Forbes: Rais Samia na aliyekuwa mke wa Jeff Bezos, Mackenzie Scott miongoni mwa wanawake 100 wenye uwezo mkubwa duniani

Rais Samia Suluhu Hassan

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa wanawake wenye ushawishi mkubwa walioorodheshwa katika orodha ya jarida la Forbes la wanawake wenye uwezo mkubwa duniani 2021.

Suluhu ambaye alimrithi mtangaluzi wake hayati John Pombe Magufuli mapema mwaka huu ameshirikishwa katika orodha hiyo ambayo pia inamuweka aliyekuwa mke wa mtu Tajiri zaidi duniani Jeff Bezos, Mackenzie Scott kuwa katika nafasi ya kwanza .

Scott ambaye alitalakiana na bilionea Jeff Bezos na kuolewa na mwalimu ndiye mwanamke wa tatu Tajiri zaidi duniani.

Hatua yake ya kutoa fedha anazomiliki kwa shghuli za ufadhili ndio liomuwezesha kuorodheshwa katika nafasi hiyo.

Bilionea MacKenzie Scott, ameolewa na mwalimu wa sayansi katika shule ya watoto wake .

Taarifa ya kuolewa kwake na Dan Jewett ilifichuliwa kupitia tovuti ya kutoa misaada.

Bi Scott, ambaye thamani ya utajiri wake ni karibu dola bilioni 53 kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Forbes, amesema nia yake ni kutoa sehemu kubwa ya mali hiyo.

Mackenzie - aliyekuwa mke wa Jeff Bezos

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mackenzie - aliyekuwa mke wa Jeff Bezos

Kwa upande wake Rais Samia ambaye yuko katika nafasi ya 94 amejipatia sifa kwa kufuata maagizo ya corona na kuyaidhinisha nchini Tanzania.

Sifa moja kubwa ambayo watu waliowahi kufanya naye kazi wanaisema na ambayo si watu wengi wa nje wanaifahamu ni uwezo wake mkubwa wa kiuongozi.

Kwa mfano mbunge wa jimbo la Bumbuli (CCM), January Makamba, anasema Samia ni miongoni mwa wanasiasa wenye uwezo mkubwa aliowahi kufanya kazi nao na ni bahati mbaya tu kwamba wengi wa Watanzania hawajapata fursa ya kuliona hilo.

Makamba alifanya kazi kwa karibu na mama Samia katika kipindi cha kati ya mwaka 2015 hadi 2020 wakati akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - ambapo alikuwa akiripoti kwa mama huyo moja kwa moja.

Kulingana na muhariri wa jarida la Forbes, Maggie McGrath , wanawake hao hawamiliki pesa au nafasi za madaraka tu , Mtu ni sharti awe anatumia fedha, alizonazo , sauti yake au majukwaa ya umaa kuimarisha jamii.

''Haitoshi tu kuwa na pesa, au nafasi ya madaraka. Mtu ni sharti awe anatumia fedha, alizonazo , sauti yake au majukwaa ya umaa kuwawezesha raia''.

Mwanamke aliyeshikilia nafasi ya pili katika orodha hiyo ni makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris ambaye amepanda juu nafasi moja na kumpiku Christine Lagarde - rais wa Benki kuu ya Ulaya ambaye yuko katika nafasi ya tatu.

Kwa mujibu wa muhariri wa Forbes orodha hiyo ya 18 ambayo hutolewa kila mwaka ya wanawake 100 wenye uwezo mkubwa duniani, inatoka kutoka mataifa 30 na inaangazia wanawake wanaofanya kazi katika idara za fedha teknolojia, siasa , uvumbuzi, burudani na zaidi, wote wakiwa na lengo moja.

Orodha hiyo pia inamshirikisha rais wa Taiwan Tsai Ing-wen , ambaye matamshi yake ya kupigania uhuru na demokrasia mbele ya shinikizo kuu kutoka China yamemuweka katika nafasi ya 28.

Mfahamu Rais Samia Suluhu Hassan kwa ufupi

Mama Samia aliolewa na mumewe, Hafidh Ameir, mnamo mwaka 1978 na katika ndoa yao wamejaliwa kupata watoto wanne.

Mtoto wake maarufu zaidi - Wanu, ni mbunge wa bunge Tanzania.

Samia ni msomi wa kiwango cha shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza na ni mhitimu pia wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alikosomea masuala ya utawala.

Aliajiriwa kama mchapishaji katika serikali ya Zanzibar mwaka 1977 na akapanda ngazi hadi kuwa afisa wa mipango serikalini kati ya 1987 na 1988.

Alihudumu pia kama meneja wa mradi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Zanzibar kati ya 1985 na 1997, na pia kama meneja mkurugenzi wa Mwamvuli wa NGO 1998 hadi 1999.

Alichukua wadhfa wa kuwa makamu wa rais wa Tanzania , jukumu ambalo alichaguliwa mara ya kwanza 2015.

Mnamo mwezi Septemba , alikuwa mwanamke wa tano rais kutoka Afrika kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Alitumia hotuba hiyo kukosoa ukosefu wa usawa katika usambazaji wa chanjo za corona kulingana na jarida la forbes.

Orodha kamili ya wanawake 100 wenye uwezo mkubwa duniani

1 MacKenzie Marekani

#2Kamala Harris Marekani

#3Christine Lagarde Ufaransa

#4Mary Barra Marekani

#5Melinda French Marekani

#6Abigail Johnson Marekani

#7Ana Patricia Botín Uhispania

#8Ursula von der Leyen Ujerumani

#9Tsai Ing-wen Taiwan

#10Julie Sweet Marekani

#11Karen Lynch Marekani

#12Carol Tom Marekani

#13Emma Walmsley Uingereza

#14Jane Fraser54 Marekani

#15Nancy Pelosi Marekani

#16Gail Boudreaux Marekani

#17Rosalind Brewer Marekani

#18Susan Wojcicki Marekani

#19Safra Catz Marekani

#20Ruth Porat Marekani

#21Martina Merz Ujerumani

#22Kristalina Georgieva Bulgaria

#23Oprah Winfrey Marekani

#24Shemara Wikramanayak Australia

#25Judith McKenna Uingereza

#26Amanda Blanc54United KingdomBusiness

#27Nicke Widyawati53IndonesiaBusiness

#28Amy Hood49United StatesTechnology

#29Catherine MacGregor-FranceBusiness

#30Phebe Novakovic63United StatesBusiness

#31Shari Redstone67United StatesMedia & Entertainment

#32Laurene Powell Jobs58United StatesPhilanthropy

#33Ho Ching68SingaporeFinance

#34Jacinda Ardern41New ZealandPolitics & Policy

#35Jessica Uhl53United StatesBusiness

#36Sheryl Sandberg52United StatesTechnology

#37Nirmala Sitharaman62IndiaPolitics & Policy

#38Gwynne Shotwell58United StatesTechnology

#39Janet Yellen75United States-

#40Kathy Warden-United StatesBusiness

#41Adena Friedman52United StatesFinance

#42Marianne Lake Jennifer Piepszak-United StatesFinance

#43Sheikh Hasina Wajed74BangladeshPolitics & Policy

#44Gina Rinehart67AustraliaBusiness

#45Thasunda Brown Duckett-United StatesFinance

#46Vicki Hollub61United StatesBusiness

#47Mary Callahan Erdoes54United StatesFinance

#48Ozlem Tureci-GermanyBusiness

#49Lisa Su52United StatesBusiness

#50Dana Walden57United StatesMedia & Entertainment

#51Tricia Griffith57United StatesBusiness

#52Roshni Nadar Malhotra40IndiaTechnology

#53Cathie Wood66United StatesFinance

#54Jennifer Salke-United StatesMedia & Entertainment

#55Tokiko Shimizu56Japan-

#56Donna Langley53United KingdomMedia & Entertainment

#57Hana Al Rostamani--Finance

#58Dong Mingzhu67ChinaBusiness

#59Yuriko Koike69JapanPolitics & Policy

#60Elvira Nabiullina58RussiaPolitics & Policy

#61Suzanne Scott-United StatesMedia & Entertainment

#62Lynn Good-United StatesBusiness

#63Ann Sarnoff-United StatesMedia & Entertainment

#64Judy Faulkner78United StatesBusiness

#65Melanie Kreis50GermanyBusiness

#66Sri Mulyani Indrawati59IndonesiaPolitics & Policy

#67Paula Santilli-MexicoBusiness

#68Rihanna33BarbadosMedia & Entertainment

#69Laura Cha-Hong KongFinance

#70Queen Elizabeth II95United KingdomPolitics & Policy

#71Mette Frederiksen44DenmarkPolitics & Policy

#72Kiran Mazumdar-Shaw68IndiaBusiness

#73Joey Wat50ChinaBusiness

#74Reese Witherspoon45United StatesMedia & Entertainment

#75Wang Feng Ying-ChinaBusiness

#76Beyoncé Knowles40United StatesMedia & Entertainment

#77Güler Sabanci66TurkeyBusiness