Ndovu azaa mapacha katika tukio nadra Kenya

Iliyochapishwa

Mapacha wawili wa ndovu wamezaliwa wiki hii katika tukio la nadra lililotokea katika hifadhi ya kitaifa iliyopo kaskazini mwa Kenya.

Mapacha hao wa kike na wa kiume waligunduliwa kwa mara ya kwanza na muongozaji wa watalii aliyekuwa akisafiri katika hifadhi ya wanyamapori ya Samburu mwishoni mwa juma.

Mapacha hao ni mapacha wa pili wa ndovu kuwahi kugunduliwa na shirika la uhifadhi wa wanyamapori linalotoa msaada kuhifadhi ndovu nchini Kenya la Save the Elephants.

Shirika hilo linasema idadi ya ndovu mapacha ni 1% tu ya ndovu wanaozaliwa, huku tukio la mwisho la uzazi wa mwisho wa mapacha unaofahamika ukirekodiwa mwaka 2006.

Akizungumza na Shirika la habari la Reuters , muasisi wa shirika hilo Dkt Iain Douglas-Hamilton alisema ni kipindi kigumu kwa watoto hao wa ndovu kwani mapacha wa mwisho walizaliwa miaka 15 iliyopita hawakuweza kuishi muda mrefu baada ya kuzaliwa.

Mara nyingi mama huwa hana maziwa ya kutosha kuwalisha mapacha wote wawili, aliongeza, akisema kuwa kila mtu " amekuwa akiwaotakia kunusurika".

Ndovu wa Afrika wana kipindi huwa na kipindi kirefu cha ujauzito kuliko mnyama mwingine yoyote yule. Hubeba mimba kwa karibu miezi 22, na huzaa kila baada ya takriban miaka minne.

Bishara ya pembe za ndovu na kupotea kwa mazi muhimu kumesababisha kuwekwa kwa ndovu katika orodha nyekundu ya Muungano wa kimataifa uhifadhi wa viumbe asilia-(International Union for the Conservation of Nature) ya spishi waliomo hatarini.

Unaweza pia kusoma:

Hatahivyo idadi ya ndovu imeongezeka nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni, kulingana sensa ya kwanza ya taifa hilo ya wanyamapori, iliyochapishwa mwaka jana.

Unaweza pia kutazama: