Hatari za "kemikali za milele" tulizonazo majumbani mwetu na safari ndefu ya kuziepuka

"Kemikali za milele " zipo katika bidhaa mbali mbali za nyumbani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, "Kemikali za milele " zipo katika bidhaa mbali mbali za nyumbani
Iliyochapishwa

Hebu tazama katika bidhaa unazozitumia kila siku zinazokusaidia kurahisisha maisha yako ya kila siku... Je uliwahi kujiuliza ni kwanini vyakula havinati kwenye kikaango chako, na ni kwanini Mafuta huwa hayagandi kwenye microwave, au ni kwanini maji hayawezi kupenya kwenye jaketi lako?

Ni kemikali zile zile bandia ambazo huenda zinahusika katika utendaji wa vifaa hivi vya nyumbani. Lakini kemikali hizo kwa sasa zimejulikana na, katika baadhi ya maeneo ya dunia, matumizi yake yameanza kuondolewa kabisa.

Kundi la kemikali zinazofahamika kama " PFAS " (per and polyfluoroalkyl substances) ni kubwa. Kuna zaidi ya aina 4,700 za kemikali hii inayotengenezwa kwa kutumia fluorine.

Kuna aina 4,700 za PFAS.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna aina 4,700 za PFAS.

Zikijulikana zaidi kama "kemikali za kudumu " kutokana na uwezo wake mkubwa wa kunata kwenye bidhaa, kemikali hizi zimegundulika ndani ya maji ya kunywa, vumbi na hata katika mfumo wa damu ya binadamu.

Na ukweli ni kwamba una karibu aina zote za kemikali ya PFAS katika nyumba yako na katika mwili wako.

Matatizo ya kiafya

Ni vigumu sana kwa wanunuzi kujua ni bidhaa ipi siyo na kemikali ya PFAS

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni vigumu sana kwa wanunuzi kujua ni bidhaa ipi siyo na kemikali ya PFAS

Kemikali hizi ambazo hupatikana katka bidhaa mbali mbali, kuanzia zile zinazosindika chakula, vipodozi hadi katika samani za nyumba zimekuwa zikihusishwa na matatizo ya afya ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa maini, saratani ya figo na kuzaliwa kwa watoto wenye kasoro za kimwili.

Hatahivyo, shinikizo la walaji pekee halijajafanikiwa kumaliza viwango vya kemikali hii ya PFAS.

"Kama wewe ni mnunuzi wa mara kwa mara, ni suala gumu sana na ni kitu ambacho huwa hakizungumziwi mara kwa mara, ni kama jambo ambalo mtu wa kawaida hawezi kulielewa ," anasema Jonatan Kleimark , Mshauri wa ngazi ya juu kuhusu kemikali na biashara katika ChemSec, kampuni inayohamasisha matumizi ya kemikali salama nchini Swedish.

Kemikali hizi zimehusishwa na matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja uharibifu wa figo, maini na saratani pamoja na kujifungua watoto wenye kasoro

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kemikali hizi zimehusishwa na matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja uharibifu wa figo, maini na saratani pamoja na kujifungua watoto wenye kasoro

Halafu pia hakuna yeyote mwenye muda na hamasa ya kuandikia makampuni kuyauliza iwapo bidhaa zao zina kemikali ya PFAS, jambo ambalo baadhi ya mashirika ya serikali yalipendekeza.

Baadhi ya wazalishaji wa bidhaa huenda hata wasijue kuwa wanatumia PFAS katika bidhaa zao.

"Iwapo tunataka mabadiliko, basi tunahitaji sheria, kwasababu hilo ndilo makampuni watakalolizingatia ," anasema Kleimark.

Ni sheria gani zilizopo za udhiti kwa sasa ?

Hadi sasa, masharti ya ydhibiti yaliyopo ni madogo.

Mwezi Julai, Jimbo la Marekani la Maine lilikuw ala kwanza duniani kuweka marufuku ya mauzo ya bidhaa zenye kemikali ya PFAS- kua nzia mwaka 2030, isipokuwa wakati ambapo matumizi yake yanaonekana kutoweza kuepukika.

Kampuni ya Ikea iliondoa kemikali yote ya PFAS katika samani zake za nyumbani

Chanzo cha picha, IKEA

Maelezo ya picha, Kampuni ya Ikea iliondoa kemikali yote ya PFAS katika samani zake za nyumbani

Nchi za Muungano wa Ulaya (EU) imeweka masharti fulani na matumizi ya PFAS. Lanini wanaharakati wa mazingira na baadhi ya serikali za Ulaya zinatoa wito wa kudhibitiwa kwa PFAS kwa ujumla.

Watengenezaji wa bidhaa pia wametakiwa kutoa taarifa zaidi juu ya bidha mbadala wanazotumia.

Wanachama wa viwanda vya kemikali wanatafuta taarifa na muongozo kuhakikisha kipindi hiki cha mpito kinakuwa cha mafanikio

Baraza la viwanda vya kemikali la Ulaya (CEFIC) pia limeomba uwazi zaidi juu ya kile kinachoweza kujumuishwa kama matumizi muhimu ya PFAS.

Matumizi mbadala

Kupata bishaa mbadala limekuwa jambo rahisi katika baadhi ya viwanda kuliko vingine "Sekta ya ushonaji imekuwa mstari wa mbele katika kutafuta bidhaa mbadala," anasema Kleimark.

Mara nyingi kemikali hutumiwa kutengeneza nguo zinazozuwia maji kupenya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mara nyingi kemikali hutumiwa kutengeneza nguo zinazozuwia maji kupenya

Hatahivyo baadhi kampuni zimebadili bidhaa PFAS kwa bidhaa nyingine ambazo ni bora kwa afya ya binadamu lakini ambazo zina madhara sana kwa sayari, kama vile nguo zinazotengenezwa kwa plastiki.