Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mlaji wa nyama za watu ahukumiwa kwa kumuua mwanaume mwenzake aliyemlaghai kimapenzi
i
Mahakama ya Ujerumani imemuhukumu mwalimu wa zamani kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya mwanaume aliyekutana naye katika wavuti wa mtandao wa kutafuta wapenzi na kuula mwili wake kuunajisi mwili wake.
Jaji mjini Berlin alisema Stefan R, mwenye umri wa miaka 42, alimuua mhandisi wa umeme kwa ajili ya "kukidhi kiu yake ya kula nyama ya mtu".
Mwalimu huyo wa zamani alikamatwa Novemba wakati baadhi ya mifupa ya muathiriwa ilipogunduliwa na watu ikiwa imetupwa katika bustani kaskazini mwa Berlin.
Mama yake muathiriwa huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa ameripoti kuwa kijana wake alikuwa amepotea wiki kadhaa kabla.
Wanaume hao wawili walikuwa wamepanga kukutana kwa ajili ya kufanya tendo la ngono katika makazi ya Stefan R yaliyoko katika wilaya ya Pankow, ambako muuaji alikuwa akifundisha hisabati katika shule ya kibinafsi . Vyombo vya habari vya Berlin vilisema alikuwa amejiita CanOpener79 kwenye ukumbi wa kutafuta wapenzi.
Muuaji huyo awali alitembelea mtandao wa mazungumzo chatrooms ambapo watu walijadili ulaji wa nyama ya watu. Wapelelezi walisema muathiriwa wake alikufa saa kadhaa baada ya kukutana na walipata mfupa na kisu cha machinjioni wakati walipokuwa wakifanya msako kwenye makazi yake.
Wakati wa kesi yake Stefan R aliiambia mahakama alimpata mwanaume huyo akiwa amekufa sebuleni kwake asubuhi baada ya kufanya ngono na kutokana na wasi wasi aliokuwa nao akaamua kutupa mwili wake.
Vipande vya mwili wake vilipatikana na wahudumu wa bustani ya jiji mwezi Novemba 2020.
Alitumia gari la kukodishwa kutupa vipande vya mwili katika maeneo kadhaa ya kaskazini mwa wilaya ya Pankow.Ni viungo vya jinsia tu vya muathiriwa vilivyopotea.
''Matamanio ya ngono au matamanio ya kuchinja sio uhalifu ," wakili wake aliiambia mahakama, akitoa wito wa kuondolewa makosa na kuachiliwa.Walidai mhandisi huenda aliuliwa na mchanganyiko wa madawa ya kulevya aliyokuwa ameyanywa.
Unaweza pia kusoma:
Lakini waendesha mashitaka walisema kigezo cha mauaji kimepatikana, kiasi kwamba muathiriwa alilaghaiwa kuingia katika mtego na muuaji alifanya hivyo kukidhi kiu yake ya ngono na kumuwezesha kutekeleza uhalifu zaidi.