Je, Uingereza inatoa silaha gani kwa Ukraine?

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine walio mstari wa mbele sasa wanatumia silaha na vifaa vingine vinavyotolewa na Uingereza.
Serikali inasema inatumia £1.3bn ($1.6bn) kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine.
Kwa hivyo ni nini hasa kinachotumwa, na inaleta tofauti gani?
Silaha za kupambana na mizinga
Uingereza imetuma zaidi ya silaha 5,000 za kupambana na mizinga ya kisasa NLAW kwa Ukraine.
Ilha za NLAW zimeundwa kuharibu mizinga katika umbali mfupi kwa kurusha pigo moja.
Muhimu sana kwa vikosi vya jeshi vya Ukraine vinavyohitaji silaha mara moja, makombora hayo ni rahisi kusafirisha na ni rahisi kutumia. Askari anaweza kufundishwa kuzitumia chini ya siku moja.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Nlaw ilikuwa muhimu sana katika kwa kuipiga Urusi katika hatua za mwanzo za vita," anasema Justin Bronk, wa Taasisi ya Royal United Services
Silaha hizo NI ZILE "zinazofaa zaidi" zinapotumiwa pamoja na mizinga, anasema.
Anaonyesha mashambulizi yaliyofaulu kwenye safu ya mizinga, ambapo Nlaws zimeharibu magari ya mbele na kuwaweka nyuma ili kulenga mizinga.
Makombora ya masafa mafupi
Waziri wa Ulinzi James Heappey alithibitisha kwamba "mamia" ya makombora ya Brimstone yangetumwa Ukraine tarehe 28 Aprili.

Chanzo cha picha, BBC research
Makombora ya brimstones yanaweza kutumika dhidi ya vifaru, mizinga na vyombo vingine vidogo kama vile boti za kuweka vifaa vya kijeshi, kwa mujibu wa Kapteni Chris Carlson, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani.
Makombora hayo huwa yanarushwa kutoka kwenye ndege, lakini nchini Ukraine yanafanyiwa marekebisho ili yarushwe kutoka kwenye malori.
Kuzizindua kutoka ardhini kunapunguza ufanisi wake, anasema Capt Carlson.
Yakitumiwa kama makombora ya kuzuia meli, Brimstones ni ndogo sana kuweza kuzamisha meli kubwa, lakini inaweza kusababisha uharibifu mkubwa.
"Yote inategemea wapi unapiga," anasema. "Ikiwa itapiga injini au karibu na njia ya maji, unaweza kuwapa adui matatizo makubwa."
Magari ya kivita
Uingereza imetoa magari 120 ya kivita kwa Ukraine, yakiwemo magari ya doria ya Mastiff.

Chanzo cha picha, BBC research
Magari haya aina ya Mastiff yalikuwa maarufu sana miongoni mwa wanajeshi wa Uingereza nchini Afghanistan kwani yanatoa ulinzi wa hali ya juu dhidi ya mabomu ya ardhini na vifaa vya vilipuzi vilivyoboreshwa.
Wachambuzi wanasema kwamba katika eneo ambalo limechimbwa sana kama Donbas, Mastiffs zinaweza kuwa muhimu sana.
Inafahamika kuwa pande zote mbili katika mzozo huo zimetumia sana mabomu ya ardhini, mara nyingi kulazimisha magari ya adui katika maeneo ambayo yanaweza kulengwa kwa silaha za kukinga mizinga.
Ndege zisizo na rubani
Wizara ya Ulinzi inasema inasambaza "dazeni" za mifumo ya kuinua vitu vizito visivyo na rubani (UAV) ili kutoa msaada wa vifaa kwa vikosi vilivyotengwa.

Chanzo cha picha, BBC research
Wachambuzi wanasema kwamba ndege zisizo na rubani zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa kutoa vifaa katika "maili za mwisho" kwa askari wa mstari wa mbele, hasa chini ya tishio la silaha za mizinga ya Kirusi na katika hali ambapo kuna hatari ya kuzingirwa.
Wakati Urusi hadi sasa imeshindwa kuzingira idadi kubwa ya wanajeshi wa Ukraine mashariki mwa Ukraine, tishio la mizinga katika baadhi ya maeneo linaendelea kuwepo.
"Ni wingi wa vitu vinavyohitajika na wanajeshi," anasema Bw Bronk. "Kila wakati unaweza kutumia ndege isiyo na rubani badala ya askari kupeleka vifaa mbele ni mara chache zaidi mtu anapowekwa kwenye hatari kubwa."
Mifumo ya ulinzi wa anga
Uingereza inasema imetoa mifumo mitano ya ulinzi wa anga, ikiwa ni pamoja na makombora ya Starstreak.

Chanzo cha picha, Getty Images
Starstreak imeundwa kuteremsha ndege zinazoruka katika masafa mafupi.
Inapuuza hatua za kukabiliana kama vile miale na makapi yanayotumwa na ndege nyingi.
"Kwa mtazamo wa rubani, Starstreak ni jambo lisilopendekezwa," asema Bw Bronk. "Kuna kidogo sana unaweza kufanya kuhusu hilo."
Anasema vikosi vya Urusi vinaweza kuona oparesheni zingine kuwa hatari sana ikiwa wanafahamu kuwa silaha hatari kama Starstreak iko ardhini.
Hata hivyo, Starstreak inahitaji mafunzo zaidi kuliko mifumo kama vile Nlaw, na haina mbadala, wasema wachambuzi, kwa mifumo ya ulinzi wa anga ya masafa marefu.
Uingereza pia inasambaza "idadi ndogo" ya magari ya Stormer yanayofuatiliwa ili kufanya kazi kama jukwaa linaltembea la makombora ya Starstreak.

Chanzo cha picha, BBC research
Muda mrefu zaidi
Kudumisha usambazaji wa vifaa vya Magharibi, silaha na risasi itakuwa muhimu sana kwa Waukraine kwa muda mrefu, kulingana na Brig Ben Barry aliyestaafu katika Taasisi ya Kimataifa ya Mafunzo ya Kimkakati.
Anasema kwamba ingawa Ukraine ina uwezo wake wa kutengeneza silaha, itakuwa vigumu kwa wanajeshi wake kuchukua eneo kubwa kutoka kwa vikosi vya Urusi bila msaada mkubwa kutoka nje.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wataalamu wa kijeshi wanaeleza kwamba hitaji la Ukraine ni la vifaa ambavyo wanajeshi wake tayari wanajua jinsi ya kutumia au wanaweza kufundishwa kwa haraka sana.
Silaha nyingi za Ukraine zilibuniwa na kutengenezwa katika nchi za zamani za Warsaw Pact mashariki mwa Ulaya.
Kwa sababu hii, Uingereza imejitolea kutuma mizinga 2 ya Challenger 2 nchini Poland ili kujazia misaada yake ya mizinga ya T-72 kwa Ukraine.
Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimekuwa vikitumia T-72 kwa miongo kadhaa na vina uwezo wa matengenezo na vipuri pamoja na wafanyakazi waliofundishwa.
Katika siku chache kabla na baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, mawaziri wa Uingereza walisisitiza kwamba vifaa kwa Ukraine vitawekwa kwenye silaha za "kulinda".
Hiyo ina maana ya silaha ambayo inaweza tu kutumika kuilinda Ukraine kutokana na mashambulizi na si kushambulia Urusi.
Serikali imeashiria kuwa inaondokana na vifaa vya kujihami, lakini wataalam wengine wanahoji tofauti nzima.
Vifaa vingine vinavyotolewa na Uingereza ni pamoja na:
Zaidi ya makombora 200 ya kuzuia mashambulizi ya mizinga
Mabomu 1,360 ya anti-structure munitions
Tani 4.5 za vilipuzi vya plastiki
Zaidi ya raundi 400,000 ya silaha ndogo ndogo (small-arms munitions)
Zaidi ya vipande 200,000 pieces of non-lethal aid ikiwemo helmeti, body armour, range finders na vifaa vya matibabu.
Vifaa vya vita vya elektroniki
Mifumo ya rada ya kukabiliana na vikosi vya mizinga
Vifaa vya GPS
Maelfu ya vifaa vya kuoa usiku
Dazeni ya Mifumo ya UAV ya kuinua vitu vizito ili kutoa msaada wa vifaa kwa vikosi vilivyotengwa













