Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ramadhan 2022: Je kufunga kula kunaimarisha uwezo wa kumbukumbu wa ubongo?
Inaaminiwa kwamba kadri mtu anavyoendelea kuwa na umri mkubwa, ndivyo uwezo wake wa kukumbuka mambo unavyoendelea kuzorota.
Lakini baadhi ya tafiti zinasema kuwa tunaweza kukabiliana na tatizo hili na kurejesha uwezo wa kumbukumbu ya mambo, kulingana na kiasi cha chakula au vinywaji tunavyokunywa.
Dkt.Gilles Yew wa taasisi ya Kings College mjini London aliyewahi kushiriki katika utafiti wa awali alikusanya taarifa muhimu kuhusu suala hili.
Utafiti
Tafiti zilizofanywa kwenye panya zimeonyesha kuwa wakati vyakula vya kutia nguvu mwilini vimepungua, ubongo hutengeneza seli mpya au neva. Mchakato huu huitwa neurogenesis kwa lugha ya kitaalamu. Wanasayansi wamebaini kwamba uwezo wa kumbukumbu yao ulikuwa bora zaidi.
Madaktari katika Kings College, Sandrine Thuret na Curie Kim, wanachunguza iwapo hili linawezekana kwa binadamu pia.
Majaribio
Watu 43 akiwemo Dkt. Gilles, wa taasisi ya Kings college walichaguliwa kufanya majaribio.
Washiriki walikuwa ni watu wenye umri wa kuanzia miaka 45 hadi miaka 75. Kwa wiki nne, walilishwa chakula chenye viwango vya chini vya kutia nguvu mwilini. Ilikuwa ni kati ya gramu 500-600 za vyakula vya kutia nguvu mwilini, siku mbili kwa wiki. Siku nyingine tano walikula chakula cho cha kawaida. Na wakafunga.
Kumbukumbu ya kila mmoja wao Ilipimwa mwanzoni na mwishoni mwa wiki nne za majaribio.
Malengo ya majaribio yalikuwa ni kubaini tofauti kati ya uwezo wao wa awali na uwezo wao mpya wa kumbukumbu.
Kila mtu aliyeshiriki katika jaribio hilo alipimwa damu, ambayo ilichunguzwa kiwango cha protini ndani yake.
Utafiti umeonyesha kuwa seli mpya na neva vinaundwa kusaidia mtu anayefunga kula chakula na kupunguza virutubisho vya kutia nguvu mwilini.
Matokeo yake
Matokeo ya uchunguzi ni ya kutia moyo sana.
Ilibainika kuwa hali ya mwili kwa kila mshiriki aliyeshiriki majaribio haya ilikuwa bora zaidi, na viwango vyao vya protini ndani ya mwili viliongezeka. Uchunguzi huu ulionyesha kwamba kula chakula kidogo au kufunga, huongeza uwezo wa mtu wa kumbukumbu ya mambo.
Hata hivyo kuna matokeo tofauti yaliyojitokeza kwa baadhi ya watu. Kw amfano, umbo la mwili la Dkt Gilles lilibadilika na kuwa dogo kuliko awali na viwango vya protini havikubadilika.
Kulingana na wataalamu, huenda kukawa na sababu ambazo zilichangia matokeo haya.
Usingizi mzuri una uhusiano wa karibu na neva. Lakini wakati wa utafiti Dkt. Gilles alipata kiwango kidogo cha usingizi,na labda ilikuwa ninkwasababu ya njaa.
Dkt Gilles alikuwa ndiye mwenye umri mdogo zaidi ya washiriki wote waliofanyiwa uchunguzi. Hufanya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara.
Athari za kufunga kwa muda mfupi zitapungua. Sasa tunamfundisha mtu mwneye umri wa miaka 60 kufanya jaribio la kufunga.
Matokeo yanaonyesha, kuwa iwapo una umri n mkubwa na huwezi kufanya mazoezi sana, basi kufunga kwa siku mbii kwa wiki kunaweza kuboresha uwezo wako wa kumbukumbu.
Kwa hizo siku mbii, wanawake wanapaswa kupunguza viwango vyao vya vyakula vya kutia nguvu mwilini hadi gramu 500, huku wanaoume wakitakiwa kula gramu 600. Na kwa siku tano za wiki zilizobaki, unaweza kula tu kama kawaida unavyokula kila siku.