Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndovu 9 wauawa na umeme nchini Botswana
Ndovu tisa wameuawa kwa kupiwa na umeme kati kati mwa Botswana baada ya kuangusha nyaya za umeme walipojaribu kunywa maji kutoka na bomba lililokuwa likivuja, kwa mujibu wa shirika la Reuters.
Ndovu hao wate walikuwa wanajaribu kulifikia bomba hilo linalopeleka maji katika kijiji cha Dukwi wakati ajali hiyo ilitokea, mkurugenzi wa shirika la wanyama pori Otisitswe Tiroyamodimo alisema.
"Bado uchunguzi unaendelea, lakini tumegundua kuwa ndovu hao walikuwa wakijaribu kunywa maji kutoka kwa bomba lililokuwa likivuja."
Kuna kati ya ndovu 150,000 na 200,000 nchini Botswana,