Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ahmaud Arbery: Wazungu watatu wapatikana na hatia ya mauaji ya mtu mweusi aliyekuwa mazoezini
Wanaume watatu wamepatikana na hatia ya kumuua mtu mweusi aliyekuwa akijfanya mazoezi kukimbia mwaka jana katika kesi ambayo iligeuka kuwa kilio cha kudai haki ya rangi ya waandamanaji.
Ahmaud Arbery, mwenye umri wa miaka 25 alipigwa risasi na kuuawa Februari 2020 katika makabiliano na Travis na Gregory McMichael na jirani wake, William Bryan.
Wanaume hao walijitetea kwa kusema kuwa walichukua hatua ya kumpiga risasi katika kujilinda , lakini waendesha mashitaka walisema rangi ilikuwa ni sababu ya kumpiga risasa.
Wanaume hao sasa wanakabiliwa na hukumu za kifungo cha maisha jela.
Jopo la mahakama lililoundwa na jumla ya wazungu 12 liliketi kutathmini kesi hiyo kwa saa 10 kabla ya kurejea kutoa hukumu takriban saa sita za mchana Jumatano.
Watatu hao walipatikana na hatia ya mauaji, kufanya shambulio kali, kusema uongo na kuazimia kutekeleza uhalifu kwa makusudi .
Mwezi Februari wanaume hao watatu watakabiliwa na mashitaka mengine katika kesi ya mahakama ya shirikisho kuhusiana na uhalifu wa chuki , kwa madai kuwa walimlenga Arbery kwasababu alikuwa mtu mweusi.
Ahmaud Arbery alikufa vipi?
Arbery alikuwa nje akifanya mazoezi ya kukimbia majira ya mchana viungani mwa mji wa mwambao wa Brunswick katika jimbo la Georgia.
Mzee McMichael, ambaye ni mkazi wa eneo hilo, aliiambia polisi kuwa Arbery alifanana na mshukiwa katika msururu wa visa vya wizi katika kitongoji cha kijamii cha pwani ya Satilla .
Polisi wamesema hakuna ripoti iliyowasilishwa kwao kuhusu wizi huo, na hakuna mali yoyote iliyopatikana katika mali za Arbery.
Wawili hao walijihami kwa piston na bunduki kubwa na kumfuata Arbery, ambaye hakuwa na silaha, wakiwa ndani ya gari aina ya lori la pickup truck na kumfuata katika eneo lake. Baadaye Bryan alijiunga na msafara huo.
Jopo la mahakama lilisikiliza simu iliyopigwa kwa nambari ya polisi 911 ambapo mzee McMichael alimwambia mpokeaji wa siku: "Niko nje hapa katika pwani ya I'm Satilla. Kuna mwanaume mweusi ambaye anakimbia nje mtaani."
McMichael mdogo alitoa ushahidi wakati wa kesi kwamba alijaribu kuzungumza na Arbery wakati wawili hao walipokuwa bado ndani ya lori na Arbery hakumjibu.
Alishuka kutoka ndani ya lori na kumfyatulia risasi Arbery wakati wa mapambano. Travis McMichael alidai kujilinda, akisema kuwa Arbery alimpokonya bunduki yake. Bunduki tatu zilifyatuliwa.
Uchunguzi wa mwili ulionyesha Arbery alikuwa na majeraha mawili ya risasi kifuani mwake pamoja na na jereha kubwa ndani ya mkono wake mmoja.
Gregory McMichael, 65, na mwanaye wa kiume Travis, 35, na jirani yao William "Roddie" Bryan, 52, walikamatwa mwezi Mei, 2020
Waendesha mashitaka walidai kuwa Travis McMichael alitumia maneno ya ubaguzi wa rangi na matusi dhidi ya Arbery alipokuwa amelala chini . Wanaume hao watatu walikana kuwa wabaguzi wa rangi.
Jinsi rangi ilivyohusika katika kesi hii
Katika mashitaka yao, waendesha mashitaka huenda walichagua kutozungumzia ukweli kwamba Ahmaud Arbery alikuwa ni mtu mweusi na wauaji walikuwa ni wazungu, lakini sio vigumu kuona ni kwanini mauaji haya yamekuwa yakiangaliwa na wengi kwa mtizamo wa rangi.
Wazazi wa Arbery walikuwa wamekasirishwa na jinsi mawakili wa utetezi walivyomuelezea mtoto wao wa kiume kama mtu ambaye alikuwa mwenye makosa kwa kuwakimbia watu wenye silaha wasio wajua na kwa kugeuka na kujaribu kupigania maisha yake wakati walipomzingira.
Ukweli kwamba wanaume hawa walimuona Arbery kama tisho, ingawa hawakuwa na Ushahidi kwamba alifanya chochote kinyume cha sheria, kiasi kwamba walihisi walikuwa na haki ya kujihami na kumfukuza; kwamba wakati maafisa wa polisi walipowasili eneo la tukio waliwaliwaza wauaji, na sio kumshugulikia mara moja kijana ambaye alikuwa amelala amejikunja ardhini; ukweli kwamba hakuna yeyote aliyekamatwa kwa zaidi ya wiki 10 na ni baada ya video ya mauaji kusambazwa sana, yote haya yanaonekana kwa waangalizi wengi kama mabaki ya ukatili wa kipindi kilichopita.
'Tumelishinda kundi la wauaji'
Nje ya mahakama Jumatano makumi ya watu, baadhi yao wakionyesha ishara za kampeni ya Black Lives Matter ,walishangilia wakati hukumu zilipokuwa zikisomwa.
Baba yake Arbery, Marcus Arbery, alionekana akilia na kuwakumbatia waliomuunga mkono.
"Hakufanya lolote," baba yake alisema, "bali alikimbia na kuota ndoto za maisha yake." Aliwaambia watu waliofika kumuunga mkono: "Tumelishinda kundi la wauaji''
Mama yake Arbery, Wanda Cooper-Jones, aliushukuru umati wa watu na kusema hakudhani angeiona siku hii.
"Yamekuwa ni mapambano marefu. Yamekuwa ni mapambano magumu. Lakini Mungu ni mwema," alisema. Kuhusu mwanae wa kiume, alisema: "Sasa atapumzika kwa amani."
Arbery alikuwa amesajirlwa katika chuo cha ufundi kusomea masomo ya ufundi wa umeme wakati alipouawa.
Ni picha gani za video zilikuwa muhimu?
Video ilikuwa kiini cha kesi hii.
Kipande cha kwanza cha video kilikuwa cha sekunde 36 ambacho kilichukuliwa kwa simu ya mkononi kilichoonyesha kifo cha Arbery.
Kipande hicho kilichukuliwa na William Bryan, ambaye alikuwa ndani ya gari iliyomfuata Arbery, na video hii ilisambazwa kwa umma kwa mara ya kwanza tarehe 5 Mei 2020.
Kipande hicho kinaonyesha Arbery akijaribu kuipita lori ya pickup truck iliyokuwa mbele yake barabarani na baadaye akionekana kuhangaika na Travis McMichael. Kuna kelele za kunyamazishwa na risasi mbili zinasikika.
Mzee McMichael anaonekana akiwa amesimama upande wa nyuma wa pickup huku wawili hao wakilumbana.
Video hiyo iliibua hasira na ilifuatiwa mara moja na mashitaka ya uhalifu.
Siku tano baadaye picha kutoka kwa kamera za ukaguzi zilionekana, zikionyesha mwanaume mweusi aliyevaa fulana nyeupe-anayeaminiwa kuwa Arbery - katika eneo la ujenzi wa nyumba muda mfupi kabla ya ufyatuaji wa risasi.
Anaonekana akitembea kwenye eneo la ujenzi na kulitazama kwa muda kabla ya kuanza kufanya mazoezi ya kukimbia kwenye mtaa.
Wakati wa kesi, mmiliki wa eneo hilo la ujenzi, Larry English Jr, alitoa Ushahidi kuwa mwanaume huyo aliyeonekana kwenye eneo hilo hakusumbua wala kuharibu mali yake alipotembelea eneo hilo.
Bw English alisema kuwa kamera iliwanasa watu wengine-ikiwa ni pamoja na watoto na wenza wazungu- wakipita kwenye mali zake, lakini hakuwahi kutoa idhini akina McMichael kuingia kwenye eneo la jengo lake kuzozana na mtu yeyote.
Jopo la mahakama pia lilionyeshwa picha za kamera za mwili ya polisi iliyochukuliwa baada ya tukio hilo la mauaji.