Fahamu jinsi washawishi wa mtandaoni Kenya wanavyolipwa ili kueneza uvumi

Chanzo cha picha, Getty Images
Kukabiliana na washawishi wa mtandaoni nchini Kenya- ambapo hivi karibuni imebainika kuwa wamelipwa kwa ajili ya kutangaza taarifa feki ni sawa na kukabiliana na 'vita visivyo rasmi', anakiri mwanaharakati aliyehusika katika mapambano hayo kisheria kuzuia mabadiliko ya katiba.
"Majadiliano hayo yanaweza kuwa makubwa hadi yakakuchosha," Daisy Amdany aliiambia BBC kuwa shambulio hilo la Twitter llinawahusisha wale walioko na kesi hiyo mahakama.
Malumbano hayo yalisababisha mwanaharakati mmoja kuamua kujiondoa kwenye kampeni "na watu wapatao watatu waliamua kuchukua mapumziko kwa sababu ya kuongezeka kwa matusi na taarifa zisizo na ukweli ambazo walikabiliana nazo", alisema.
Bi Amdany alikuwa akijibu ripoti ya taarifa ya shirika lisilo la kiserikali Mozilla Foundation ambayo inafutailia tatizo hilo
Inaonesha jinsi wafadhili vivuli walivyounda jeshi la washawishi wa Twitter kuhamasisha kampeni ya taarifa za uongo kwa ajili ya serikali na kuunga mkono muswada wa marekebisho ya katiba ya maridhiano inayojulikana kama BBI.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika kati ya mwezi Mei na Juni mwaka 2021, walikuwa wanalipwa kuwadhalilisha waandishi , majaji na wanaharakati kwa kutumia jukwaa la Twitter.
Haishangazi kwa Twitter kulengwa kwa taifa la Afrika Mashariki ambalo lina kelele nyingi mtandaoni, jumuiya hiyo inayojulikana kama Wakenya kwenye Twitter (#KoT).

Utafiti unaonesha biashara ya taarifa feki kuwa na faida, na washawishi wa kukodisha kisiasa hulipwa kati ya $10 (£7) na $15 kushiriki katika kampeni tatu kwa siku.
Baadhi ya washawishi waliweza kufanikiwa kulipwa hadi $250 kwa mwezi.
Malipo yanalipwa moja kwa moja kupitia simu zao kupitia M-Pesa.
Wafuasi wa mtandaoni ambao walihojiwa walikataa kusema nani huwa anawalipa lakini mmoja aliwaambiwa watafiti kuwa mara nyingine fedha hutolewa hata kabla ya kampeni au mara nyingine baada ya uchaguzi.
Wale walikuwa nyuma ya kampeni hizo walianza kwenye makundi ya WhatsApp ambayo yalikuwa yanatumika kutuma maudhui au maelezo.
Waliambiwa kutangaza kwa kuweka kile ambacho kinaongoza kufuatiliwa kwenye mtandao Twitter.
Lengo lake ilikuwa kuwapotosha watu katika kufikiria maoni ambayo yalikuwa maarufu - hii ikiwa sawa na kuwalipa watu kuhudhuria mikutano ya kampeni za siasa", utafiti umesema.
Akaunti zilifungiwa
Twitter ilidaiwa pia kunufaika kwa kuweka matangazo na kampeni za taarifa ghushi.
Wakala ambao wanauza matangazo kwenye Twitter nchini Kenya wanatangaza kwa kulipa $3,500 kwa siku , ripoti imesema.
"Ikiwa hatukuweza kudhibitisha kwa uhuru jinsi malipo ya twitter yanavyofanyika katika ripoti yenu lakini tunaweza kuthibitisha kwa mtandao mmoja au zaidi ambao unaratibu akaunti hizo," Twitter ilijibu.
Akaunti karibu 100 zinazomilikiwa na washawishi wa mtandaoni nchini Kenya zimefungiwa na kampuni kubwa ya teknolojia kwa kukiuka masharti ya sera za jukwaa.

Chanzo cha picha, Twitter
Mashambulio dhidi ya majaji yalikusudiwa kudhalilisha uhuru wao, kwa kutumia hashtag ikiwa ni pamoja na #AnarchistJudges, #JudiciaryRevenge, #JudicialPayback and #Justice4Sale.
Wastani wa kampeni moja hivi ya kutoa habari za uongo kila siku mbili ilibainiwa kuwa wakati wa kipindi cha hukumu au kabla na baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu mnamo mwezi Mei.
Majaji wamebaini kutoa mapendekezo ya BBI kutofuata sheria , katiba au utaratibu, maamuzi ambayo yalipelekwa mahakamani mwezi Agosti ingawa mapambano bado yanaendelea wakati mwanasheria mkuu klipinga uamuzi huo katika mahakama ya rufaa.
Ilianzia kwenye Twitter kwa picha iliyotengenezwa inayoonesha wale waliofungiwa kwenye BBI, ambao walihoji kuwa kubadilishwa kwa mchakato huo hakukufuata utaratibu na wala katiba.
"Waliongelea jinsi tusivyojali kuwa na amani," alieleza bi. Amdany, kwa wale walioanzisha harakati za Linda Katiba mwezi Februari.
"Kuna wakala wa kigeni waliolipwa kudhoofisha taifa au ni raia ambapo kuna watu ambao hawawajibiki, jamii zisizokuwa na uzalendo au watu tu wanaopenda kupiga kelele.
"Mambo mengi yametumika kuhamasisha chuki na kupuuza nia na mwenendo wa watu wanaohamasisha kampeni fulani ."
Wanaharakati pia walipewa taswira ya kufadhiliwa na makamu wa rais William Ruto - mpinzani mkuu wa BBI.
Baadhi ya akaunti zilitumia picha za kupendeza za wanawake kama picha za wasifu kuwashawishi wanaume kuwafuata.
Hofu ya demokrasia
Ripoti ya taasisi ya Mozilla imebaini ushahidi mdogo kuhusu kile kinachopelekea taarifa za uongo kuhusu maoni ya watu katika mchakato wa BBI ambao uko mahakamani.
Hatahivyo, washawishi waliokodiwa wameweza kuwatisha watu kujadili kwenye Twitter, wanaharakati wanasema sasa wanajihami wenyewe katika jukwaa hilo.

Chanzo cha picha, AFP
"Eneo ambalo lilikuwa zuri kwa mijadala sasa limebadilika na kuwa sumu kabisa.
" Sauti zinazopingana mara nyingi zinaweza kufanya jeshi lote kujumuisha maoni yao, "mwanaharakati mmoja alinukuliwa.
Bi Amdany amekubali - alikubali kufuta akaunti yake binafsi ya Twitter kwa sababu ya mvurugiko huo mtandaoni -ingawa anaongoza taasisi ya haki za wanawake , imani ya wengi ipo Twitter bado.
Kuna hofu kuwa mbinu hizo zinaweza kuwa na athari kuelekea uchaguzi mkuu Agosti 2022.
Vurugu kubwa ziliibuka katika uchaguzi uliopita lakini Twitter ilikuwa eneo ambalo liliwapa fursa wanasiasa kujadili siasa.
"Jukwaa la Twitter linaweza kuchochea ghasia," utafiti umeonya.
Mtaalamu wa mitandao ya kijamii Samuel Kamau amekubali kuwa mambo yamebadilika.
"Awali, mitandao ya kijamii ililazimishwa kwa uzuri kuchochea demokrasia ," aliiambia BBC.
"Lakini kadri tunavyoenda , watu wamejifunza jinsi ya kuitumia mitandao na kudhibiti maoni ya umma. Swali sasa ni je mitando ya kijamii ni mizuri katika kuchochea demokrasia.."
Kwa Brian Obilo, mwandishi msaidizi wa ripoti , suluhisho linaweza kupatikana kwenye Twitter kwa kusitisha taarifa kuvuma wakati wa uchaguzi.
"Twitter inaweza kuweka mtu wa kufuatilia katika nchi mbalimbali kuangalia mada ambazo zinavuma ,"aliiambia BBC.















