Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine na Urusi: Mkataba wa Montreux ulivyozuia meli za kivita za Urusi kupitia Bosphorus
Ingawa vita vya Ukraine vimeendelea kupambamba moto, makubaliano ya kimataifa yaliyotiwa saini mnamo 1936 yanazuia vita hivyo kuwa mbaya zaidi.
Mkataba wa Montreux wa kupita kwenye mlango wa bahari unaipa Uturuki udhibiti wa njia ya bahari kati ya Bahari Nyeusi, makao ya jeshi kubwa la wanamaji la Urusi, na Bahari ya Mediterania.
Mkataba hui hasa, unaweka mipaka ya kupita kwa meli za kivita za kiraia na za kijeshi kupitia njia ya Dardanelles na Bosporus, ambayo pamoja na Bahari ya Marmara huunda kiungo cha baharini kati ya Bahari Nyeusi na Mediterania.
Mkataba huo wa kimataifa ulitiwa saini na Australia, Bulgaria, Ufaransa, Ugiriki, Japan, Romania, Yugoslavia, Uingereza, Muungano wa Sovieti, na Uturuki, na umekuwa ukitekelezwa tangu Novemba 1936.
Sasa Mkataba wa Montreux una jukumu muhimu katika mzozo wa Ukraine.
Ukraine imeiomba Uturuki kufunga mlango wa bahari wa meli za kivita za Urusi, ikionyesha jukumu la Uturuki katika kudumisha amani ya eneo hilo.
Serikali ya Uturuki ilikubaliana February 28, 2022.
Lakini manuari kadhaa za kivita za Urusi tayari zilikuwa zimeingia Bahari Nyeusi mapema mwezi Februari. Na Uturuki ilikuwa imesema itazizuia kuingia Bahari nyeusi ikiwa Urusi itasema zinarejea katika bandari yao ya nyumbani
Meli zinazopitia Bahari Nyeusi zinadhibitiwaje?
Kuna mambo manne muhimu katika Mkataba wa Montreux ambayo hudhibiti ni meli gani zinaweza kuingia katika Bahari Nyeusi wakati wa vita:
- Uturuki huenda ikafunga njia hiyo ya baharini kwa meli za pande zinazozozana nyakati za vita au wakati Uturuki yenyewe ni seheumu ya mzozo au inatishiwa na uvamizi wa taifa lingine.Uturuki inawena kufunga mkondo huo kwa meli za wafanyabiashara zinazomilikiwa nan chi zilizo vitani na Uturuki.
- Nchi yoyote iliyo na ufukwe kwenye Bahari Nyeusi (Romania, Bulgaria, Georgia, Russia au Ukraine) Lazima ziarifu Uturuki kuhusu nia yao ya kupitisha manuari ya kivita kupitia mkondo huo siku nane kabla.
- Wakati wale ambao hawapakani na Bahari ya Nyeusi lazima waiarifu Uturuki siku 15 kabla. Ni mataifa ya Bahari Nyeusi pekee ndio yanaruhusiwa kutuma nyambizi kupitia mkondo huo wa bahari, tu kwa taarifa ya awali na ikiwa tu hizo zimejengwa au kununuliwa nje ya Bahari Nyeusi.
4.Ni meli tisa za kivita zinaruhusiwa kupitia mkondo huo kwa wakati mmoja, na kuna udhibiti uliowekewa ukubwa wa meli, kibinafsi na kwa makundi.
Meli zilizokua na uzani wa zaidi ya tani 15,000 za metriki hazikuruhusiwa kupita. Meli za kisasa za kivita ni nzito, kama frigates zina uzani wa karibu tani 3,000 na zile aina ya destroyer na cruiser zikiwa na uzani wa karibu tani 10,000 za metriki. Meli za kisasa za kubeba ndege ni kubwa sana haziwezi kupita.
Vita vikuu vya pili vya Dunia
Zamani, Uturuki iliwahi kutumia mamlaka ya Mkataba wa Montreux. Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Uturuki ilifunga njia ya bahari kwamataifa yanayopigana.
Hilo lilizuia mamlaka za Axis kutuma meli zao za vita kushambulia Muungano wa Sovieti na kuzuia ushiriki wa jeshi la wanamaji la Sovieti katika mapigano ya Mediterranea.
Katika mazingira ya sasa, serikali ya Uturuki imejipata katika njia panda ,kwa sababu Ukraine na Urusi ni washirika wake muhimu wa kibiashara, jeshi na mikataba ya kawi.
Uturuki, mwanachama wa NATO tangu 1952, inataka kuimarisha ushirikiano wake nan chi za Magharibi bila kuikwaza Urusi. Kwa hivyo, udhibiti wake juu ya mambo haya muhimu unaweza kupima jukumu lake la kusawazisha mambo kiatika kanda hiyo.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJAUrusi na Ukraine: Mlipuko wakumba Kyiv huku Urusi ikiendeleza mashambulizi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine