Cherif Souleymane: Nilikuwa mchezaji pekee mweusi Ujerumani Mashariki

Iliyochapishwa

Wakati Cherif Souleymane alisafri kutoka Guinea hadi Ujerumani Mashariki kusomea usanifu mwaka 1962 akiwa na umri wa miaka 17, hakujua kuwa ndani ya mwaka mmoja angefikia kuibadilisha soka nchini Ujerumani.

Sio tu alikuja kuwa raia wa kwanza wa Guinea kucheza ng'ambo lakini pia mmoja wa waafrika wa kwanza.

Leo hii akitajwa kuwa mmoja wa wacheza soka bora zaidi nchini Guinea, alikuwa amesafiri akitumia mpango wa masomo na Ujerumani Mashariki, wakati ikiwa nchi ya kikoministi iliyokuwa na uhusiano wa karibu na Muungano wa Usovieti.

"Nilienda kusomea usanifu, kwa msaada wa masomo wa serikali, na wala sio kwenda kujiunga na klabu ya soka," aliiambia BBC Sport Africa.

Alijikuta akicheza soka kwenye daraja la pili nchini Ujerumani baada ya kipawa chake kutambuliwa alipokuwa akichezea chuo chake huko Neubrandenburg kilomita 130 kaskazini mwa Berlin.

"Kocha akaniuliza kama nitaweza kujiunga na klabu ya Neubrandenburg nikasema ndio."

Kisha akahisi kuwa alikuwa akiwakilisha watu wote weusi nje ya uwanja.

"Nilikuwa mchezaji mweusi peke yake mashariki mwa Ujerumani wakati huo na nilijivunia hilo," anasema Souleymane ambaye saa ana umri wa miaka 77.

Mshindi pekee kutoka nchini Guinea wa tuzo la mchezaji bora Afrika, alifurahia muda wake na klabu hiyo ambapo alifahamika vyema kwenye jamii- akapendwa na mashabiki kutokana na ujuzi na uwezo wake wa kufunga mabao.

Ustadi wake kama mshambuliaji ulikisaidia klabu ya Neubrandeburg kupanda ngazi kuwa klabu bora Ujerumani Mashariki, lakini alilazimika kuondoka kwa kuwa raia wa kigeni walipigwa marufu kutoka ligi ya 'DDR-Oberliga' wakati huo.

"Niliwachezea Neubrandenburg misimu miwili na nikafunga mabao mengine", alisema.

Msimu wa kwanza tulimaliza nafasi ya 12 na nilikuwa mfungaji bora, na mwaka uliofuatia nikakisaidia klabu kushinda ligi.

"Kisha nikaondoka kujiunga na klabu hasimu cha Neustrelitz, ambapo nilikaa msimu mmoja na tukamaliza nafasi ya pili kwenye ligi."

'Watoto walinigusa kuona ikiwa ngozi yangu ina makaa'

Kila kitu hakikuwa shwari kwa Souleymane akisema kuwa alikumbwa na ubaguzi wakati akiwa nchini Ujerumani, licha kukubalika sana kwenye jamii yake ndogo.

Lakini hakuruhusu hilo kumuathiri, anasema.

"Nilikuwa mzuri na mtulivu licha kuwa ilikuwa kawaida kwa mashambiki wapinzani kunitupia matusi ya kibaguzi," anasema.

"Tatizo lilikuwa kwenye mji ambapo hakukuwa na mtu mweusi. Baadhi walikuwa wananiuliza penye nilijifunza kucheza soka, kwa sababu hawakuamini kuwa ni mchezaji mweusi alikuwa anafunga mabao.

"Watoto walikuwa wananigusa kuona ikiwa ngozi yangu ilikuwa na makaa kuhakikisha kuwa nilikuwa mtu mweusi.

"Lakini nilifurahia sana kucheza huko kwa sababu nilijulikana sana mjini na kupendwa na watu wengi kwa sababu nilikuwa mchezaji mzuri. Meya wa Neubrandenburg siku moja alinialina kwa mlo wa jioni.

"Nilikua mdogo lakini ulikuwa ni wakati mzuri, sikuruhusu kitu chochote kiniathiri, ndio sababua niliendelea kufunga mabao."

Souleymane alicheza Ujerumani Mashariki kwa miaka miatu kabla ya kurejea nyumbani huko Hafia Conakry ambapo alipata kuwa nyota wa Afrika.

Utukufu kwenye klabu majuto kwa Guinea

Taaluma ya Souleymane huko Ujetrumani Mashariki ilifikia kikomo alipoitwa na Guinea kwa mara ya kwanza kushiriki mechi ya kufuzu kwa kombe la klabu bingwa Afrika nchini nchini Ivory Coast mwaka 1965.

Badala ya kurejea Ujerumani , alirudi mji mkuu wa Guinea Conakry kwa wito wa mamlaka za nchi.

"Hivyo ndivyo masomo na taaluma yangu ya soka kwenye nchi ya Ulaya vilifikia kikomo," alisema.

"Ninajuta kuwa sikumaliza masomo yangu Ujerumani Mashariki, Hata nikajiunga na chuo kikuu huko Conakry baadaye lakini pia sikumaliza."

Lakini kurejea kwa Souleymane's nchini Guinea kulifungua njia kwa awamu nzuri katika taaluma yake ambapo alikuja kushinda tuzo kadhaa.

Alitumia taaluma yake yote huko Haifa na kuwa sehemu ya kikosi kilicachangia klabu kisiwe ndicho bora zaidi nchini Guinea tu bali kote barani Afrika miaka ya 1970.

Ni mchezaji aliyeanza taaluma kama mshambuliaji, kabla ya kurudi safu ya kati na kumalizia taaluma akicheza kama mlinzi. Ni mchezaji ayechukuliwa kama nyota kutokana na uwezo wake mkubwab wa kufunga mabao na kuandaa fursa za kufunga.

Kama mchezaji wa safu ya kati mapema miaka ya 1970 alifanya ushirika hatari na Petit Sory na N'Jo Lea.

Watatu hao waliisaidia Hafia kufika fainali tano kwa mechi za Klabu Bingwa Barani Afrika na mataji matatu ya barani Afrika mwaka 1972, 1975 na 1977.

Kwenye ushindi wake wa kwanza alifunga katika mechi mbili dhidi ya Simba ya Uganda na kumaliza kama mfungaji bora wa klabu kwa mabao manne.

Mafanikioa hayo yalimsaidia kushinda tuzo ya Ufaransa na mchezaji bora wa mwaka barani Afrika mwaka 1972.

"Kushinda tuzo la Ballon d'O ulikuwa wakati muhimu kwangu, kwa nchi yangu na wachezaji wenzangu," alisema,. "Iilituweka kwenye ramani ya soka barani."

Souleymane aliteuliwa kama mchezaji wa karne ya 20 nchini Guinea, baada ya kuisadia timu ya taifa kufuzu kwa mechi za kombe la taifa bingwa barani Afrika mwaka 1970 na tena mwaka 1974 na 1976.

Alicheza kwenye mashindano hayo yote wakati Syli Nationale walimaliza kwenye nafasi ya pili mwaka 1976 ambayo ndiyo matokeo yao bora zaidi kwenye mechi za taifa bingwa Afrika.

Alistaafu rasmi mwaka 1980.