Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Paola Schietekat: Mmexico ahukumiwa viboko 100 nchini Qatar baada ya kushutumu kuwa alishambuliwa
Wakati ambapo Qatar inafungua fursa kwa ulimwengu huku Kombe la Dunia likikaribia, raia wa Mexico amelaani jinsi wanawake wanavyoweza kuathirika sana na kuwa katika hatari katika nchi hiyo ya Kiislamu.
Paola Schietekat aliwasili Doha mnamo Februari 2020 kufanya kazi na serikali ya Qatar katika kuandaa Kombe la Dunia la Qatar 2022.
Baada ya kuishi huko kwa mwaka mmoja na nusu, anasema kwamba alikuwa mwathirika wa kushambuliwa.
Lakini alipoenda kwa mamlaka kuwasilisha malalamiko, kesi ilimgeukia: alishtakiwa kwa kushiriki "ngono nje ya ndoa," uhalifu chini ya sheria za Kiislamu.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 27 alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela na kuchapwa viboko 100.
Vinginevyo, walimwambia, angeweza kuepuka adhabu hiyo ikiwa angeolewa na mshambuliaji wake.
"Baada ya mchakato huu, niligundua kuwa licha ya digrii zangu za kitaaluma, maandalizi ya kitaaluma, uhuru wa kifedha na licha ya kufanya kazi kwa serikali ya Qatar, niko katika hatari ya kupitia ukiukwaji wa haki za binadamu na taasisi za kizamani na zenye kuendeleza unyanyasaji, na siwezi kupata ulinzi katika ubalozi wangu," Schietekat alishtumu tukio hilo kupitia ukurasa wa Facebook ambako alifichua kilichotokea.
Mwanamke huyo kijana alifanikiwa kuondoka Qatar mwaka jana, lakini tangu wakati huo anasema kuwa haki haijatendeka katika kesi yake na kwamba mshambuliaji wake yuko huru.
Na anaonya kwamba watu wa Mexico, na pia vikundi vilivyo hatarini kama vile wanawake na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanaotembelea nchi hiyo kwa Kombe la Dunia baadaye mwaka huu, wanaweza kuwa waathiriwa wa mfumo wa Qatar.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico Marcelo Ebrard alikutana naye Ijumaa iliyopita na kumhakikishia kuwa wakili bora zaidi atapatikana kumtetea.
Anasikitika kwamba msaada huo haukufikia hadi kesi yake ilipoanza kugonga vichwa vya Habari huko Mexico na kimataifa wiki iliyopita.
Madai ya kushambuliwa
Kulingana na Mashariki ya Kati tangu 2019, Schietekat alihamia Qatar mnamo Februari 2020 kufanya kazi kama mwanauchumi wa Kamati Kuu, chombo kinachosimamia kuandaa Kombe la Dunia la Qatar 2022.
Ilikuwa kazi ya ndoto yake, kama yeye mwenyewe alivyosema, hadi ilipokatizwa ghafla mnamo Juni 6, 2021. Kulingana na malalamiko ya kijana huyo wa Mexico, usiku alipokuwa amelala, mtu anayemjua kutoka jamii ya Latino huko Doha aliingia nyumbani kwake kwa nguvu na kumshambulia kimwili.
Shambulio hilo linadaiwa kumsababishia majeraha kadhaa kwenye mkono na tumbo, alisema.
Alikwenda polisi kuripoti shambulio hilo, lakini kwasababu hajui kiarabu kwa ufasaha na ukosefu wa ushauri kutoka kwa ubalozi wa Mexico, au wakili wa nje ya nchi, kulingana na maelezo yake, mambo yalianza kumbadilikia.
"Ubalozi haukunishauri jinsi malalamiko yangu yanavyoweza kutumika dhidi yangu," msichana huyo alieleza kwa vyombo vya habari vya Mexico.
Na kwa hilo, nikawa natafuta kufikia matokeo ya mwisho ya kisheria, kama ilivyopendekezwa na balozi wa Mexico nchini Qatar, Luis Ancona, sheria ya Kiislamu inawaweka wanawake katika hali ya hatari au wanakuwa na uwezo mkubwa wa kupitia mabaya ikilinganishwa na wanaume.
Kushtumiwa kwa "zinaa"
Mshambulizi wake aliitwa kufika mbele ya mamlaka, lakini alitumia hoja iliyompendelea: alidai kwamba alikuwa na uhusiano na Schietekat.
"Ingawa hakukuwa na ushahidi wa kuunga mkono madai yake, hakukuwa na dhana ya kutokuwa na hatia kwangu pia. Na kama nilikuwa mwathirika, mamlaka ilinichukulia kama mhalifu," msichana huyo alisema.
Kulingana na Wizara ya Mahusiano ya Kigeni (SRE) ya Mexico, mamlaka ya Qatar ilianzisha uchunguzi "ambao matokeo yake yalikuwa shutuma za mzalendo huyo na aliyeshitaki akawa na hatia ya utendaji wa zina ambao ni uhalifu."
Hivi ndivyo jinsi mahusiano ya ngono nje ya ndoa au mahusiano ya kabla ya ndoa yanavyofafanuliwa, ambayo adhabu yake ni hadi miaka 7 jela na viboko 100.
"Sheria ya Qatar inaadhibu vikali baadhi ya tabia chini ya kanuni za kidini (sharia)," inaeleza SRE.
Katika mchakato huo, polisi walijaribu kumfanya awe ni mwenye kufanyiwa "vipimo vya ubikira", kitendo ambacho Schietekat alikielezea kama cha "kudhalilisha, kufedhehesha na kurudisha enzi zilizopitwa na wakati"; ambacho alifanikiwa kukiondoa kwa nguvu kwa kuwasilisha cheti cha talaka ambayo alipitia hapo awali.
"Ofisi ya Mwendesha Mashtaka iliniachia kwa sharti la kuacha simu yangu ya mkononi ili kukamilisha upelelezi wa kesi ya 'uasherati'," alisema.
Ingawa aliachiliwa kwa dhamana, jambo lile lile lilifanyika kwa mtuhumiwa wake aliyemchokoza, jambo ambalo alihofia uadilifu wake ikiwa angebaki nchini humo.
Usaidizi kutoka ubalozi wa México
Schietekat alidokeza kwamba ubalozi wa Mexico nchini Qatar ulimpa "msaada" mwanzoni, lakini ulifanya hivyo "kwa kutojua tamaduni, sheria na lugha ya wenyeji, ambayo ilichangia usimamizi mbovu wa haki. "
Usaidizi niliopokea kutoka kwa balozi ulikuwa wa chini na wa dharau," alisema, akiongeza kuwa mara tu alipoajiri wakili wa nje, mamlaka ya Mexico ilimwacha na hata kuondoa hofu ya kushambuliwa na mshtakiwa.
Kabla, ya kufikisha malalamishi yake kupitia mitandao ya kijamii, walipendekeza "funga mlango," msichana alisema.
Schietekat alifanikiwa kuondoka Qatar siku ya 20 baada ya shambulio hilo.
Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexico ilisema katika taarifa yake wiki iliyopita kwamba ubalozi huo "umetoa msaada kwa raia wa nchi hiyo na umehakikisha kwamba utaratibu unaostahili unaheshimiwa, kwa mujibu wa sheria zinazotumika nchini humo. "
Kwake, kauli hiyo ilikuwa na "lengo la kubatilisha kinachoendelea. Hakukuwa na huruma na taarifa hizo zilikuwa za uongo," alisema.
Raia wengi wa Mexico walionyesha kumuunga mkono Schietekat, ambaye amesema anatumai haki itatendeka katika kesi yake na hata kutathmini uwezekano wa kurejea Qatar.
Mnamo Machi 6, kesi hiyo imepangwa kusikilizwa huko Doha kutatua hali yake na ambayo mwanamke huyo kijana anajiandaa.