Kuanzia makazi ya kibinafsi hadi kasri za umma- Ufahamu mji mzima wa Ujerumani uliojengwa kwa almasi

Iliyochapishwa

Wakazi wa kwanza katika mji wa wa Ujerumani wa Nordlingen wanadhaniwa kuishi katika eneo la shimo lililotokana na volkano. Lakini mandhari ya kipekee ya eneo lenyewe ilikuwa tofauti kabisa.

Unapopanda ngazi za mnara wa Kanisa la Gothic lililopo mjini humo, unaweza kuona ngazi zinazomelemeta kutokana na miale inayofifia ya jua . Na baada ya hapo utaona miale hiyo ikigeuka na kuwa ya rangi ya jivu jeusi.

"Sababu ni kwamba eneo lote la kanisa hili limetengenezwa kwa mawe ya Suez , na mawe haya yana chembechembe za almasi," anaeleza mlinzi wa kasri Horst Lenner.

"Kwa bahati mbaya chembechembe hizi ni ndogo sana. Viginevyo, wangekuwa wameibomoa zamani," aliongeza huku akitabasamu.

Kuna ukweli katika maneno ya Lener. Wakati wa ujenzi wa mji huu, wakazi walifahamu kuwa mawe wanayotumia yamejaa mamilioni ya almasi ndogo. Tunazungumzia kuhusu karne ya 9. Kiasi hiki cha almasi hakijawhi kupatikana kwingine kokote duniani.

Kuanzia juu ya kasri, ukiangalia mji huu uliopo katika jiji la Bavaria, huwezi kukosa kuhisi uwepo wa eneo hili. Miamba inayozingira jua(Asteroid ) ambayo ilianguka zama za kale kwenye eneo hili yapata miaka milioni 15 iliyopita iliugeuza mji wa Nordlingen kuwa mji wa almasi nchini Ujerumani.

Miamba ambayo ilikadiriwa kusafiri kwa kasi ya kilomita 25 kwa sekunde, iligonga ardhini na kutengeneza shimo lenye upana wa kilomita 26, ambako mji huu sasa unapatikana.

Lilitengenezwa povu la kaboni kutokana na viwango vya juu joto na shinikizo, na mara moja zikatengenezwa chembechembe za almasi zenye ukubwa wa milimita 0.2 ambazo hakuna binadamu anayeweza kuziona kwa macho yake.

Bila kujua mfereji wa Suez ambao umefunikwa na almasi watu wamejenga mji uliojaa mawe ya thamani na kuufanya mji wa Nördlingen kuwa eneo la kipekee duniani.

"Majengo yote katika mji huo yalijengwa kwa mawe yaliyosababishwa na athari za miamba ya asteroid ,"alisema Roswitha Feil, mkazi wa Nordlingen.

Kitu cha kushangaza ni kwamba wakazi wa Nordlingen walijua kuhusu historia hii miongo mitano tu iliyopita.

Wakazi ambao hawakujali kuhusu thamani ya nyumba zao, wanamini kuwa mji wa Nordlingen ulijengwa katika simo lilisababishwa na volkano iliyotoweka.

Hadi wanajiolojia wa Marekani Eugene Shoemaker na Edward Chao walipouzulu mji huo mwaka 1960.

Wanasayansi waliochunguza mandhari ya mji wa Nordlingen kutoka mbali wamegundua kwamba shimo lililotokana na volcano halikidhi vigezo vya Volkano.

Waliamua kuutembelea mji huo kupima taarifa zao kuuhusu na kuona kwamba mji huo uliundwa kutoka nje, sio kutoka ndani.

Haikuchukua muda mrefu kwa wanasayansi kuthibitisha nadharia zao. Inatosha kuangalia kuta za kanisa la Nordlingen.

"Vitabu vya shule vilifunza kwamba udongo uko katika muundo huu kwasababu ya Volkano ,"anasema Feil.

"Halafu ikakubalika kuwa sababu ilikuwa ni athari za asteroid , na vitabu vyote vya shule vikabadilishwa."

Muda mfupi baada ya wanajiolojia Shoemker na Chao kuutembelea mji wa Nordlingen, wanajiolojia mjini humo walifanya mahesabu na kubaini kwamba kuta za mji huo na majengo vimejengwa kwa tani 72,000 za almasi.

Ingawa mfereji wa Suez unaweza kupatikana katika maeneo mengine ya dunia ambayo yalipigwa na mlipuko sawa na huo, lakini hakuna mahali pengine palipopatwa na athari kubwa kama katika Nordlingen.

Wanajiolojia wa eneo hilo wanakadiria kuwa kuta za mji na majengo vimejengwa kwa tani 72,000 za almasi.

"Katika maeneo mengine ya dunia, inawezekana kuona udongo wa aina hiyo weny uliotokana na asteroid ukitumiwa katika shuguli za ujenzi wa majengo, lakini sio sana," anaeleza Holzl alipokuwa akitembelea jumba la makumbusho."Hapa almasi ilitumiwa katika ujenzi wa mji wote ."

Holzl ananaleza jinsi shimo la Nördlingen lilivyo la kipekee. Kiasi kwamba wanaanga Apollo 14 na Apollo 16 walitembelea eneo hilo kabla Ya safari yao ya mwezini na kushangaa ni mawe gani watarajie kuyaona katika anga za mbali n ani mawe yapi wanaweza kuyaleta duniani.

Hatahivyo kwa wakazi wa mji huo, ni jambo la kawaida kuishi na mamilioni ya chembechembe ndogo za almasi.

Mwanamke mmoja aliyetoka ndani ya kanisa aliiambia BBC , "Kwanini kitu tunachokiona kila siku kiwa cha kipekee ?!"

Holzl, ambaye alihama kutoka Munich kwenda Nordlingen, kwake anaona baridi iliyopo pale ni kitu cha ajabu sana.

"Hawafikiri kwamba ni kitu cha kushangaza. Wanashangaa kwamba watalii wanakuja hapa ," analalamika.

Holzl anaamini kwamba Nördlingen ni mji wa kipekee ulioundwa kwa jiwe la mwezini.

"Uhusiano unaounganisha mji wa Nordlingen na hali hii asilia, umekuwepo kwa miaka mamilioni. Hata ule mji mkongwe kwa kiasi gani, bado inawezekana kuuona uhusiano huu ," anasema.

"Hali ya sasa ni mazao ya kipindi kilichopita."