Bakteria wanaoishi kwenye kibofu cha mkojo wanaoweza kuwa dalili ya saratani ya tezi dume-utafiti

میتیازې

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Wanasayansi wanasema wamebaini bakteria ambao wanapatikana katika mkojo na wanahusishwa na saratani ya tezi dume.

Ugunduzi huu, wataalamu wanasema unaweza kusaidia kulenga saratani katika hatua zake za mapema na hata kuizuwia. Imebakia kushuhudiwa iwapo bakteria hawa wanaweza kusababisha saratani wenyewe au iwapo wataonyesha dalili tu.

Kikundi cha wanasayansi kutoka Chuo kikuu cha East Anglia, ambacho kilibaini uhusiano huu, kilisema utafiti zaidi utafanyika kubaini iwapo kutumia dawa za maambukizi (antibiotics ) zinaweza kuponya ukuaji wa saratani au uvipe wake.

Ni wazi kwamba maambukizi ya bakteria yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kusababishwa kwa baadhi ya aina za saratani . Hakuna bakteria aina ya pylori , kwa mfano, inayoweza kusababisha saratani ya tumbo, lakini antibiotics zinaweza kupunguza hatari.

اکټران وایي، پر وخت تشخیص ځکه ګټور دی چې ناروغ له لویو عملیاتو او ازموینو ژغورل کېدای شي

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ugunduzi wa mapema wa vimelea hawa ni muhimu kwasababuunaweza kuyaokoa maisha ya mgonjwa na hivyo kumuepusha na kufanyiwa upasuaji na vipimo, madaktari wanasema.

Saratani ya tezi dume kila mara inauwa-baadhi ya uvimbe hukua taratibu sana kiasi kwamba hausababishi matatizo-hauhitaji kuondolewa na unaweza kufuatiliwa kwa karibu.

Changamoto ni kung'amua na kuzuwia saratani ya tezi dume miongoni mwa wanaume wakati ingali katika hatua za mwanzo, ambayo inaweza kukua kwa kasi na inaweza kuuwa.

Kwa sasa kuna vipimo vya kimatibabu, kama vile vipimo vya damu au uchunguzi wa mara kwa mara-inawezekana mara kutambua saratani itakuwa mwelekeo gani na hatari kiasi gani.

Kuhusu utafiti wa hivi karibuni, wataalamu walichunguza ufanisi wa vipimo vya kibaiolojia vya vibofu visivyokuwa na mkojo vya wagonjwa zaidi ya sita, baadhi wenye saratani ya tezi dume na baadhi wasiokuwa nayo.

Walibaini aina tano za bakteria ambao walikuwa katika sampuli za mkojo zilizochukuliwa kutoka kwa wagonjwa wa kiume, na baadhi yao baadaye walipatwa na aina mbaya inayofanana na ya saratani ya tezi dume.

پروستات سرطان

Chanzo cha picha, SPL

Bakteria hawa wote wanaweza kukua bila oksijeni. Baadhi walikuwa ni wa aina mpya kabisa ambayo haijawahi kugundulika.

Watafiti walibaini aina mpya za bakteria na kuwapatia majina ya mhisani aliyethamini utafiti.

Dr Rachel Hurst, mjumbe wa timu ya watafiti alisema: "Kile ambacho bado hatujakifahamu hadi sasa ni vipi baktereia hawa huingia katika mwili wa binadamu , iwapo wanasababisha saratani na iwapo wanadhoofisha mfumo wa kinga ya mwili, au husababisha ukuaji wa bakteria. "

Aliongeza kuwa: "Tunatumaini kuwa utafiti wetu na kazi zaidi katika eneo hili unaweza kutua njia ya matibabu ambayo yanaweza kuzuwia aina mbaya ya saratani ya tezi dume. Utafiti wetu utaelekezwa katika kutafuta vipimo vya aina hizi mpya za bakteria ." Inatoa njia kwa ajili ya tiba yenye ufanisi zaidi kwa mtu yeyote mwenye saratani.

Profesa Colin Cooper mtafiri mwenzake na Rachel Hurst, ambaye aliongoza utafiti huu, aliiambia BBC kwamba matokeo ya utafiti wake yalikuwa sahihi na alikuwa mwangalifu kuhakikisha anaweka mbali sampuli na virusi wakati wa vipimo vya maabara.

Maelezo ya video, Ayalo: Nimeumizwa sana na saratani ya tezi dume

Matokeo hayakuathiri

Dkt Sam Godfrey, mjumbe wa taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza, alisema : "Karibu sababu nne kati ya kumi zinazosababisha nchini Uingereza huhusiana na uvutaji wa sigara au unene wa kupindukia wa mwili, kwa mfano. Lakini kuna sababu nyingine pia.

Kuna sababu nyingine pia zinazochangia katika kusababisha saratani, kama vile bakteria, na sasa tuna taarifa sahihi kuwahusu bakteri . "

Aliongeza kuwa: "Utafiti zaidi unahitajika kuonyesha jinsi bakteria wanavyochangia katika kusababisha sararani ya tezi dume. "

Maelezo ya video, Gharama ya kutibu saratani Kenya