Fahamu uwezo mkubwa wa jeshi la China unavyotishia Marekani na nchi za Magharibi

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

China imekuwa ikiimarisha jeshi lake kwa kasi kubwa.

Kiasi kwamba maendeleo katika teknolojia ya makombora, silaha za nyuklia na ujasusi wa nchi hiyo yenye nguvu katika bara la Asia yanaleta wasiwasi na kutikisa nguvu za nchi za Magharibi.

Rais Xi Jinping ameliagiza jeshi la nchi hiyo kumaliza mchakato wao wa kulifanya jeshi hilo kuwa la kisasa ifikapo mwaka 2035.

Anasema, Beijing inapaswa kuwa na "nguvu ya kijeshi ya kiwango cha ulimwengu", yenye uwezo wa "kupigana na kushinda vita," kufikia mwaka 2049.

Hilo ni jambo kubwa na ahadi kubwa kwa nchi hiyo iliyo katika mstari sahihi.

Gharama kubwa

Baadhi ya wataalamu wa kimataifa wameikosoa China kwa "ukosefu wa uwazi" kuhusu ni kiasi gani cha fedha inatumia katika ulinzi na wanaikosoa pia kwa kuwasilisha takwimu "zisizoendana".

Beijing inachapisha takwimu rasmi juu ya matumizi yake ya kijeshi, lakini makadirio ya nchi za magharibi kuhusu uwekezaji wa China kwenye majeshi ni kubwa zaidi ya kinachosemwa na China.

China inaaminika kutumia fedha nyingi zaidi kwenye majeshi yake kuliko nchi nyingine yoyote duniani isipokuwa Marekani.

Jinsi uwekezaji wa kijeshi wa China unavyoongezeka

Ukuaji wa bajeti ya kijeshi ya China umezidi ukuaji wake wa uchumi kwa ujumla kwa angalau muongo mmoja, kulingana na Kituo cha Mafunzo ya Mkakati na Kimataifa huko Washington.

Kuongeza hifadhi za nyuklia

Mwezi Novemba, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitabiri kuwa China ingetumia silaha zake za nyuklia ifikapo mwishoni mwa muongo mmoja.

Alisema China "huenda inakusudia kuwa silaha za aina hiyo 1,000 ifikapo mwaka 2030."

Vyombo vya habari vya serikali ya China viliuita utabiri huo kuwa "uvumi wa uwongo na wa upendeleo," ukibainisha kuwa silaha za nyuklia ziko katika "kiwango cha chini."

Hata hivyo, Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, ambayo inachapisha tathmini ya kila mwaka ya jumla ya hifadhi za dunia za silaha za nyuklia, inasema China imeongeza idadi yake ya silaha hizo za kivita katika miaka ya hivi karibuni.

China bado ina safari ndefu kuipiku hifadhi za Marekani yenye silaha hizo 5,550, lakini ujenzi wake wa nyuklia unachukuliwa kuwa moja ya vitisho vikubwa kwa nguvu za kijeshi za Magharibi.

"Silaha za nyuklia za China ni tatizo kubwa" alisema Veerle Nouwens wa Taasisi ya Royal ya Royal Institute for United Services huko London.

"Kuna ukosefu mkubwa wa imani kwa pande zote mbili na mazungumzo hayako karibu kufikiwa. Kuna hatari kubwa na njia za kujinasua hapo hazionekani."

Silaha za Hypersonic

Makombora ya Hypersonic husafiri mara tano kwa kasi zaidi kuliko kasi ya sauti.

Hayana kasi kubwa kama makombora ya masafa marefu, lakini ni vigumu sana kuigundua katika ndege na kuizuia.

"Wachina wanaelewa kwamba wako nyuma sana, kwa hivyo wanajaribu kupiga hatua kubwa ili kudhibiti nguvu zingine," anasema mtaalamu Zeno Leoni wa King's College London.

China imekanusha kufanya majaribio ya makombora ya hypersonic, lakini wataalamu wa nchi za Magharibi wanaamini kuwa kurushwa kwa makombora mawili msimu uliopita wa joto kunaashiria kuwa majeshi yake yako katika njia sahihi.

Haijulikani ni mifumo gani ambao China inaweza kuibuka nao. Lakini kuna aina mbili kuu:

  • Makombora ya Hypersonic glide ambayo yanabaki ndani ya anga ya dunia.
  • Mifumo ya Mabomu ya Mzunguko wa Fractional (FOBS) ambayo inaruka katika obiti ya chini kabla ya kuelekea kwenye lengo kwa kasi.

Dr. Leoni, kutoka King's College London, anaelezea kwamba wakati makombora ya hypersonic peke yake hayawezi kuleta mabadiliko, lakini watafanya maleneo lengwa kuwa na mazingira makubwa ya hatari ya kushambuliwa.

"Makombora ya Hypersonic hufanya ndege kushindwa kuwa ngumu zaidi kuzizuia," anaongeza.

Hata hivyo, inaonyesha pia kwamba tishio la makombora ya China ya hypersonic inaweza kuwa imetiwa chumvi na baadhi ya maafisa wa Magharibi, ambao wanataka kutafuta sababu ya kufadhili teknolojia ya anga za kijeshi.

Mustakabali usio na uhakika

Je, China inaondoka katika hali isiyo ya makabiliano kuelekea kuwa tishio zaidi?

Kwa sasa, muelekeo wa China unasalia kuwa "kushinda bila kupigana," kwa mujibu wa Dk. Leoni, ingawa anaongeza kuwa mkakati huu unaweza kubadilika katika siku zijazo.

"Kuwa na nguvu za kisasa kabisa za jeshi lake la majini inaweza kuwa chanjo cha hali hiyo kubadilika."

Kwa upande wake, Kanali Zhou anasisitiza kuwa hofu za Magharibi hazina msingi.

"China haina nia ya kufuatilia ulimwengu, tofauti na Marekani," alisema. "Hata kama China itakuwa na nguvu zaidi siku moja, itadumisha sera zake za msingi."

China haijapigana vita tangu mwaka 1979, ilipoingia vitani na Vietnam, uwezo wake mwingi wa kijeshi haujajaribiwa kikamilifu.

Nchi za Magharibi na China zinatarajia kuendelea kuwa hivyo.