Josephine Baker: Maisha yasiyo ya kawaida ya mcheza densi na jasusi atakayetuzwa na Ufaransa

Josephine Baker

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Novemba 30, Josephine Baker atatuzwa kwa makumbusho na sanamu eneo la Pantheon mjini Paris, mahala ambapo tamaduni zinazoheshimiwa za kifaransa zipo kuanzia za Voltaire na Victor Hugo, hadi Marie Curie na Jean-Jacques Rousseau.

Baker atakuwa mwanamke wa sita kupata tuzo hiyo na mwanamke pekee mweusi.

Mcheza densi huyo wa kigeni, mwenye asili ya Marekani na maarufu kwa ngoma za utupu, alikuwa mmoja wa karibu watu 80 walioheshimiwa sana nchini Ufaransa?

Ukweli ni kwamba, Josephine MacDonald - jina lake la asili - hakuja kuwa mtu maarufu tu katika nusu ya kwanza ya karne ya ishirini.

Bali kidosho huyu alipewa jina la utani "Bronze Venus", akawa shujaa kwenye vita vya pili vya dunia na baadaye mtetezi wa haki.

Katika safari yake, Baker alivunja vizuizi vyote vya kila namna kuanzia vya kitamaduni hadi vya kibaguzi.

Kutoka kwa umaskini hadi kuwa nyota

Alizaliwa St Lois, Missouri Juni 3 1906 na alikabiliwa na changamoto si haba utotoni mwake. Baba yake aliyekuwa mcheza ngoma kwenye baa za honky-tonk, aliitelekeza familia, na mama yake ambaye alikuwa nusu mweusi na nusu Mmarekani alifanya kazi ya kuosha ili kuwalea watoto wake.

Josephine alianza kufanya kazi akiwa na umri wa miaka 8 na kukabiliwa na dhuluma. Akiwa na umri wa mika 14 alikuwa tayari ameolewa na kutengana mara mbili na ilikuwa ni kutoka kwa mume wake wa pili ambapo alikuja kupata jina Baker.

Akiwa mdogo alikuwa maskini sana kiwango cha kuishi mitaani na alitegemea taka kupata chakula.

Wakati mmoja alisema alianza kucheza ngoma ili apate joto la mwili kwenye mitaa ya St. Louis.

Josephine Baker

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Josephine Baker alianza kazi yake kwa kucheza densi.

Lakini kipawa chake na haiba limwezesha kujiunga na kikundi cha vaudeville na baadaye kampuni ya densi, The Dixie Stepper, ambapo mwaka 1919 ilichangia ahamie New York.

Ni mjini New York ndipo aligunduliwa na muajiri aliyekuwa akitafuta wasanii kecheza kwenye tamasha moja la jarida ya kwanza kuandaliwa kwa watu weusi mjini Paris.

Kwa ahadi ya dola 1,000 kwa mwezi, Baker alisafiri kwenda Ufaransa ambapo maisha yake yalibadilika milele.

"Ngoma ya ndizi"

Hatua kubwa ya kupata umaarufu alipiga mwezi Aprili mwaka 1926, ambapo akiwa na miaka 19, alicheza katika tamasha la Folies Bergère.

Pale alipowatumbuiza kwa ngoma tofauti kuliko ile iliyozoelewa na wakazi wa Paris ya Danse Sauvage.

Baker, akiwa amevaa lulu tu, sidiria na sketi iliyokuwa imetengenezwa kutokana na ndizi na mawe ya kumetameta, alishangaza kila mtu kwa densi yake.

Usiku wa ufunguzi wake umati ulishangilia mara 12.

Josephine Baker alivyotumbuiza kwa "densi ya ndizi"

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Josephine Baker aliwatumbuiza wakazi kwa "densi ya ndizi"

Ngoma ya ndizi ikamfanya nyota na kuwa mwanzo wa umaarufu wake nchini Ufaransa kama "Bronze Venus."

Hakupata tu kuigiza na kucheza ngoma katika ukumbi wa michezo, alishirikia pia kwenye filamu nne: : "Mermaid of the Tropics" (1927), ZouZou (1934), Princesse Tam Tam (1935) and Fausse Alerte (1940), kitu ambacho si cha kawada kwa msanii mweusi.

Kama mwanamke mweusi, hangeweza kutimiza kile alichofanya kama angeishi nchini Marekani, kulingana na Bennetta Jules-Rosette, mkurgenzi wa kituo ch utafiaia kwa masomo ya Afrika na Marekani chuo cha California na mwandishi wa wasifu wake, aliimbia BBC.

Kulingana na mwandishi huyo wa wasifu, kile kilichomtofautisha Baker ni kwamba hakufikiria kuwa kulikuwa na jambo lisilowezekana.

Ujasiri

Baker hakuwa tu jarisi jukwani. Yalikuwa pia maisha yake ya siri.

Wengi wanamkumbuka kidosho huyo, aliyekuja kuwa nyota wa mitindo akitembea mitaa ya mji mkuu wa ufaransa akiandamana na kipenzi asiye wa kawaida: duma.

Josephine Baker con su chita

Chanzo cha picha, Getty Images

Msanii huyo akasisitiza kuwa tamasha zke ziwe wasi kwa watazamaji wa kila aina na wakatai akifanya ziara zake nchini Marekani alikataa kucheza kwenye tamasha ambazo ziliwazuia watu weusi.

Kulingana na Jules-Rosette alikuwa wa kwanza kuvunja ubaguzi wa rangi huko Las Vegas, hata kabla ya wasanii kama Frank Sinatra na Sammy Davis Jr.

Lakini hata umaarufu wake haukumkinga kutokana na ubaguzi wa rangi nchini mwake: baadhi ya hoteli na migahawa ilikataa kumpokea na mwaka 1951 alijumuishwa kwenye orodha ya watu wasiopendwa na idara ya ujasusi FBI kwa kupinga ubaguzi dhidi ya mmliki wa klabu ya Stork mjini New York.

Jasusi wa upinzani

Wakati vita vya pili vya dunia vilizuka (1939-1945) Baker aliweka kando taaluma yake ya uigizaji na mitindo iliyomfanya kupata umaarufu kufanya kitu mastaa wachache na wanamitindo wanaweza kufanya, alivaa sare.

Josephine Baker en 1945 vestida con su uniforme militar

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati wa mzozo huo wa muda mrefu, alihudumu kama luteni wa cheo cha pili kwenye jeshi la wanahewa la ufaransa.

Kwa ujasiri tena, alitumia uaamrufu wake kuwafanyiaa ujasusi washirika.

Kwa kutumia mawasiliano yake, na mialiko kwenda kwa tamasha za balozi alipata habari kuhusu mienendo ya wanajeshi adui na kwanza kutuma bahari hizo kwa jeshi la Ufaransa

Kupinga ubaguzi wa rangi

Upande mwingine unaosherehekewa kuhusu Baker ni ule wa kupigania haki za raia.

Mwaka 1963 baada ya kurejea nchini Marekani kwa msaada wa aliyekuwa mwanasheria mkuu wakati huo Jenerali Robert Kennedy alishiriki kwenye maandamano maarufu mjini Washington, akiandamana na kiongozi wa vuguvugu la kupigania haki Martin Luther King, ambaye alitoa hotuba yake maarufu, "Nina ndoto".

Akiwa amevaa sare ya jeshi la ufaransa, Baker alikuwa mwanamke pekee aliyehutubia umati.

"Mnaju kawadia nimetembea barabara yenye mawe," aliuambia umati.

"Sikutembea ile rahisi, Lakini vile ninazidi kukua, na kufahamu kuwa nina nguvu, nimechkua barabara yenye mawe na kujaribu kuilainisha kidogo," alisema.

Josephine Baker en 1961 vestida con su uniforme militar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baker alitoa hotuba wakati wa maandamano ya kihistoria ya Washington kwa Haki za Kiraia mnamo 1963.

"Nilitaka kufanya mambo rahisi kwenu. Ninataka muwe na fursa na muwe na nilichokipata," alisema, akimaanisha mafanikio aliyoyapata nchini Ufaransa.

Baker hakuzungumza tu na kuchukua hatua kupinga ubaguzi wa rangi na ubaguzi wa kidini. Pia alikuwa mfano: mwaka 1937 alibadili dini kuwa myahudi kumuoa mfanyabiashara Jean Lion,ambaye kupitia kwake aliweza kupata uraia wa ufaransa.

Ndoa hiyo ilidumu kipindi cha mwaka mmoja. Miaka kumi baadaye alimuoa mwanamume mwingine mzungu: Joe Bouillon, ambaye naye waliwapanga watoto 9 kutoka nchi tofauti na rangi kuunda alichokiita Kabila la Upinde wa Mvua

Hata baada ya kumtaliki Bouillon mwaka 1957, aliongeza watoto wengine watatu kwa kabila lake ambao aliweza kuwalea peke yake.

Msanii huyu ambaye alikuja kuwa mwanamke mweusi tajiri zaidi duniani, aliishia kufilisika na kutumia miaka yake ya mwisho huko Monacho kwa msaada wa nyota mwingine mmarekani Grace Kelly, aliyekuwa binti mfalme wa taifa hilo dogo la ulaya.

Grace Kelly na Prince Raniero wanamkaribisha Josephine Baker na watoto wao Monaco mnamo 1969.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Grace Kelly na Prince Raniero wanamkaribisha Josephine Baker na watoto wao Monaco mnamo 1969.

Alipofariki dunia mwaka 1975 kutona na kuharusi, alizikwa kwenye manispaa hiyo lakini alipata tuzo za kijeshi wakati wa mazishi yake nchini ufaransa.

línea