 300. Mshahara wa wastani katika jiji ni wa chini kwa karibu mara nne.
Kwa mikoa miji mingi ya Urusi huduma ya kijeshi chini ya mkataba ni njia pekee ya kupata pesa. Watu wasio na uzoefu wa kweli wa kushiriki katika mapigano wanakubali kazi hiyo.
Kwa kulinganisha, ni vifo sita tu kutoka Moscow vinavyojulikana, ingawa wenyeji wa mji mkuu ni karibu 9% ya idadi ya watu wa Urusi.
Majenerali
Kwa sasa, BBC inajua kuhusu kifo cha majenerali watatu katika vita na Ukraine. Hadi hivi karibuni, mikoa ya Urusi ilithibitisha vifo vya wawili, lakini mnamo Mei 24 ilijulikana juu ya kifo cha Kanamat Botashev, jenerali mkuu mstaafu wa jeshi la anga.
Machi 22, Mkuu wa Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine walitangaza kuwa ndege ya Urusi ya Su-25 ilidunguliwa angani juu ya mji wa Luhansk, rubani hakupata muda wa kuiondoa. Wenzake wa zamani walithibitisha kwamba Jenerali mstaafu Botashev alifanya kazi kwenye Su-25. Botashev ndiye rubani wa cheo cha juu zaidi kati ya wanajeshi wote waliofariki.
Jisi alivyofika Ukraine haijabainishwa, lakini ushiriki wake katika vita vya anga kunaweza kuonyesha uhaba wa wataalam waliohitimu sana katika safu ya jeshi la Urusi linalopigana.
Mamlaka ya Ukraine hapo awali imeripoti vifo vya majenerali saba zaidi wa Urusi, lakini angalau wawili kati yao - Magomed Tushaev na Andrey Mordvichev - waligundulika kuwa hai, mara kwa mara walijitokeza kwenye rekodi za video na wanaendelea kushiriki katika mapambano nchini Ukraine.
"Hasara kubwa ya maafisa"
Kati ya askari 3,052 wa Urusi waliofariki nchini Ukraine, 152 ni wale wanaoitwa maafisa wakuu (majenerali, kanali, luten kanalii, meja). Wengine 405 ni maafisa wa chini wa jeshi. Kwa jumla, zaidi ya 18% ya waliofariki wanaojulikana ni maafisa.
Hapo awali, BBC Idhaa ya Urusi ilitaja kwamba asilimia kubwa kama hiyo inaweza kuwa kutokana na ukweli kwamba miili ya maafisa waliopoteza maisha huwasilishwa nyumbani kwa msingi wa kipaumbele. Lakini sababu nyingine ni muundo wa amri katika jeshi la Urusi.
Kazi nyingi za kuongoza vita huchukuliwa na maafisa. Wakati katika majeshi ya nchi za NATO, kazi nyingi zimeidhinishwa kutatuliwa na sajenti, koplo na vyeo vingine vya chini.
Mei 30, hii ilithibitishwa na ujasusi wa Uingereza. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Uingereza, Urusi kwa kweli inakabiliwa na hasara kubwa kati ya maafisa wa chini na wakuu.
Maafisa wadogo walipaswa kuelekeza hatua za chini kabisa za mbinu, kwani jeshi la Urusi halina sajenti waliofundishwa sana na wenye uwezo ambao huchukua jukumu hili katika majeshi ya Magharibi, "ujasusi ulisema.
Hasara hizi zitaongeza shida zilizopo katika jeshi la Urusi, na hata mbinu za vikundi vya kijeshi ambavyo jeshi la Urusi linaunda nchini Ukraine kutokana na vitengo vilivyobakia. vitakuwa na ufanisi mdogo kwa sababu ya uhaba wa makamanda.
Mwishoni mwa Mei, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza pia ilidai kwamba idadi ya wanajeshi wa Urusi waliokufa katika miezi mitatu ya kwanza ya vita huko Ukraine ina uwezekano mkubwa sawa na idadi ya hasara za Soviet katika vita vya Afghanistan. Kulingana na takwimu rasmi, karibu askari 15,000 wa Soviet walikufa katika vita hivyo.
"Mchanganyiko wa mbinu duni, ulinzi mdogo wa anga, ukosefu wa mabadiliko na utayari wa amri ili kukabiliana na vikwazo na makosa ya mara kwa mara imesababisha kiwango cha juu cha majeruhi ambacho kinaendelea kuongezeka wakati wa mashambulizi huko Donbass," Uingereza ilisema.
Tayari kuna wapiganaji wengi wa bunduki waliopoteza maisha kuliko askari wa miamvuli
Takriban 20% ya watu wote waliofariki walihudumu katika kitengo cha askari wa kushka bunduki (Riflemen. Hadi kufikia mwanzoni mwa Juni, kwa hali kamili ya hasara, vifo vya askari washika bunduki vilipita vile vya vikosi vya ndege (ingawa sehemu ya askari wa anga bado inachangia 19% ya vifo vilivyothibitishwa).
Wataalam wanaona kuwa hii inaweza kuwa ni kwa sababu ya hali ya vita ambayo jeshi la Urusi linaendesha hivi sasa. Katika wiki za kwanza za vita, Moscow ilifanya operesheni kubwa kadhaa ardhini. Sasa Warusi wanapigana vita vya muda mrefu kwenye eneo la Donetsk na Luhansk. Katika vita kama hivyo, mzigo mkubwa kawaida huanguka kwa askari wachanga, na sio tu kwa vikosi vya mashambulizi
Lakini kiwango hicho cha juu cha hasara miongoni mwa askari wa anga na wapiga bunduki kwenye magari kinaweza pia kuhusishwa na matatizo katika kuwapa askari vifaa vya huduma ya kwanza na vifaa vya kisasa vya huduma ya kwanza na mfumo duni uliowekwa wa kuwahamisha majeruhi kutoka mstari wa mbele.
Taarifa kuhusu vifo cha marubani wa kijeshi zinaendelea kuwasili. Kufikia mwanzoni mwa Juni, marubani 37 wa kijeshi (ikiwa ni pamoja na mabaharia na mafundi wa ndege na helikopta) inajulikana kuwa walizikwa. Hawa ni wataalamu wa vipande na wasomi wa jeshi lolote. Mafunzo ya rubani mmoja yanaweza kuchukua hadi miaka 10 na kugharimu kutoka dola milioni 3 hadi 7.
Orodha ya hasara ambazo tuliweza kuthibitisha ni pamoja na wafanyikazi 119 wa Walinzi wa Urusi, pamoja na wapiganaji kutoka vikosi vya wasomi Vityaz, Rosich na Typhoon. Miongoni mwa waliokufa ni angalau askari 53 wa kikosi maalum cha GRU na Kanali wa Luteni wa kikosi maalum cha FSB "Alpha". Mgawanyiko huu wote unachukuliwa kuwa na nguvu zaidi nchini Urusi.
Tunajisikiaje
Kila siku nchini Urusi, majina mapya zaidi na zaidi ya waliopotez maisha na picha za mazishi huchapishwa. Mara nyingi, majina hutolewa na wakuu wa miji ya Urusi au wawakilishi wa tawala za wilaya, vyombo vya habari vya mitaa na taasisi za elimu ambapo marehemu alisoma hapo awali, pamoja na jamaa.
BBC na timu ya watu waliojitolea wanachunguza takwimu hii na kuiongeza kwenye orodha ambayo tumekuwa tukihifadhi tangu mwanzo wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Hatuzingatii ripoti za vyombo vya habari kuhusu askari kadhaa na wakati mwingine mamia ya waliofariki, ikiwa hawana taarifa maalum kuhusu majina na ubini wao. Pia hatuzingatii ripoti za vifo vya askari mamluki wa kile kinachoitwa Wagner PMC.
Pia ni wazi kuwa hasara zingine haziripotiwi hadharani, kwa hivyo orodha yetu haijakamilika, na hasara halisi ya jeshi la Urusi na Walinzi wa Kitaifa huko Ukraine ni kubwa zaidi.
Walakini, idadi ya takwimu iliyokusanywa inatusaidia kutambua mwelekeo na kuchambua kile kinachotokea kwa jeshi la Urusi linalopigana huko Ukraine.