Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanawake wenye ndevu: 'Haijalishi ukiambiwa wewe ni mbaya, inauma kuambiwa unafanana na mwanaume'
Wanajiita wanawake wenye ndevu na wengine sasa hawafichi tena ndevu hizo kwenye nyuso zao na wameanza kujitokeza na kueleza uzoefu wao.
Wamekuwa wakishiriki sana katika mitandao ya kijamii na hata wameunda makundi ili kuonekana.
BBC Mundo ilizungumza na wanawake wawili kati yao ili kuelewa jinsi mchakato wao wa kujikubali na kuikubali hali ya kuwa na ndevu ulivyokuwa na masuala mengine.
Na huu ndio uzoefu na simulizi zao:
LUTA: Jina langu ni Luta Cruz. Nilizaliwa Chile, mimi ni mwanamke, afro, mimi kutunga nyimbo, mimi kuimba na mimi ni hairy.
Nina nywele nyingi. Nimekuwa napata nywele mpaka kwenye vidole vyangu vya mikono.
Niligundua kuwa nywele nyingi kwa mara ya kwanza nilipokuwa na umri wa miaka 11.
Mama yangu alinipeleka kwenye nyumba ya rafiki yangu ili kuziondoa.
Nadhani alitaka kujilinda kwa sababu nilikuwa tayari na nywele nyingi, ajabu: Niliitwa msichana mwenye manywele nchini Chile na kwa kuongeza, nilikuwa na nywele mpaka usoni.
ANA: Mimi ni Ana Dino. Mimi ni mwanamke, mchoraji na msanii wa kuona. Mimi natoka Mexico na nina ndevu.
Katika umri wa miaka 13 sikuwa nimegundua kuwa nina ndevu zangu, alitokea mwanaume mmoja alinambia ananipenda, lakini tatizo lilikuwa nina nywele nyingi.
Sikutilia maanani sana jambo hilo hadi nilipofika elimu ya juu ya sekondari, nywele zangu zilianza kujitokeza zaidi na watu wakaanza kuninyooshea vodole. Niliamua kunyoa.
Nilipata matibabu kwa miezi sita ambapo waliweka sindano ndogo katika kila kitundu ya nwele ili kuchoma mizizi (chanzo) na kisha kuzivuta nywele.
Ulikuwa mchakato wa kutisha
Niliishia kuvimba sana uso, ukawa mwekundu. Nilipata mpaka na mzio (aleji).
Mwishowe nilifanikiwa kupunguza kiasi kidogo, lakini nywele ziliendelea kuonekana.
ANA: Nilipokwenda kutembea na marafiki nililazimika kubeba mkoba na kuficha vifaa vyote kama: taa, kioo, na vitu vingine.
Sikumwambia mtu yeyote kuhusu ndevu zangu na utaratibu wangu wa kuondoa nywele. Niliishi kwa miaka mingi kwa aibu na kutafuta kuificha.
LUTA: Nilimuona daktari kwa mara ya kwanza nilipokuwa na umri wa miaka 13. Alikuwa daktari wa masuala ya uzazi, alinigundua nina ovari za 'polycystic' na alielezea kuwa ovary hiyo ndiyo iliyosababisha kuwa na nywele za ziada.
Hirsutism:
Hirsutism ni hali ambayo huathiri zaidi wanawake na husababisha kuongezeka kwa nywele nyeusi au nene zinazofanana zile za wanaume, hasa kwenye uso, kifua na mgongo.
Ukuaji wa nywele hizi huwa hatua kadhaa.
Hatua mojawapo inaitwa anagen, ambayo hutokea wakati nwele hukua kwa haraka ambapo nywele hukomaa na kuwa nyeusi.
Hirsutism inaweza kutokea kwa sababu mbalimbali.
"Kuna sababu mbili kuu: ongezeko la uzalishaji wa homoni za kiume (androgens), kama vile testosterone, na kuongezeka kwa unyeti wa ngozi kwa androgens hizi," anasema Felizzola, ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Endocrinology cha Colombia.
"Lakini pia kunaweza kuwa na matatizo ya yanayohusiana na metaboliki na pia tatizo hili la hirsutism linaweza kutokuwa na sababu inayoyojulikana na hutokea karibu 5% ya waliofikwa nalo, "anaongeza mtaalamu.
LUTA: Kwa miaka kumi nilitumia vidonge vya uzazi wa mpango, lakini nywele ziliendelea kubaki .
Nilipotimiza miaka 25 niliamua kutafuta suluhisho la uhakika. Nilikuwa nimechoka.
Nilienda kwa daktari mmoja mpaka mwinginebila mafanikio, mapaka nilipoamua kufanya kitaalamu kitu kinaitwa endocrinology consultation.
Nikafanya vipimo kadhaa na nikaambiwa kwamba utambuzi wa miaka yangu 13 haukufanana. Nilikunywa dawa zisizostahili.
Walinambia nadhani nilikuwa na Congenital Adrenal Hyperplasia (HSC).
Nakumbuka nilikuwa nawaza, Ee Mungu wangu, hii ni kitu gani? Nitakufa,... Ni kitu gani hichi chenye jina refu hili.
Nilifana vipimo vingi sana maabara. Mwishowe waliniona nikiwa na afya.
Congenital Adrenal Hyperplasia:
Ni hali ya maumbile ambayo huathiri tezi za adrenal, viungo vilivyoko juu ya figo, ambayo hutoa homoni ambazo husaidia kudhibiti metaboliki, mfumo wa kinga, shinikizo la damu, na kazi zingine muhimu.
Miongoni mwa homoni wanazotengeneza androgens ni kama vile testosterone.
Tiba ya kuwa na nywele za ziada
Moja ya matatizo katika kutibu nywele za ziada ni kwamba inahusishwa na homoni ambazo haziwezi kupimwa, kama vile dihydrotestosterone, na unyeti wa androgenic wa ngozi, ambayo pia haipimwi, anasema Dk Felizzola.
Wanawake wenye 'hirsutism mara nyingi huaelekezwa kutumia dawa ambazo husaidia kupunguza kiasi cha androgens.
Lakini sio suluhisho la uhakika, kwani unyeti wa androgenic ni wa juu sana kwenye ngozi kwamba ni vigumu sana kukabiliana na athari zake.
Kwa kuongeza, unapaswa kuzingatia madhara ambayo dawa nyingi zinazo.
"Dawa za uzazi wa mpango, kwa mfano, zinaweza kupunguza kitu kinaitwa 'libido," anasema mtaalam.