Kwanini Chelsea inaonekana kuwa timu isiyozuilika?

Iliyochapishwa

Mbio za kuwania taji la ligi kuu England ndio kwanza zimeanza, lakini Chelsea wanaonekana kama watakuwa wagumu kuzuilika.

Kikosi hicho cha Thomas Tuchel, kinaonekana kimepania hasa wakati huu, lakini wanaonekana kufanya hivyo tangu achukue mikoba Januari mwaka huu.

Hata wanapoonekana hawachezi vizuri, ama mambo hayawaendei vizuri kama ilivyotokea Anfield mwezi uliopita alipolimwa kadi nyekundu mlinzi wake Reece James - Chelsea walionekana bado imara.

Kama walivyooyesha kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Tottenham ugenini jumapili hii, 'the Blues' wanakikosi imara na meneja mzuri.

Tuchel alifanya mabadiliko wakati wa mapumziko, kwa kumuingiza N'Golo Kante akimtoa Mason Mount, mabadiliko yaliyowapa nguvu Chelsea kwenye eneo la kiungo a kuruhusu mabeki wake wa pembeni hasa Marcos Alonso, kusogea mbele zaidi.

Atukuona hilo katika kipindi cha kwanza, lakini wakaonekana imara zaidi kipindi cha pili. Walikuwa wazuri kila idara, na walippata bao lao la kwanza, ilikua tu ni magoli mangapi watafunga na sio mangapi watafungwa.

Ingeweza kuwa magoli 6 au 7, ingeweza kuwa hivyo kama sio makosa ya ufungaji ama uzuri wa golikipa kwenye kuzuia.

Matokeo mengine bora ya Tuchel ugenini

Tuchel anataka maboresho Chelsea, licha ya ushindi wake dhidi ya Spurs

Wakati Spurs ilionekana kuwa tishio katika kipindi cha kwanza, walinzi wote wa kati wa Chelsea walionekana imara zaidi hasa Thiago Silva, ambaye alionekana kama mchezaji bora wa Mechi hiyo. Aliwapa bao la kuongoza na alionekana anajua nini anachokifanya.

Ndio kwanza ni mchezo wa tano tangu msimu mpya uanze, lakini Chelsea tayari ameshacheza ugenini dhidi ya Arsenal, Liverpool na Tottenham na kufanikiwa kupata alama 7 katika michezo hiyo mitatu.

Walipoteza alama katika mchezo wa sare dhidi ya Liverpool, wakiwa pungufu wakicheza na watu 10 katika kipindi chote cha pili. Hilo linakuonyesha walivyo bora kiakili na namna wanavyoweza kuzuia na kupata matokeo.

Kabla ya msimu mpya kuanza, niliichagua Chelsea kuibashiria ubingwa na nilidhani Romelu Lukaku anaweza kuleta tofauti kwenye eneo la ushambuliaji baada ya kuonekana kupoteza nafasi nyingi za mabao msimu uliopita.

Lukaku sio sababu pekee ya kuonekana tishio, walishinda ligi ya mabingw aUlaya mwezi Mei bila yeye, lakini kuwasili kwake kunamaanisha kwamba hawana udhaifu kwenye muunganiko wa timu yao, lakini pia wanakikosi bora na kipana pia.

Kumuingiza mchezaji mzuri kama Kante kutoka benchi dhidi ya Spurs ni mfano mwingine wa ubora wao. Meneja wao hana tu uwezo wa kuona kwamba sasa mambo hayaendi vizuri uwanjani, lakini pia ana wachezaji bora walioko benchi ambao wanaweza kubadili mambo na kuleta utofauti wanapoingia.

Mtihani unaofuata kwa Chelsea ni dhidi ya Manchester City utakaopigwa nyumbani Stamford Bridge siku ya Jumamosi, lakini hilo halionekani kuwashitua.

Wakiwa chini ya Tuchel waliwatwanga City mara tatu msimu uliopita t ikiwemo mchezo wa

Alama tatu muhimu kwa Man Utd

Ushindi 2-1 wa Manchester United dhidi ya West Ham mapema Jumapili hii haukuonekana wa wazi, lakini ulikuwa aina ya ushindi muhimu kwa timu hiyo , ambayo ilishambuliwa kwa lawama baada ya katikati ya wiki kuchapwa katika mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Makosa ya Jesse Lingard yaliwazawadia bao vijana wa Young Boys na kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya United. Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer alitupiwa lawama kwa mabadiliko ya wachezaji aliyoyafanya mwishoni mwa mchezo huo, lakini walirejea na nguvu na kushinda mwishoni mwa wiki dhidi ya West ham pale London Stadium.

Solskjaer alionekana kutumia akili kwa kufanya mabadiliko mengine dhidi ya West Ham wakati huo matokeo yakiwa sare ya 1-1.

Mabadiliko haya wakati huu yalimlilipa. Kama alivyofanya Jumatano wa kumuingiza Lingard na Nemanja Matic - ilikuwa Matic aliyempa pasi Lingard aliyefunga bao la ushindi. Baada ya hapo hakuna aliyehoji kwa nini mabadiliko hayo ya Solskjaer.

Badala yake, maneno ni kuhusu marefarii. Ilikuwa jambo la kushangaza kwa maamuzi ya marefarii na VAR yalioonekana mengi kutokuwa sawa.

West Ham walipaswa kupewa penati nyingine, na United walipaswa pia kupewa penati moja ama mbili, zote kutokana na kutendewa madhambi Cristiano Ronaldo ambazo zilionekana za dhahiri kabisa.

Ilikuwa siku ambayo kama maamuzi yangeenda sawa, huenda yangeigharimu Manchester United, lakini ikageuka ushindi na alama muhimu tatu kwa United.

David de Gea alikuwa mfalme wao kwa kuokoa mkwaju wa penati dakika ya mwisho ya mchezo, lakini uikuwa uamuzi wa kushangazwa uliofanywa na meneja wa wapiga nyundo (West ham) David Moyes wa kumuingiza Mark Noble kwa ajili ya kupiga penati tu.

Kabla ya hapo Noble hakuwa amegusa mpira na hakuwa hata amepasha misuli joto. Anajua alikuwa ana rekodi nzuri kwenye upigaji wa penati, lakini ulikuwa ni mchezo wa pata potea kwa Moyes uliomgharimu.

Vipi kuhusu wa timu nne bora za juu 'Top four'?

Liverpool nayo imeanza vizuri msimu huu mpya wa ligi kuu, wakiwavutia wengi.

Tofauti na washindani wengine wanaowania ubingwa wa ligi kuu, wekundi hao wa Anfield, hawakufanya usajili wowote mkubwa wa kutisha wakati wa majira ya joto - mchezaji pekee wa maana waliomsajili ni mlinzi Ibrahima Konate aliyesajiliwa kwa ada ya £35m

Kikosi hicho cha Jurgen Klopp huwezi kukipuuza, hasa wakati huu ambapo beki wake mahiri Virgil van Dijk amerejea baada ya kuwa nje kwa majeraha na kuonyesha kwa nini ni mchezaji muhimu.

Mpaka sasa City ndio wamepoteza alama zaidi ukilinganisha na washindani wake. Sare ya nyumbani Jumamosi hii dhidi ya Southampton yalikuwa matokeo mabaya ukilinganisha kiwango cha Liverpool dhidi ya Crystal Palace, Ushindi wa United na kile walichofanya Chelsea ugenini kwa Spurs.

Ubingwa wa ligi kuu msimu huu, itakuwa kati ya timu hizi nne, Lakini Chelsea inabaki kuwa timu ya kutazamwa zaidi. Hawafungiki kirahisi.