Tsunami yaikumba Tonga baada ya mlipuko mkubwa wa volcano

Maelezo ya video, Tazama: picha za Satellite zilizonaswa mara baaada ya mlipuko wa volcano Hunga Tonga-Hunga Ha'apai
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mawimbi ya Tsunami yaliyosababishwa na mlipuko mkubwa wa volkano chini ya maji yameikumba nchi ya Pasifiki ya Tonga.

Picha za mitandao ya kijamii zilionyesha maji yakipita kwa kasi eneo la kanisani na nyumba kadhaa, na walioshuhudia walisema majivu yalikuwa yakianguka kwenye mji mkuu, Nuku'alofa.

Tahadhari ya tsunami iliyotolewa iliwafanya wakazi kukimbilia maeneo ya miinuko.

Mlipuko wa volcano ya Hunga Tonga-Hunga Haʻapai ulisikika Pasifiki ya Kusini, ikiripotiwa hadi New Zealand na Australia.

Mji mkuu wa Tonga uko kilomita 65 kasakazini ya eneo lililokumwa na mlipuko wa volcano, kwenye kisiwa kikuu cha Tongatapu nchini humo.

Mkazi mmoja, Mere Taufa, alisema mlipuko huo ulitokea wakati familia yake ilikuwa ikijiandaa kwa chakula cha jioni, na mdogo wake alidhani ni mabomu yalikuwa yanalipuka karibu.

"Kitu cha kwanza kilichonijia akilini ni kujificha chini ya meza, Nilimchukua dadangu mdogo na kuwaomba wazazi wangu na watu wengine nyumbani kufanya hivyo," New Zealand tovuti ya habari Stuff.co.nz ilimnukuu akisema.

Bi Taufa anasema alishtukia, maji yalikuwa yakiingia nyumbani kwao.

"Ungesikia mayowe kila mahali, watu wakipiga kelele huku wakikimbilia usalama, ili mradi mtu afike mahali pa juu," aliongeza.

Mabomba ya gesi, moshi na majivu yanayomiminika kutoka kwenye volcano yalifikia kilomita 20 angani, Huduma za Jiolojia za Tonga zilisema.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

1px transparent line

Wenyeji walisema mlipuko huo ulisikika kama ngurumo ya radi, ikifuatiwa na anga giza huku mawingu ya volkeno yakianza "kunyesha majivu na kokoto ndogo".

Maeneo mengi ya Tonga yanakabiliwa na uhaba wa umeme, huku huduma za simu na intaneti zikikatizwa, Kumaanisha mawasiliano yalikatizwa. Lakini video kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha msongamano mkubwa wa magari huku watu wakijaribu kukimbilia maeneo ya juu kwa gari.

Vanuatu, taifa lingine la kisiwa cha Pasifiki, lilitoa onyo kama hilo.

Prof Shane Cronin, mtaalamu wa volkano katika Chuo Kikuu cha Auckland, alisema mlipuko huo ulikuwa moja ya milipuko mikubwa zaidi nchini Tonga katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

"Hili ni tukio kubwa sana - ni mojawapo ya milipuko muhimu zaidi ya muongo uliopita angalau," aliiambia BBC. "Hili ni tukio kubwa sana - ni mojawapo ya milipuko muhimu zaidi ya muongo uliopita angalau," aliiambia BBC.

A map shows location of Tonga in the South Pacific, and a close-up shows the vast plume of ash and steam seen from a satellite

Chanzo cha picha, EPA

1px transparent line