Mzozo wa Tigray: Tunachofahamu kuhusu mashambulizi ya kutumia ndege zisizo na rubani nchini Ethiopia?

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Woman injured by air strike in Ethiopia's Tigray region

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mmoja wa majeruhi wa shambulio la Dedebit akitibiwa katika hospitali

Makumi ya watu wameuawa katika mashambulizi ya anga katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia katika miezi ya hivi karibuni.

Baadhi ya mashambulio hayo yamehusisha utumiaji wa ndege zisizo na rubani, na kuna wasiwasi juu ya idadi ya vifo vya raia.

Serikali, ambayo imekuwa ikipambana na waasi kwa zaidi ya mwaka mmoja, inasema ina haki ya kutumia silaha zozote inazoona zinafaa.

Inakanusha kuwa imelenga raia.

Januari 8: Mashambulizi kwenye kambi ya watu waliohama makwao

Shambulizi la anga kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dedebit huko Tigray mnamo Januari 8, liliua zaidi ya watu 50 na kuwaacha zaidi ya mia moja wakiwa na majeraha.

Picha zilizotolewa kwa Politico na wafanyikazi wa misaada - zimesababisha wachunguzi kuamini kuwa silaha moja iliyotumiwa katika tukio hili inaweza kuwa kombora lililorushwa kutoka ndege isiyo na rubani ya Bayraktar TB2 inayotengenezwa nchini Uturuki.

Map showing airports and site of three drone strikes

Vipande - ikiwa ni pamoja na vipande vya mabawa - vinaonekana kufanana na aina ya vile vinavyotumiwa kwenye ndege hizi zisizo na rubani, kulingana na watafiti kutoka kundi la amani la Pax lenye makao yake Uholanzi na Amnesty International.

Uwepo wa ndege zisizo na rubani za Uturuki nchini Ethiopia ulifichuliwa mwezi wa Disemba na Wim Zwijnenburg, mpelelezi anayefanya kazi na Pax.

Aliangazia picha za satelaiti zinazoonyesha ndege zisizo na rubani za Uturuki zikiwa zimeegeshwa kwenye kituo cha anga cha serikali kusini mwa eneo la Tigray.

Wanaweza kutambuliwa kwa kulinganisha vipimo, ikiwa ni pamoja na mbawa na urefu, kutoka kwa picha za satelaiti.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Hatujui iwapo ndege hizi zisizo na rubani zilitumika katika tukio hili, na serikali ya Ethiopia haijathibitisha matumizi yao.

Uturuki ilisaini makubaliano ya ushirikiano wa kiulinzi na Ethiopia mwaka jana, ingawa maelezo hayakuwekwa wazi.

Shirika la habari la Reuters liliripoti mwezi Disemba kwamba Marekani ilielezea wasiwasi wake kwa serikali ya Uturuki kuhusu mauzo ya ndege zisizo na rubani kwa Ethiopia.

Januari 6: Shambulio dhidi ya waasi wa Oromo

Mashambulizi mapema Januari yalifanywa dhidi ya waasi katika eneo la Oromia, ambao walikuwa wamepiga hatua sawa waasi wa huko Tigray.

Maelezo machache yameibuka, na haijulikani ikiwa kulikuwa na maafa.

Hata hivyo, mashambulizi ya anga katika eneo la Gidami yaliacha ushahidi - vipande vya makombora - ambayo kulingana na uchunguzi, ulionyesha matumizi ya silaha za Iran.

Satellite image showing an Iranian drone at Harar Meda airport

Picha za satelaiti za Desemba mwaka jana zilifichua kuwepo kwa ndege isiyo na rubani ya Iran katika uwanja wa ndege wa Harar Meda, iliyotambuliwa kwa vipimo na njia zingine.

Mchunguzi wa ufuatiliaji wa ndege amegundua takriban ndege 15 za mizigo kutoka Iran hadi viwanja vya ndege vya Harar Meda na Bole mnamo Agosti 2021 na kile zilizobeba hakijulikani.

Hata hivyo, Oktoba mwaka jana, mamlaka ya Marekani ililaani hadharani Iran kwa mauzo yake ya ndege zisizo na rubani na kuitaja Ethiopia kuwa mojawapo ya wapokeaji wa teknolojia ya ndege zisizo na rubani za Iran.

Desemba 16: Shambulio katika la soko la Alamata

Katikati ya Desemba mwaka 2021, mfululizo wa mashambulizi ya anga yalisababisha vifo vya raia 28 katika soko la Alamata kusini mwa Tigray.

Kundi kuu la waasi la Tigray, TPLF, lilidai ndege za serikali na ndege zisizo na rubani zilihusika.

Picha za video zilionyeshwa kwenye kituo cha televisheni cha Tigrayan, zikionyesha mabaki ya kombora linalosemekana kutumika katika tukio hili.

Bomba la nyuma la kombora, ambalo hufahamika kustahilimi kishindo, linaweza kutambuliwa kutoka kwa picha.

Uchunguzi mmoja ulihitimisha kuwa, kulingana na picha hizo, vipande hivyo vilifanana na kombora la Blue Arrow 7 lililoundwa na China ambalo linaweza kupachikwa kwenye ndege isiyo na rubani.

Picha za satelaiti zilifichua kuwa ndege zisizo na rubani za Wing Loong zilizotengenezwa na China ziliegeshwa katika kambi ya kijeshi ya Harar Meda ya Ethiopia tarehe 15 Desemba - siku moja kabla ya shambulio la Alamata.

Wachunguzi wa tovuti wanaamini kuwa China ilikuwa chanzo cha ndege zisizo na rubani za Wing Loong za Ethiopia, ambazo awali zilikusudiwa kutumiwa kwa uchunguzi.

Data kutoka kwa programu za kufuatilia ndege zinaonyesha shehena kutoka Chengdu nchini Uchina, kilipo kiwanda cha kampuni mtengeneza ndege zisizo na rubani ya Chengdu Aircraft Industry, hadi Ethiopia Septemba na Oktoba mwaka jana.

Screengrab from Tigrai TV showing the remains of a tailpipe from a Blue Arrow 7 Missile
Maelezo ya picha, Masalia ya vifusi vya nyuma vya mabomba kutoka kwenymakombora yalipatikana baada ya shambuliokatika Alamata (yalionyeshwa kwenye Tigrai TV)

Lakini kuna nchi nyingine yenye ndege zisizo na rubani za Wing Loong na makombora ya Blue Arrow ambayo pia yametuma vifaa nchini Ethiopia ambayo ni UAE.

Kwa kutumia data ya silaha inayodumishwa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI), UAE ina ndege zisizo na rubani za Wing Loong, na makombora ya Blue Arrow.

Satellite image showing an Wing Loong drone at Harar Meda airport

Chanzo cha picha, PLANET LABS

Maelezo ya picha, Two Chinese-made Wing Loong drones seen on 15 December at the Harar Meda airbase

Na utafiti wa data ya ndege unaonyesha safari 119 za mizigo katika kipindi cha miezi mitano mwaka jana kutoka viwanja vya ndege vya kijeshi vya UAE hadi kituo cha anga cha Harar Meda (kusini-mashariki mwa Addis Ababa) na Bole, uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu. Hakuna uhakika safari hizi za ndege zilibeba nini.

Unaweza pia kusoma:

Ethiopia inasema nini?

Msemaji wa serikali ya Ethiopia Legesse Tulu hakutaka kueleza kwa undani matukio hayo hapo juu.

Aliiambia BBC: "Sitasema wapi, lakini serikali imezitumia [ndege zisizo na rubani] katika nyakati fulani na maeneo tofauti." Pia alisisitiza kuwa hazikutumiwa dhidi ya raia.

BBC iliwasiliana na serikali zinazohusika kuhusu ripoti kwamba ndege zisizo na rubani kutoka nchi zao zimetumiwa nchini Ethiopia lakini hazijajibu.

Pia kampuni ya ulinzi ya Uturuki inayotengeneza ndege isiyo na rubani ya Bayraktar iliombwa kuzungumzia suala hilo, lakini haijasema lolote

Hakuna vikwazo vya silaha dhidi ya Ethiopia kwa sasa, na uuzaji nje wa ndege zisizo na rubani haujawekwa wazi kwa kuzingatia kanuni na mikataba ya kimataifa.

Lakini matumizi yao katika maeneo yenye migogoro duniani kote yanaonekana kuongezeka.